CWT tawi la Songea kwanini hamtoi hela za wastaafu waliopunjwa kuanzia 2016 hadi 2024 wakati nauli zao mlikula?

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,855
6,054
2021 aliwaita wastaafu wote ambao walipunjwa pensheni zao na mkafanya nao kikao mkakubaliana atumwe katibu dodoma kwenda kufuatilia hayo mapunjo ambayo baadhi ya wastaafu katika penshen zao walipata pesa tofauti na wanachodai na mkakiri kweli mahesabu hayakufanyika vizuri.

Baada ya katibu kutumwa huko dodoma akarudi na jibu mkubwa wenu anadai apelekewe risiti za mishahara yote ya nyuma wastafu hawakuwa na baya wakazitafuta wakazileta na mkaomba na michango ya nauli wastafu wakawachangia kila mmoja alitoa elfu 30 walikuwa wastaafu 200 hao wa songea mjini pamoja na vijijini mkiijumuisha na wiliya ya namtumbo.

Kilichofuata katibu umeenda ukalud na majibu mkubwa kakubali kuwalipa kwahiyo mnangoja fungu tokea 2021 mpaka leo majibu ni hayo hayo muda wowote mtawalipa.

Matokeo yake baadhi wanakufa kila kukicha na wakati raisi alisha saini pesa imetolewa na wengine wa mikoa mingine na baadhi ya wilaya wamezipata nyinyi majibu yenu ni yale yale au mnataka wote wafe? kwanini msiwalipe jasho lao
 
Back
Top Bottom