Shalom
JF-Expert Member
- Jun 17, 2007
- 1,315
- 125
? alama hiyo ina maana gani?, au sasa imekuwa lama ya tuhuma?
mambo yaliyonifanya nikujue kuwa wewe na Engineer Mohamed ni wamoja!
? alama hiyo ina maana gani?, au sasa imekuwa lama ya tuhuma?
CUF yaandaa mgomo dhidi ya bidhaa za BOPAR
Na Ali Suleiman, Zanzibar
CHAMA cha CUF kimesema kitaitisha mgomo Unguja na Pemba kuwataka wananchi kususia mchele unaoagizwa na kampuni ya BOPAR Enterprises baada ya kubainika kwamba ni mbovu.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Bw. Salim Bimani, alisema jana kwamba mchele unaoagizwa na kampuni hiyo ni mbovu na haufai kwa matumizi ya binadamu, na kudai kuwa Serikali inamlinda mfanyabiashara huyo.
"Saratani kwa asilimia kubwa inatokana na watu kula vyakula vibovu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu, sasa sisi tunataka kulishughulikia tatizo hili kwa kulikomesha moja kwa moja," alisema Bw. Bimani.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) juzi ilitoa taarifa kuhusu mchele mbovu uliozusha malalamiko kwa wajumbe wengi wa Baraza hilo, ambapo ripoti yake haielezi hali halisi ya mchele huo unaolalamikiwa.
Lakini taarifa hiyo ilisema inakusudia kuwachukulia hatua kali baadhi ya watendaji wa taasisi zinazojishughulisha na vyakula kikiwamo kitengo cha kumlinda mlaji kwa kutokuwa makini katika kushughulikia tatizo hilo.
Akichangia taarifa hiyo, Mwakilishi wa CUF, Bw. Haji Faki Shaali, alisema Serikali inamlinda mfanyabiashara huyo, ambaye amekuwa akifadhili CCM.
Sijui ni ukweli gani ambao SMZ wamejalibu kuuficha!..CUF pia ilisema kuna vifo vingi vinavyosababishwa na matumizi ya dawa zisizofaa na vyakula vilivyomaliza muda wake.
Chama hicho kimelaani hatua ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kuthubutu kuficha ukweli juu ya kashfa ya kuingizwa nchini mchele mbovu.
Alisema ni jukumu la SMZ kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika ili kulinda afya za wananchi.