Dada zetu wakinunuliwa Zawadi na waume zao wanasema Mahaba lakini sisi tukifanya hivyo Kwa wake zetu wanasema tumerogwa!!

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
5,827
11,836
Hivi ndivyo ilivyo wakuu......
Shemeji zetu wanapo onyesha upendo hadharani Kwa dada zetu kuwanunulia zawadi kadhaa wa kadhaa . Dada zetu hufarahii sana na kusema haya mahaba (Upendo/Anapendwa)

Ni mara kadhaa tunaona mashemeji wakijenga ukweni. Familia nzima itamsifia sana huyo shemeji(mkwilima)!!


Ajabu ni kwamba wewe ukifanya Yale Yale anayofanya shemeji Yako kwenu na wewe ukayafanya ukweni kwako (Kwao na mkeo)

Basi Dada zako watatoka hadharani na kumwambia wifi Yao kuwa umeturogea kaka yetu sio Bure na kama haitoshi watakuambia hata wewe au utakalishwa kikao Cha familia waone uwezekano wa kukuokoa kuhusu na kurogwa na mkeo.

Watasema haiwezekeni kabisa kaka hata kwetu hajawahi Jenga lakini ukweni kajenga hii sio Bure Kuna kitu mke wake anamfanyia.

Tena usiombe Dada zako wakae vizuri na mama Yako wamjaze maneno na mama aamini nakwambia hata kwenu utapachukia.

Hawatakaa wakumbuke Tena kuwa hata kwenu mkwilima kajenga pia na hata ukisema mfano huo Bado utaonekana una halalisha upuuzi!!!


Wanawake wanawake wanawake shida Huwa Nini wajameni?
 
Sasa utajenga ukweni wakati hata kwenu bado kuna nyumba ya nyasi?
 
Hawa Viumbe hawaeleweki....na ni Viumbe Hatari sana Hapa Duniani,
Niliwai Jenga nyumba kumjengea mwanamke Ili awe anachukua Kodi sasa Cha kushangaza aliniambia kua Sina akili, kwa kua Nimejenga nyumba sio yake Bali ni yangu.wakti Kodi anachukua yeye Mimi Wala siusiki na kuchukua Kodi... Ila umiriki wa jengo ni wangu.
 
Sasa utajenga ukweni wakati hata kwenu bado kuna nyumba ya nyasi?
Ukiwa na akili timamu huwezi Jenga ukweni kama kwenu Kuna mazingira mabaya zaidi.

Mara nyingi Huwa tunajenga ukweni Kwa kuwahurumia Watoto wetu pindi wanapoenda kuwatembelea Babu/ bibi zao wanalala kama mifugo na hili huwezi wazuia wasiende.

Ukipima mazingira unaona kabisa kwenu Kuna uangalau sehem ya kulala wajukuu na wageni ipo lakini ukweni haipo kabisa. Je ukijenga Kwa mlengo huo ni kosa?
 
Akili zao wanazijua wenyewe mkuu
 
We jenga tu ukweni siku ukiachana na mtoto wao kwa vimbwanga ndio utajua
Mkuu kujenga ukweni haimanishi unajenga Kisha unapategemea. Ni kama zawadi tu ambayo unaweza mpa mtu yeyote pasipo kutegemea utarudishiwa kitu.

Mara nyingi wanaojenga ukweni ni Kwa ajiri ya mke wako hasa anapoenda na watoto wenu kusalimia na muda huo unajua kabisa ukweni sehemu ya kulala ni changamoto
 
Hata shetani atashanga huyu mkeo katumia uchawi gani mpaka ukamjengea, wakati yeye katumia ujanja tu wakuliwa tunda na Hawa.
Mkuu ukiwa na watoto na huko ukweni hawana mahali pazuri pakulala utafanyaje? Mbona shemeji Yako kwenu ajenge isiwe nongwa ila wewe kuweka na parapanda kama lote?
 
Mkuu ukiwa na watoto na huko ukweni hawana mahali pazuri pakulala utafanyaje? Mbona shemeji Yako kwenu ajenge isiwe nongwa ila wewe kuweka na parapanda kama lote?
Fainali uzeeni wewe jenga ukizeeka utakumbuka hii comments yangu. Kuna mshkaji kaoa jamaa yetu mmoja huyu mwamba anajitahidi kila kitu kwa familia yake.
Lakini ukweni wanamuona jau kichizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…