Dawa ya fungus za miguuni

Nasumbuliwa na fungus kwa Muda mrefu sana huwa navumilia na kwenda nao kibishi. Kwa sasa Hawa fungus wananisababishia vidonda kwa juu ya mguu na vikipona vinahama sehemu nyingine.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati.
JITIBU TATIZO LA FANGASI ZA MIGUUNI KWA NJIA ZA ASILI






Juisi ya ndimu.

Fangasi za miguuni ni tatizo linalo wakabili watu wengi duniani. Kama una sumbuliwa na tatizo la fangasi za kwenye miguu unaweza kujitibu kwa kutumia njia za asili kabisa.
Yafuatayo ni maelezo ya jinsi ya kujitibu fangasi za miguuni kwa njia za asili.
1. MAHITAJI
i. Majivu robo kilo
ii. Juisi ya ndimu milimita mia mbili hamsini ( Kikombe kimoja )
iii. Sufuria
iv. Kopo au chupa ya plastiki.
MATAYARISHO
Chukua majivu yako, weka kwenye sufuria kisha changanya na juisi ya ndimu, halafu koroga hadi ichangamane, kisha hifadhi kwenye chupa au kopo la plastiki..
MATUMIZI : Nyunyiza dawa yako kwenye sehemu iliyo athirika na fangasi. Fanya hivyo mara mbili kwa siku a subuhi na jioni hadi tatizo lako litakapo isha.chanzo.Neema Herbalist & Nutrtional Foods Clinic: JITIBU TATIZO LA FANGASI ZA MIGUUNI KWA NJIA ZA ASILI
 
Nasumbuliwa na fungus kwa Muda mrefu sana huwa navumilia na kwenda nao kibishi. Kwa sasa Hawa fungus wananisababishia vidonda kwa juu ya mguu na vikipona vinahama sehemu nyingine.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati.
Paka utomvu wa papai bichi kwenye sehemu yenye tatizo.
 
pic+fungus.jpg

Mara nyingi ngozi ya miguuni hasa katika ngozi ngumu ya nyayo na katikati ya vidole, ndizo zinazopatwa sana na vimelea wa fangasi.

Wanaume wanaoishi katika maeneo yenye joto la wastani mpaka la juu ni moja kati ya kundi la wanaokabiliwa na maambukizi ya fangasi wa ngozi ya miguuni, kitabibu hujulikana ‘Tinea pedis.’

Mara nyingi ngozi ya miguuni hasa katika ngozi ngumu ya nyayo na katikati ya vidole, ndizo zinazopatwa sana na vimelea wa fangasi.

Uwapo wa unyevunyevu, joto na giza ni mazalia mazuri ya fangasi wa miguuni.

Wanaume ambao wako katika hatari ya kupata fangasi za miguuni ni wale wenye dosari ya nyayo ya miguu kuwa na kiasi kikubwa cha tezi zinazotoa jasho nyayoni. Vilevile, wenye kinga dhaifu, wanaougua kisukari, wanaoishi maeneo yenye joto kali na wale wanaovaa viatu kwa muda mwingi.

Maambukizi haya yanaweza kuwa chanzo cha kupata fangasi maeneo mengine ikiwamo katika sehemu za siri, viganja vya mikono na mwili mzima.

Uwapo wa fangasi miguuni unaweza pia kumhatarisha mwathirika kuvamiwa na bakteria rafiki wa juu ya ngozi ambao wakipenya ndani ya ngozi huleta madhara.

Vimelea wa fangasi ni mojawapo wa wanaoweza kusambaa na kumpata mwanadamu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kugusana na vitu vilivyotumiwa na mwenye vimelea wa fangasi.

Katika maisha ya kila siku mara nyingine watu huweza kuvaliana soksi na viatu; hii ni mojawapo ya njia zinazoweza kueneza maambukizi ya fangasi wa miguuni kwa wanaoishi katika mazingira ya pamoja.

Si hivyo tu, bali pia kuvaa viatu na soksi za mitumba ambavyo pengine vimetumiwa na mtu mwenye maambukizi ya fangasi, inaweza pia kuwa sababu mojawapo ya maambukizi ya fangasi za miguuni.

Vilevile kutumia pamoja sakafu au vitu vilivyokanyagwa ikiwamo mazulia, mabwawa ya kuogelea, vifaa vya mazoezi vilivyotumiwa na mtu mwenye vimelea.

Dalili kubwa ya fangasi ni muwasho unaokulazimisha kujikuna na kujihisi raha au utulivu unapojikuna, harufu nzito ya kuoza katika miguu, kumomonyoka ama kulika kwa ngozi yenye fangasi.

Pia kuvuja kwa majimaji yenye kuteleza na harufu nzito, maumivu au kuhisi kuchomachoma baada ya kuchubuka na pia mara nyingine kuhisi kuwaka moto.

Ugunduzi wa fangasi wa ngozi ya miguu ni rahisi, huhitajiki kwenda maabara, wahudumu wa afya wanaweza kugundua kwa kupata historia ya dalili na kutazama kwa macho.

Mara nyingine unaweza usihitaji kupewa dawa za kukabiliana na fangasi wa miguu, elimu ya afya inaweza kukubadili tabia na ukadhibiti fangasi wa ngozi ya miguuni bila dawa.

Njia ya kukabili fangasi

Moja ya njia rahisi za kukabiliana na kujikinga na fangasi ni kubadili mienendo ya kimaisha ikiwamo kupenda kuwa msafi wa mwili pamoja na kufua nguo zinazovaliwa ikiwamo soksi ambazo wengine huzivaa kwa muda mrefu bila kuzifua.

Tumia soksi zenye asilimia nyingi ya pamba ili kuweza kunyonya jasho la miguuni, kutumia kitambaa safi au taulo dogo kwa ajili ya kukaushia maji baada ya kuoga au unapotoka kazini, matembezini na mchezoni.

Mara tu baada ya kutoka katika shughuli zako vua viatu vya kufunika na tumia viatu vya wazi, kausha kwa kitambaa kikavu maeneo ya miguuni katika upenyo wa vidoleni.

Matibabu ya dawa za fangasi za kupaka zilizo katika mtindo wa poda zinaweza kutumika kutibu, kwa fangasi sugu, dawa za kumeza zinaweza kutolewa. Kama kukiwa na maambukizi mchanganyiko na bakteria dawa za antibiotic zinaweza kutolewa.

Mara nyingine fangasi zinaweza kupata nyufa za vidoleni zikatengeneza vidonda ambavyo vinaweza kupata maambukizi wa bakteria ikiwamo wale wa tetenasi.

Hakikisha pia ukiwa una tatizo hili kiasi cha kufikia kupata vidonda miguuni, hakikisha unapata chanjo ya tetenasi kama hukuwahi kuchomwa.

Fangasi za miguuni ni ugonjwa kama magonjwa mengine, hivyo wanaogua wasipuuze wakidhani ni tatizo dogo.

Wanaogua tatizo wafike katika huduma za afya mapema kwa ajili ya ushauri na matibabu.

Chanzo:Mwananchi
 
Na Mimi ninafangasi sehemu ya siri , kwenye korodani, Nimetumia Dawa nyingi kama vile gentrisone,sonaderm ,Vidonge kama vile flucan, predisoline, n k lakini hali bado, Ngozi inakuwa inatoka magamba magamba yaani kama nyoka anavyojitoaga magamba, Tatizo lina miezi minne sasa, Hospital nimetembea lakini bado.Mwenyewe Dawa anisaidie
Ukishawahi kupiga punyeto kwa muda mrefu?
 
Habari zenu!! Jamani nasumbuliwa na fangasi miguuni nishatumia dawa za hospital lakin tatizo likipona linarudia tena... je nikitumia kwa kupaka mafuta ya taa au spiriti nitaweza kupona??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu!! Jamani nasumbuliwa na fangasi miguuni nishatumia dawa za hospital lakin tatizo likipona linarudia tena... je nikitumia kwa kupaka mafuta ya taa au spiriti nitaweza kupona??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu!! Jamani nasumbuliwa na fangasi miguuni nishatumia dawa za hospital lakin tatizo likipona linarudia tena... je nikitumia kwa kupaka mafuta ya taa au spiriti nitaweza kupona??

Sent using Jamii Forums mobile app
Infection ipo kwenye damu,tumia vitunguu swaumu ni Sawa kumeza na kupaka baada ya kuisaga maji yake,kunywa na kupaka Kwa mwezi mmoja hata miwili ukiweza,Ila Kama una BP ya kushuka usitumie kitunguu swaum

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu!! Jamani nasumbuliwa na fangasi miguuni nishatumia dawa za hospital lakin tatizo likipona linarudia tena... je nikitumia kwa kupaka mafuta ya taa au spiriti nitaweza kupona??

Sent using Jamii Forums mobile app
fda6cf87ea3ee6a46a35044c0d03b577.jpg

dawa hii itakua msaada kwako, ni ya uhakika kupona tatizo lako kwa kuipata nicheki pm ,,, polee na karibu kwa tiba
 
Kidole changu mguu wa kushoto, fangasi wataondoka nacho, ngoja nipake hiyo ndimu nione kesho asubuhi kama nitaamka nimepona
 
Back
Top Bottom