Dar: Kinondoni kutengeneza Mtaa maalum wa Baa tu

Najaribu kuipata hii picha; Walevi St. Kwa fadhila za Mh. Makonda. Dah! Ukionekana mtaa huo, basi hatuna haja ya kipimo. Usiendeshe gari.
Baa huenda ni vikolombwezo vyake, Mtura, vimini, kond..om na simama wima uchochoroni. Dah! Naona ni mtaa wa Sodoma huo. Makonda umewapata
 
Mambo ya red lighst districts
dunia nzima haya mambo yapo...

unapaswa kuwa na eneo maalum ambako watu wanaweza kukesha na kupiga kelele usiku kucha
mchana kutwa....

sheria tulizo nazo zinasema pombe kuuzwa ni kuanzia saa kumi
na mwisho saa tano usiku....

sio kila kitu kupinga sababu ni Makonda kasema
hii idea ni nzuri

Ni wazo zuri sana.

Ila hapa najiuliza...hivi hatuna kabisa planning & zoning commission au vyombo vyenye hiyo dhima?

Kwa sababu, kwa jinsi mambo yalivyo holela holela ni kama vile hatuna kabisa.
 
Napendekeza mtaa huo uitwe Delilah Dean, itasaidia sana sio kama sasa ambapo bar ni nyingi kuliko maktaba mitaani.
 
...

....ha ha hapa katikati ya JIJI maarufu duniani.. juu viota chini ulanzi 24hrs hakuna kwereee mbongo tuuu

handandshears.jpg
 
inasaidia malezi mazuri kwa watoto badala ya kuruhusu kila mta uwe na madanguro na ma bar
'massage parlous ' na kadhalika

Pamoja na kusaidia malezi, pia inaondoa kero.

Kuna baa zipo katikati kabisa ya maeneo ya makazi ya watu ambazo huwa ni kero sana.

Kuanzia kelele za walevi hadi za muziki. Zinaeneza uchafu, hususan sehemu ya jiko.

Husababisha msongamano wa magari na huleta hatari kwa wakazi kwani wakati mwingine watu wakishalewa wanaingia kwenye magari yao na kuendesha huku wakiwa kwenye hiyo hali.

Fikiria kuna watoto wanacheza mtaani halafu lije li drunk driver.....
 
nadhani sikubaliani nalo...hiyo tabia ya kutukushanya walevi wote sehemu moja halafu muanze kuvizia wake zetu hatuitaki...
Kkkkkkkkk Ahsante sana Ndugu kwa kunichekesha nikiwa pekee yangu, watu wamenishanga na tena niko ughaibuni, I had to share the story as I was in a train. Ahsante sana Ndugu that was funny
 
“Kinondoni nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar tu ili watu wakitaka kwenda kunywa pombe waende mtaa huo bila kubugudhi. Nasubiri muda tu ufike kwa sababu haiwezekani kila eneo liwe na bar mpaka nyuma ya misikiti na nyuma ya makanisa,” ameeleza Makonda. Unakubaliana nayo hii au unaipinga??
Hivi,Hiyo ni kazi ya baraza la madiwani au mkuu wa wilaya?
Huyu anaumwa
 
Kuna watu wataona kama makonda amekuwa kichaa, Lakini ukweli kuwa watakuwa hawajaishi nje ya tz,
Haya anayoyasema makonda Ndio utaratibu wa dunia nzima, Kila kitu Kila huduma zinasehemu zake maalum sio Kila sehem unaweza kufanya chochote bila kujali eneo
BigBig
utaratibu ni mzuri
haukulazimishi kwenda huko kama hutaki
bar zitakuwepo sehemu zingine
isipokuwa hapo zinakuwa masaa 24
nchi zingine hapo sio bar tu hadi madanguro yanakuwa na eneo maalum...
so unakuta mtaa mmoja mreefu una bar ,casino,madanguro na kadhalika

inasaidia malezi mazuri kwa watoto badala ya kuruhusu kila mta uwe na madanguro na ma bar
'massage parlous ' na kadhalika
Big up comrade Makonda.
Duniani kote kwenye ustaarabu kuna mpango kama huo....kila kitu mahala
 
Hii idea nimeipenda.


Walevi wakusanywe sehemu moja..... Mkilewa mtukanane na kutwangana wenyewe kwa wenyewe.
 
Kule Beijing katika wilaya ya Chaoyang maeneo ya Sanlitun kuna Bar street( Jiubajie) usiku kule ndio kunakuwa mchana. Watu wanakula maisha kwa raha zao bila kubughudhi wengine.
 
Watengeneze na mtaa maluum wa hospitali tu, pia mtaa maalum wa gesti na madanguro tu halafu na huo mtaa wao wa bar tu!
Ili Wazinzi, Wagonjwa na walevi wakutane pamoja!
 
Mi naona ni poa sana kifanya hivo tena iwe Sinza maana ule mtaa mmmmmh
 
HII NDOTO YA MCHANA, ZA HIVI ZINAOTWAGA PALE LUMUMBA! NA KINA JINGALAO,FAIZA,LIZABONI,TATAMADIBA. NA WENGINEO!
 
Mambo ya red lighst districts
dunia nzima haya mambo yapo...

unapaswa kuwa na eneo maalum ambako watu wanaweza kukesha na kupiga kelele usiku kucha
mchana kutwa....

sheria tulizo nazo zinasema pombe kuuzwa ni kuanzia saa kumi
na mwisho saa tano usiku....

sio kila kitu kupinga sababu ni Makonda kasema
hii idea ni nzuri
Idea ni nzuri tena sana tu lakini wrong approach. Hivi vitu vinatakiwa viwe kwenye master plan ya City na vifuatwe. Sasa tukianza kuwaachia wakuu wa wilaya kila mmoja aje na plan yake itakuwa kizungumkuti. Anyways mimi nadhani njia rahisi kabisa la kutatua tatizo la Dar lingekuwa kuanza kujenga jiji jingine maeneo kama Bagamoyo huko. Kuna mahali tulikosea tukajenga holela sana na kila kitu kikawa zig zag kiasi ambacho kurekebisha itagharimu sana! Kuna siku nilikuwa napita maeneo ya Kinondoni A yale yaliyokuwa na National housing. Ni masikitiko na majuto! Zamani katikati ya kila nyumba kulikuwa na sehemu ya miti na bustani. Nyumba zilipangiliwa vizuri. Siku hizi watu wamejenga mpaka sehemu ya kuweka dirisha hamna. Na ni mchanganyiko wa nyumba eg mabanda ya kuku, nyumba za kupanga, bar na guest house, gereji, vijiwe vya madawa, yard za magari uffff. Sasa haya mambo kama wana dhamira ya kweli ni kufanya kwa pamoja na sio one man show...
 
Back
Top Bottom