Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,725
- 6,729
Kuna vitu vitatu tunaweza kuwa tunavichanganya ambavyo ni Dar Rapid Transit Agency (DART) yaani Wakala wa Usafiri wa Haraka, Bus Rapid Transit System (BRT) ambayo ni miundo mbinu yenyewe iliyojengwa na DART na kitu cha tatu ni UDA Rapid Transit (UDART).
Tunachopaswa kuelewa ni kwamba DART wamejenga miundo mbinu yaani BRT na ndiyo wasimamizi au waendeshaji wake. Hawa UDART (muungano wa kampuni ya UDA na wamiliki wengine wa mabasi) ndiyo waliopewa kazi na DART ili kuweza kutoa huduma kwenye miundo mbinu yake yaani BRT system.
Sasa hii ya kusema kuwa Sabri Mabrouk ni msemaji wa DART (yaani wakala) wakati siyo mtumishi wake siyo sahihi na inakuwa inapotosha kwa wasiolewa kwani yeye ni msemaji wa kampuni ya watoa huduma yaani UDART.