BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,820
20240312_132129.jpg
20240312_132126.jpg

20240312_132123.jpg

20240312_132119.jpg


Pia soma: NHIF yarudisha dawa 178 zilizoondolewa
 
Huo mfuko wa bima ya afya kwishinei. Waziri mkuu anapambana na muhasibu wa Serikali za mitaa aliyekula milioni 200 anawaacha watumishi waliomega na kujikopesha zaidi ya bilioni 40 za mfuko wa bima ya afya ambazo ni bajeti ya kutosha ya dawa na vifaa tiba
 
Watu tukisema tunaonekana wabaya na watu tunapinga kila kitu 😀😀😀🫣🫣🤐🤐🤐🤐🤐..

Mama anauchapa Mwingi sana.. Sio?

Unaondoa Aminophiline Tabs na Injection, Beclomethasone +salbutamol inhaler ,Beclomethasone inhaler,Budesonide +Formeterol inhaler
Unategemea Mgonjwa wa Pumu "Emergency case" utamtibu kwa Dawa ipi kwa ngazi za Chini?

Unaondoa amlodipine,Atenolol,Valsatan,Atenolol+Nifedipine, isosorbide mononitrate tabs,
Metformin 400 +Glibenclamide 2.5mg..

halafu kutea kujisifu kuwa wagonjwa wa Presha na sukari na wenye matatizo ya moyo kutibiwa Kwa Kitita kipya Sasa kwa dawa zipi?

Kwa malaria unaondoa..

Artemether inj 40mg/0.5ml
Artemether lumefantrine syrup
Artemisinin & piperaquine tabs
Artesunate & Mefloquine tabs
Artesunate &Metakelfin tabs
Artesunate &Naphthoquine tabs
Artesunate inj 120mg, 30mg
Artesunate rectal suppositories
Quinine all dosage forms

Sulfamethoxypyrazine & Pyremethamine tabs (SP)

Nado huridhiki unaondoa Chloroquine tabs for sickle cell prophylaxis "Unawatakia Nini wagonjwa wa Sickle cell"
Kwamba mmewachoka sasa mnataka wapungue???

Halafu kuna Mtu anakuja anashout Kitita kimeboreshwa M****** zake ataona watu watakavyokipata cha Mtema kuni..
wallah hakuna Mchawi
 
Kama utakuwa na uwezo kidogo Bora kujiunga na bima za makampuni binafsi za AAR ama nyingine tu, hizi bima zetu za kinyonge za NHIF tutajikuta tunafia hospitali Kwa kukosa dawa 🙌😭

Nchi imegeuka ya Matajiri hii saivi
 
kuna mtu utamsikia akisema wanawake wamuunge mkono mwanamke mwenzao swali ni je? yeye anawaunga mkono na uungwaji mkono ndio kama hivi mtu wa kijijini mwenye bima hapati huduma unatarajia nn sasa
 
Huo mfuko wa bima ya afya kwishinei. Waziri mkuu anapambana na muhasibu wa Serikali za mitaa aliyekula milioni 200 anawaacha watumishi waliomega na kujikopesha zaidi ya bilioni 40 za mfuko wa bima ya afya ambazo ni bajeti ya kutosha ya dawa na vifaa tiba
Ukute na yeye kwenye mgao wa hizo bilioni 40 yumo...
 
Hii nchi jamani mbona tunazidi kuzama shimoni kila siku.Sasa umuhimu wa bima ni nini kama madawa hayo yote yameondolewa ?
 
Lakini Bima ni ajiri ya dharula, unaweza ugua na hauna kitu! Sasa ukiambiwa kununua tena dawa na vifaa maana yake nini?
 
Back
Top Bottom