Mbugi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,488
- 257
CZ INFORMATION&MEDIA CONSULTANT LTD
S.L.P 100026
DAR ES SALAAM
TANZANIA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
14/05/2016
Taasisi ya CZI imesikitishwa na kauli ya mwanasiasa mkongwe Profesa Ibrahimu Lipumba kuhusu suala la Sukari na tunamtaka awe mkweli kuwaeleza watanbzania namna hali ya sukari ilivyo.
Lipumba ambaye alikuwa mwenyekiti wa CUF kabla ya kujitoa amesema kuwa chanzo cha Uhaba wa Sukari ni rais John Magufuli na kusahau kwamba wafanyabiashara wa sukari walipanga hujuma hizi baada ya Magufuli kuteuliwa na chama chake kugombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania walikaa na kupanga mipango ya kumkwamisha kwa kuwa hakuwa chaguo lao.
Akizungumza na waandishi wa habari wa habari Kaimu Afisa Mahusiano wa CZI Augostino Matefu amesema kwamba kauli ya Lipumba haina mashiko na tunawashauri wananchi waidharau kwa kuwa rekodi yake na historia yake inaonyesha kwamba amekuwa anatumika nna mafisadi wa nchi hii,kwa mkutano wake alitumwa na wafanyabiashara wanaoihujumu serikali na kupewa kiasi cha pesa milioni 100 ili akaongee na vyombo vya habari.
Ndugu wananchi ukweli ni kuwa chanzo cha uhaba wa sukari ni wafanyabiashara wasio waaminifu na waliokuwa wanakwepa kodi kwa miaka zaidi ya 30 na vita hii waliipanga muda mrefu na baada ya mipango yao kujulikana wakaanza mapambano kuhakikisha rais na serikali yake wanakwama..
CZI tunaamini kwamba rais wa Tanzania John Magufuli ana nia njema na watanzania wenzake na anajua namna watanzania hao walivyoumia kwa miaka mingi ,lakini wakati anajaribu kuweka mambo sawa ili wananchi wa kawaida nao watumie rasilimali za nchi yao vizuri kundi la watu waliozoea kula bila kuulizwa wanakwamisha juhudi za rais ambazo anazifanya kwa matakwa ya wananchi wake.
Ndugu wananchi CZI tunajua namna Profesa Lipumba alivyokuwa karibu na utawala uliopita pamoja na wafanyabiashara waliokuwa wanakwepa kodi pamoja na kujinasibu kuwa yeye ni mtaalam wa uchumi.
Home Shopping Centre pamoja na tuhuma zote zile za kukwepa kulipa kodi na kuaguza bidhaa zilizoisha muda wake bado Lipumba alikuwa anamahusiano nao na alikuwa moja ya watu waliokuwa wanatumika na kampuni hiyo kwa maslahi ya kampuni hiyo.
NDUGU WANAHABARI NA WATANZANIA ,Lipumba alitumika na utawala uliopita na alikuwa anafuata maagizo ya watawala waliopita na ndio waliomshawishi kujitoa na kuisaliti CUF ili ishindwe kwenye harakati za kisiasa na akafikia kutoa maneno mazito ya kashfa kwa maalim Seif Sharrifu Hamad kabla ya kuomba kurejea tena katika uongozi.
Ndugu wananchi na wanahabari kwa maslahi mapana ya nchi yetu tunapenda tu kuwaambia kwamba Profesa Lipumba aliondoka CUF kwa maagizo ya serikali iliyopita kwa ufadhili wa wafanyabiashara wa home shopping Centre ambao walimpeleka Rwanda kwa Gharama zao,akaishi Rwanda kwa Gharama zao,akarejea Tanzania kwa Gharama zao.
CZI kama taasisi huru isiyo ya kiserikali,tunawatahadharisha wanaCUF nchi nzima Tanzania bara na visiwani,wawe makini na Profesa Lipumba kwa kuwa ni kigeugeu na amekuwa anafanya kazi zake kwa kutumwa na watu ambao walikuwa wanamtuma kwa maslahi ya kutaka kuiua CUF.
Ndugu wananchi na wana habari tunawataka wafanyabiashara ZACHARIA,Gulam Dewji,Said Bhakresa na Mohamed Dewji ambao walikuwa wafanyabiashara pekee wanaoagiza sukari kutoka nje waache kabisa vita hii na kama wasipoacha tunamuomba rais na serikali yake kusitisha vibali vyao mara moja ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine.
Ndugu wananchi tunaamini kwamba uhujumu huu ulianza tu baada ya serikali ya awamu ya tano kuanza kufuatiliwa namna wanavyoagiza sukari wakaona njia pekee ya kumhujumu rais ni kuficha sukari ili bei iwe juu wananchi waanze kumchukia rais wao.
Ndugu waandishi wa habari,Moja ya njia ya kumkosanisha rais na wananchi wake ni kupandisha bei ya sukari kutoka 1800/= hadi 3500/= kwa kilo ili waanze kuona Magufuli ameingia na ugumu wa maisha na kumuona mstaafu Kikwete alikuwa na nafuu.
Wafanyabiashara wa Tanzania hususani wa Sukari na Mafuta wamekuwa wanafanya biashara zao bila kubughudhiwa na mtu na baada tu rais wa awamu ya tano kuingia akabadilisha upepo na kuanza kuwataka wafanyabiashara hao walipe kodi jambo ambalo limefanya wakasirike na kuanza vita ya kumhujumu rais kwa maslahi yao ili wamuyumbishe yeye na serikali yake.
Lipumba lazima ajue kwamba vita hii imeanza tu baada ya rais kutangaza usitishaji wa kuagiza sukari nje ili kuvipa nguvu viwanda vya ndani kuwa na soko na rais alifanya hivyo kwa nia njema kabisa ,lakini kwa kuwa waliisha zoea kutolipa kodi wakaona waanze kumhujumu rais na serikali yake kwa kupandisha na kuficha sukari hiyo kwenye maghala yao.
uzalishaji ulifikia tani 290,112 ikilinganishwa na matarajio ya tani 288802 kwa kuwa viwanda vbya ndani havikuwa na ubavu wa kuzalisha sukari ya matumizi ya viwandani hivyo sukari iliyotarajiwa kuagizwa ilikuwa ni zaidi ya tani 131198 kwa matumizi ya kawaida na tani 170000 kwa matumizi ya viwandani.Rekodi zinaonyesha kwamba takwimu hizi kama rais asingezuia uagizwaji nje ya nchi zisingesomeka hivyo lakini baada tu ya serikali kusitisha uagizwaji wa sukari hiyo ndipo vita ikaanza .
IMEANDALIWA NA KAIMU AFISA MAHUSIANO CZI
AUGOSTINO MATEFU
Nimemsikia PROF. nilichojifunza ni kuwa katika ulimwengu huu wa frustration haijalishi elimu yako na hii ni tatizo zaidi kwa wasomi wetu especially pale wanaposifiwa na wanafunzi wao kiasi cha kuamini wanakubalika na ikitokea matokeo ni tofauti na mbaya zaidi kuangushwa na mshindani ambaye hata chuo kikuu hakupita basi ni shida kwa wasomi wetu, leo tumeona maprof. tena wa uchumi/political science wanawaaminisha vijana kuwa utumwa ulikuwa na faida kwa africa ukiuliza sababu ni kwamba bila utumwa weusi/waafrica wasingekuwa Marekani. tmewasikia mara kadhaa wakidai kunyimwa misaada ni hatari kwa watanzania, kitu ambacho ni hatari kurithisha watoto imani mbovu ya kuamini misaada ndiyo msingi uliotufikisha hapa, katika ulimwengu wa leo huwezi ukaendelea ku-influence jamii kwa title tu ya mimi msomi bingwa nk kama huwezi binafsi kuionyesha jamii namna personally unavyofanikiwa (personal achievements) kwa kutumia elimu yako hiyo. wakati furahi usishangae ukakuta watoto wakiulizana katika familia " hivi baba alisomea nini?? na baadaye utasikia wakikataa kabisa kufuata nyayo za wazazi simply kwa kuwa wanaona ni hovyo kabisa na mwisho wanafanya waki - associate na wanacho experience kutoka kwa wazazi tena wanaotambulika kuwa ni wasomi katika jamii zao na hatimaye wanaamua kuacha kusoma na wanachagua mbadala.