DAS Kahama: Wanawake acheni mikopo ya kausha damu chukueni mikopo ya Samia

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
1,029
1,667
Wanawake wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuchangamkia fursa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri bila riba na kuachana na mikopo umiza.

Rai hiyo nimetolewa na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Glory Absalum ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mboni Mhita kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ambapo kimkoa yanafanyika katika Kata ya Bugalama halmashauri ya Msalala.

DAS Absalum amesema " Tuachane na kausha damu Mama Samia ameleta mikopo ya asilimia 10 twende tukakope kupitia halmashauri, maafisa maendeleo ya jamii wapo kata zote kwa ajili ya kutoa elimu na vikundi vinaundwa"

Baadhi ya Wananwake waliohudhulia maadhimisho hayo wameipongeza serikali kwa kuleta mikopo hiyo isiyokuwa na riba kwani kwa kipindi kirefu mikopo umiza imekuwa ikiwarudisha nyuma badala ya kuwainua kiuchumi.

Naye, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo Julika Joel amesema wametenga zaidi ya TZS. bilioni moja na milioni mia tatu kwaajili ya kuwakopesha Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu na mpaka sasa wamekopesha takriban Milioni 317 tu.

Kila ifikapo March 8 kila mwaka dunia huadhimisha siku ya wananawake ambapo kwa mkoa wa Shinyanga maadhimisho hayo yameanza Tarehe 4-6 Machi, 2025 yakiwa na kauli mbiu isemayo "Wanawake na Wasichana 2025 tuimarishe usawa nauwezeshaji"
 
Vijana msi hangaike kuandaa ma katiba wala mipango kazi kwenye iyo Mikopo ya asilimia 10% kama mna jijua sio makada ,ni hivi izo pesa wana nunua pikipiki zile za kijani na kuwa kopesha makada
 
Back
Top Bottom