Dar: Atoboa bomba la mafuta ya Dizeli la bandari(SPM) na kujiunganishia nyumbani kwake

Jamaa Katiwa Mbaroni Kwa Kutoboa bomba la mafuta ya Dizeli mali ya TPA na kujiunganishia bomba lake la mafuta hadi nyumbani





Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi nchini, wanamshikilia Ndugu Samwel Nzagi Kilang'ani mwenye umri wa miaka (63), kwa tuhuma za kutoboa bomba la mafuta ya Dizeli la "Single Point Mooring" mali ya TPA na kujiunganishia bomba lake la mafuta hadi nyumbani kwake ambako ameweka mantaki makubwa ambayo ameyachimbia chini ya ardhi.

Msemaji wa TPA, Janeth Ruzangi amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo huku polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ikiendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.


 
Huyu jamaa ni genius

Nampa maksi 100


Kumbe TZ kuna vichwa namna hii

Zaidi ya Scolfield ,zaidi ya El chapo
 
Duh, kweli jasiri haachi asili. Inaonekana huyu mzee hizo ndio shughuli zake tangu ujana wake.

Vv
 
ukiangalia kwa jicho la pili huyo mzee hayupo peke yake hapo.......kwa sababu zifuatazo
  • Kwanza hiyo shughuli ya kuunganisha ilo bomba toka kwenye bomba kubwa linahitaji utaalamu na pia sio shughuli ya siku moja. Lazima alishirikiana na watu wa inside/au watu wenye taaluma ya fluid flow
  • Pili huyo mzee lazima atakuwa alikuwa na wateja
  • Tatu kama bomba lina likage ni rahisi kugundua...maana kiasi kitolewacho kwenye source kinakuwa tofauti na kule kinapopelekwa....sasa siku zote walikuwa hawajagundua.....security na uongozi inabidi wahojiwe
  • All in all hiyo siyo ishu ya huyo mzee pekee.....sio rahisi kufanya dili kama hilo peke yako
 
Hisia zangu;

mzee katoa tu eneo lake kwa ajili ya kufanikisha dili kwa malipo ya cha juu.

wahusika ni wengine.
 
Ndio napata mashaka na habari hii maana mafuta yaliyo kwenye Bomba ni ghafi anapata wapi dawa ya kuyasafisha ... Pia kutoka kwenye Bomba la mafuta kuna Presha kubwa mno kwa hicho kitengi ni uwongo kabisaaa tena wa mchana kweupe pia huwa yanaharufu mbaya sana kwa kijumba hicho Doh. Na kama ni kweli basi huyo jamaa wamwajiri TPA ili awezekutoa elimu ya kuyapooza na kuyasafisha
Acha Kujitoa Akili Nani Kakwambia Yale Mafuta Ni Crude Oil , , Meli Ikifika Bandalini Wanaconect Had Sehem Hucka
 
Jamaa Ana stahili pongezi Sema ndy hvyo keshadakwa,sheria itambana

Ova
 
Et watu wanafurahia na kumpongeza... wengine wanamuona bingwa shujaa
Hivi siku ingetokea ajali ya moto huko kwake na hiyo diesel hali ingekuaje??
Madhara yake yangelikua vipi kama asingeangamiza mtaa wote mpaka kwenye mabomba husika halafu lawama zote zingerudi kwa serikali
Kwa kweli Tanzania inaogopesha. Tumekuwa jamii ya "wagonjwa wa akili" na watu wasiokuwa na maadali. Siamini kuwa mtu kama huyu anashangiliwa na wachangiaji walio wengi kiasi hiki. Tuna kazi kubwa ya kurekebisha maadili yetu. Jamii inayoshangilia wizi na kuwaona wezi mashujaa haiwezi kuendelea.
 
km ni kweli bcTZ tunawataalamu wa kiwango cha lami.nashauri hy mzee asifunguliwe mashtaka ili atoe elimu kwa wengine na atunukiwe PHD.uthubutu wake ni mzuri
 
Ndio napata mashaka na habari hii maana mafuta yaliyo kwenye Bomba ni ghafi anapata wapi dawa ya kuyasafisha ... Pia kutoka kwenye Bomba la mafuta kuna Presha kubwa mno kwa hicho kitengi ni uwongo kabisaaa tena wa mchana kweupe pia huwa yanaharufu mbaya sana kwa kijumba hicho Doh. Na kama ni kweli basi huyo jamaa wamwajiri TPA ili awezekutoa elimu ya kuyapooza na kuyasafisha
 
-Wakati anajiunganishia walinzi walikua wapi?

-Kwa namna yoyote zoezi zima si la siku moja, watendaji Wa mtaa walikua wapi?

-Kuna kila dalili za jamaa alikua anakula na wakubwa Fulani..malengo yalikua ni nini?

-Soko lake haswa ni lipi?

-Kwanini TPA ivamie January hii? mzee alizingua kutoa mgao m?

-Kama Huyo mmoja wamembaini baada ya muda mrefu (obvious) Wa kuiba wese..kuna wangapi Wa sampuli yake?

-Kwanini mkuu Wa ulinzi asiwajibishwe? why disciplinary action shouldn't be taken against him/her ?

-Wwnafanya patrol kwa kiasi gani kuhakikisha rasilimali hazihujumiwi?

Mkuu Wa idara ya ulinzi /Head of security unit hapa lazima awajibishwe! kuna dalili za kuhusika...huyu mzee alipata wapi guts za kufanya hayo??

Bomba tu LA dawasco ukitoboa mtaa mzima wanajua Fulani anaunganisha maji..sembuse mafuta? waache Sanaa makimba yao..

Mzee nae alichemka..angesoma alama mapema..angeingia Ccm agombee hata udiwani...angekingiwa kifua kama Salum Londa na ufisadi Wa viwanja Tanganyika Packers (Feza)!
Wewe ndo umecomment kama great thinker ambayo ndo motive ya JF. Only you.

Wengine tujifunze kucomment jamani siyo kulipuka na vicoment vya ajabuajabu au tuseme kubwabwaja na kujaza thread kwa utumboutumbo
 
Back
Top Bottom