DART mbioni kupoteza hadhi yake katika jiji la Dar

Ovyo ovyo ovyo, kukimbizana na maendeleo wakati watu wakuleta maendeleo wanapoteza masaa kibao ( mengi ) kwenye vituo vya mwendokasi!!!, hii ni shida!. Jipangeni kwa upya wakati huo daladala zirudushwe na sisi abiria tuchague!. "Ushindani wa kihuduma "
 
'



Mtu wa maxmalipo na mtu wa udart mkipeana za uso.

Nina mdogo wangu tunashea baba, ni keshia kituo fulani. Kaniambia leo kafatwa na watu wa udart na walikuwa wanapita vituoni, wanakwambia usaini au kama hutaki huna kazi.
Vituo ambavyo vinauza tiketi za UDA zile za njano za manual ni vituo ambavyo makeshia wamegoma kusaini kwa sababu bado wana mkataba na maxcom, na udart ikawaambia watoke vituoni na kwa kuwa wao ndio wana namba/ majina ya kuingiza ktk computer za tiketi, basi udart imebidi wauze tiketi za uda sababu system wameshindwa ifungua. Haya ni maneno ya mdogo wangu. Yeye ni muajiriwa wa maxcom ila eneo la kazi ni udart project, mkatabà wake ndio wasema hivyo. Na pia ni kweli udart ndio inawalipa mishahara kupitia maxcom ila inasikitisha mpaka leo tarehe 24.4.2018 hawajalipwa mshahara wa mwezi wa tatu hao makeshia ilhali wale wa getini ambao nao ni waajiriwa wa moja kwa moja wa udart wamelipwa. Kama ni waajiri wwa udart kwa nini wao wanazinguliwa kupata haki yao na wengine wanalipwa??
NHIF udart hawajawahi wawekea, LAPF ndio kabisa. Kwa maelezo yake haya ni malipo yaliyotakiwa kufanywa na udart ila wanazingua. Mdogo wangu ni mcha Mungu, chonde chonde, aaiwekwe kwenye mazingira ya kumshawishi aibe maana naamini haibi.

Alafu hivi hao unaosema wanaiba, jiweke wewe kwenye nafasi zao, anakukusanyia hela ila humlipi miezi 2 sasa. Watawapiga sana!!
Hao udart ndo walichofanya
 
Wewe unatumia huu usafiri !? Comment yako inaonesha wewe una hisa au utakuwa demu Wa dereva Wa mwendokasi yaani unapandia mlango Wa mbele.
Poa. Upo kwenye transition maana maxcom walivyotoa sasa TTCL ndo watasimamia.
Mradi hauwezi kufa kiboya kama unavyofikiri wewe na wakati kuna gari zaidi ya 70 zitaanza kazi soon.
Tanzania kitu kikislow kidogo tu kelele.
Jiulize toka umeanza kuishi graph yako inaenda tu linearnly?
 
Ulitaka achangie kwa kukufurahisha wewe!? Wewe ni nani kwani!?
Nadhani wewe huna akili na naka unazo basi hazikutoshi na kama zinatosha basi unatumia ubongo wa masikioni. Huwa sipendi kuchangia ila wewe umeniudhi aisee ila sidhani kama wewe ni mtanzania.
 
Kazi imewashinda nyie vichwa Maji. Itabidi SUMATRA waruhusu daladala zurudi kufanya kazi. Watu wachague wenyewe.
Gari ni mpya zimeongezwa kuboost mahitaji halisi. Kilichokuwa kinaendelea ni kuziingiza kwwnye mfumo wa eticketing na routing ndo mvua zikaanza. Tegemea soon kuziona
 
Tokea mwanza nilijua tu watafeli sababu mfumo wanaotumia ni wakizamani na unahitaji watu wengi.Kwann wasingeweka automated machine za kukatia tiketi?,unaingiza mpunga inatoa tikiti na chennchi kama wafanyavyo wachina
 
Kero tunayoipata watu wa Kimara Mungu anajua sasa hivi hatuna tofauti na gunia la viazi au cabbage na carot tunavyolundikwa kwenye hayo mabasi.......... yaani ni kero isiyokuwa na maelezo nawaambia.

Maonevu yasiovumilika wajaribu kuruhusu basi za kawaida kama wataona mtu kwenye huo mwendokero wao
Mi nasubiria salio liishe ktk card, ntahamia MABASI yetu ya zamani. Potelea Mbali
 
Maximalipo fans
Acha ushabiki, sio jambo zuri kwa taifa hili. Nimefuatilia comments zako, haupo objective kabisa. Usijiangalie ww tu, jaribu kuangalia maslahi mapana ya taifa na sio kusaliti taifa lako na nafsi yako kwa pato dogo.
 
Gari ni mpya zimeongezwa kuboost mahitaji halisi. Kilichokuwa kinaendelea ni kuziingiza kwwnye mfumo wa eticketing na routing ndo mvua zikaanza. Tegemea soon kuziona
Mkuu hiyo soon ulikuwa unamaanisha ni baada ya muda ganiii??
 
Naomba uzi huu msiuchanganye na ule wa maoni ya udart.

Updates.

1. Leo kwa mara ya kwanza udart wameanza kutumia tiketi za daladala.

2. Wafanyakazi wa maxcom waanza kulazimishwa kusign mikataba mipya na udart wakati bado wana mikataba na maxcom.

3. Udart wanalazimisha ttcl wakatishe tiketi wakati Dart bado hawaja tangaza mzabuni mpya atakaye katisha tiketi kwa mkataba mpya.

4. Ttcl hadi leo hawajatoa tamko lolote kuhusiana na tamko la udart kama wapo tayari kufanya kazi hiyo.


Inavyo onekana udart wanafanya siasa kutaka serikali ukwamishe mchakato wowote wa kupata kampuni itakayo fanya kazi ya kukusanya mapato ya usafiri wa mwendo kasi kwa kupitia siasa za kujipendekeza hasa ukizingatia sera ya sasa (nationalism) kushika kasi. Jiulize ttcl watapewaje kazi bila kupitia taratibu za zabuni?

Inasemekana DART walipendekeza mfumo mpya wa ukusanuaji mapato na ulipaji kwa operators ambao utahitaji operator kulipwa kwa km badala ya mfumo wa sasa ambao hata operator akitoa basi moja bado anajilipa kiasi kile kile cha fedha.


Mfumo huu unapingwa sana na udart na inasemekana ndio chanzo cha wao kuingilia majukumu ya dart kwa kupiga siasa kama zinavyo endelea muda huu.

Ushauri wangu, dart simamieni majukumu yenu bila kujali mtu, hata kama anatoka kijiji kimoja na mwenye mbwa.


Dart ni wakati sasa mtafute operator mwingine ambaye ataleta ushindani kwa lengo la kuboresha huduma katika jiji la dar es salaam.

Serikali wakikubali siasa zinazo endelea , ni sawa na kukubali kupakwa matope kwa faida ya wengine.

Dar es salam oyeee.
Yametimia
 
Back
Top Bottom