Uchaguzi 2020 Dakika 45 na Bernard Membe ITV: Baadhi ya mambo aliyoongea

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
94,245
122,340
Hahaha! Membe bana. Hivi atafika hadi mwisho wa uchaguzi kweli?

Sasa hivi yupo ITV.



===

Ikiwa kampeni zinaendelea kupamba moto, vituo mbalimbali vya utangazaji vimeanza kuwahoji baadhi ya Wagombea wa nafasi ya Urais wa Vyama mbalimbali.

Wiki iliyopita mnamo September 3, ITV ilimhoji Ndugu Tundu Lissu mgombea wa chama cha Chadema. Wiki hii kituo cha ITV kimemkaribisha Ndugu Benard Membe ambaye ni mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo. Akihojiwa na Mwandishi wa habari Bi. Farhia Middle katika kipindi kinachoitwa Dakika 45 alieleza mambo yafuatayo:

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe amesema wakati anaondoka CCM na kukaa kama raia wa kawaida mpaka alipojiunga na chama hicho anajisikia kuwa na raha sana kulinganisha na kule alikokuwa.

Amesema ndani ya ACT-Wazalendo kuna vijana wenye akili hajapata kuona na wanajadili, kukosoa na kukosoana chini ya uongozi wa Maalim Seif na baadae wanatoka wakiwa kama timu.

Membe anasema akijilinganisha na wagombea wengine anajiona kuwa ni mtu anayefaa zaidi kutokana na uzoefu mkubwa alionao katika uongozi wa ndani ya nchi na nje ya nchi na ingekuwa dhambi kubwa sana kama asingegombea nafasi ya Urais.

Aidha, ameongeza kuwa fedha za kununua ndege na kujenga reli hazijatoka kwa Watanzania bali kwenye mabenki ya nje na uwekezaji huu hauleti faida ya haraka kwa ajili ya kulipa hayo madeni. Hakuna Serikali duniani inayomiliki ndege bali ni biashara za watu na Serikali huweza tu kuchukua hisa.

Kuhusu Ilani yao
Tutaawachia wafanyabiashara wote waliobambikiziwa kesi, ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani. Uchumi hauwezi kujengwa na serikali uchumi unajengwa na watu.

Katika dk ya 47:00 ya hiyo video Membe amefanya Monologue namna hii.

Membe: Tarehe 28 wakatupigie kura sisi akina Membe, Mmoja akasema mtatangazwa, Jibu, Tutatangazwa. Hamtaibiwa, Jibu, Sikiliza mimi mwenyewe nilikuwa kwenye hizo shughuli kwa hiyo hakuna wizi mwaka huu.

Membe amedai kuwa hakutakuwa na international observers kutakuwa na observers wa ndani tu.
 
Too late, Membe amepitwa na wakati. Katika siasa mambo yanakwenda kasi mno huu ni wakati wa Tundu Antipas Lissu.

Lakini ngoja tumsikie mzee Membe alikuwa na maana gani kuanza siasa kimya kimya kiasi anazinduka anajikuta amepitwa kwa mbali hata na mgombea wa CCM Mpya John Pombe Magufuli. Tazama wanaoongoza ktk mbio za Urais kuelekea Ikulu kufuatana na mapenzi na matamanio ya waTanzania.
  1. Tundu Antipas Lissu
  2. Maalim Seif
  3. John Pombe Magufuli
  4. ...
 
Salaam Wakuu,

Ikiwa kampeni zinaendelea kupamba moto, vituo mbalimbali vya utangazaji vimeanza kuwahoji Wagombea urais wa Vyama mbalimbali. Wiki iliyopita mnamo September 3, ITV ilimhoji Ndugu Tundu Lissu mgombea wa chama cha Chadema. Wiki hii kituo cha ITV kimemkaribisha Ndugu Benard Membe ambaye ni mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo. Shuhudia hapa chini:

 
Back
Top Bottom