Dar to Pretoria na gari private: Ushauri na changamoto zake plus gharama

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,074
3,743
Wakongwe salaam,

Nina mpango wa kuwasha ndinga kutoka Dar mpaka Pretoria South Africa hivi karibuni.

Dhumuni hasa kuna mizigo miwili mitatu nataka nikafanye shopping kwa ajili ya biashara (mobile phones)


Mizigo hiyo nina mpango wa kusafiri nayo kwenye gari kwa maana niweke kwenye buti.

Lengo la kwenda na gari ni kwanza kufanya utalii wa Africa lakini pia kuendesha kwa mwendo mrefu maana passion yangu kubwa ni kuendesha mwendo mrefu.

Gari ninayotaka kuitumia ni Toyota Mark X yenye cc 2500.

Sasa wakongwe naomba ushauri katika nyanja zifuatazo;

(1) Mafuta niandae kiasi gani kwenda na kurudi (max).

(2) Sehemu gani korofi katika njia hiyo ki miundombinu na kiusalama.

(3) Mipakani regulations kama unatoka na mzigo wa biashara toka pretoria kwenda Dar inakuwaje?

(4) Vitu gani vya muhimu ambavyo ni lazima niwe navyo standby.

(5) Na safari inakadiria kuchukua siku ngapi (max).

(6) Mwisho kabisa ni changamoto gani nitarajie kukutana nayo kwenye njia hiyo.

(7) Lakini pia ni mazuri gani nitarajie kukutana nayo kwenye safari hiyo.
 
Mkuu zingatia tairi za hiyo gari usitumie ilizokuja na gari pitia Lusaka hapo Nakonde kuna road toll,bima,council hizo. kukata nadhani hazizidi 100 usd unapita Living Stone kazungura kuelekea Botswana kuingia Botswana unalipia usd 50 kwa kuingia na utakaporudi hautalipia tena utaruhusiwa kupita hizo karatasi kupata ni saa moja tuu pita boarder iliyo karibu na Gaborone kuingia haina magari mengi hata utakapotoka. South Africa kuingia haulipii kitu kupata document pale umbali kutoka Tunduma mpaka pretoria ni 2700 km..
 
Kama huna uzoefu wa kuendesha safari kubwa achana na huo mpango, unaweza kutamani kulitupa gari lako. Nenda na mtu mwenye experience.
Usalama hapo border ni soo, unaweza kuibiwa hadi passport yako. Hasa wakigundua umebeba bidhaa adimu hivyo.
Ushauri wangu, kama unaenda kwa ajili ya shopping, panda ndege kanunue vitu uvitume kwa usafiri wa ndege hiyohiyo.
Kama unataka kutembea tu, nenda na mtu kwenye uzoefu wa njia hizo na anayeweza kuendesha umbali mrefu.
 
Vipi akitumia njia ya Harare sio karibu zaidi?
 
Naufuatilia huu uzi kwa makini maana namwomba Mungu anijalie nikanunue gari huko then nidrive to bongo ninionee mazingira na iwe adventure
 
Gari ya cc 2.5 appx utatembea 8-9 km kwa kutumia lita 1 ya Petroli, sasa piga hesabu kutoka Dar mpaka Pretoria ni kilomita ngapi kwa njia utakazo pita? Hapo utapata atleast an idea ya kujua utatumia Petrol lita ngapi kwenda na kurudi.
 
Njia ya harare usumbufu police rushwa ya usd 20 kila akisimamishwa ataiweza na kutoka beitbridge kuingia Zim wakati wa kurudi wanataka deposit kwa kila ulichobeba hata kama ni Transit...tunapenda kupita Botswana hakuna usumbufu kama vizuri...
Mkumbushe aangalie na uchakavu wa gari maana south africa wanaangalia sana utoaji wamoshi wasije mzuia pale mpakani plzz
 
Mkuu Isanga family shukrani kuna kitu hapa nataka kujua ntakuwassup...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…