CRDB ni Jipu jingine linahitaji kutumbuliwa!

Hawa nao washed.nzi kweli! Ile internet banking nayo siku hizi imekuwa kimeo ya kusubiria kinoma, nilikuwa nshasahau kufanya transaction za ndan ya bank,
CRDB kama mtapitia huu uzi, rekebishen internet banking kwanza tena haraka
 
Moja ya benki zinazofanya vizuri sana nchini lakini cha ajabu wameshindwa hata kufungua branch pale nairobi,kimei kashaishiwa pumzi,

unadhani branch za Benki zinafunguliwa kama fasheni
 
Kila kitu limekuwa jipu?? sasa kama hilo kutumbua unaanzia wapi? maana halioneshi hata mdomo,siyo yote ni majipu ya ndan
Mkuu umemsikia Kasimu Majaliwa kamuagiza CAG akaichunguze CRDB kwakuwa kuna ubadhirifu mkubwa!!Jipu hilo linatumbuliwa!
 
60% ya crdb staff ni shimboni kwa hiyo usitegemee mabadiliko
CRDB mpsipo angalia mnaweza kuwa kati ya mabenki yaliyoanguka kwa kushindwa kuhudumia wateja!
Aiingii akilini kilasiku ATM zenu ndo hazina network!Watu watakimbia maana hata ukienda ndani watu ni wengi teller mmoja!
Au mnaona raha pale watu wanapokuwa katika msururu mrefu?Nasikitika kama hamtajirekebisha mtabaki wasindikizaji
 
Mtandao wao wa ATM nadhani ndio unavunja rekodi za ubovu hapa Afrika mashariki, kuna siku walizingua Mpwapwa zikawa hazina kitu, nkasafiri mpaka dodoma mjini ishu ikawa palepale,lakini nimekuja kushangaa hata jioni unakuta ATM hazina huduma na wafanyakazi wao bila aibu wanaondoka kazini sijui wakifika majumbani wanasema wametoak wapi?
 
serikali itambe kuwa na 51????.
Danida devpt agency ndio wanashare nyingi.
NSsf
na community +wananchi ndio wanashare.....serikali imdire
Sasa NSSF ni taasisi ya Nani ?kama sio mfuko wa wananchi Na iko chini ya serikali.
 
Tuhuma za wafanyakazi wa CRDB kushiriki kutafuna tozo za Bandari zipo njiani kufukuliwa
Hii habari ya January mwaka huu...

Makontena zaidi ya 11, 000 yaliyotolewa Bandari Kavu (ICD’s) bila kulipiwa tozo ya Mamlaka ya Bandari (TPA), limechukua sura mpya baada ya Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), kuwasilisha kwa Waziri ushahidi wa malipo waliyofanya kwa Bandari.Aidha, Taffa inataka kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi ili kupata ukweli wa sakata hilo.Wanachama wa Taffa walituhumiwa na TPA kwamba walipitisha makontena hayo bila kulipia tozo ya bandari, lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha na kuwarushia lawama watumishi wa bandari na benki ya CRDB.Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa (Taffa), Tony Swai alisema unahitajika umakini wa hali ya juu wakati wa kulishughulikia jambo hilo ili ukweli uweze kufahamika na wahusika kuchukuliwa hatua kali.Alisema wanachama wa chama hicho wameshawasilisha vielelezo vyao vyote kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa ajili ya kumsaidia kubaini ukweli.“Wanachama wetu walilipia tozo na nyaraka zote wanazo na wamepeleka kwa Waziri kama ushahidi, tumeomba iundwe tume maana ndiyo itabaini pumba ziko wapi na mchele uko wapi," alisema Swai. "Hatuwezi kusema kwamba wanachama wetu wote wako safi maana waswahili wanasema msafara wa mamba kenge nao wamo, lakini kwa hili ushahidi wa malipo yote tuliyofanya upo thabiti.”Alisisitiza kuwa tume hiyo ndiyo itakuwa na uwezo wa kubaini watu waliokula fedha zilizotokana kwa malipo ya tozo hiyo, na kwamba utaratibu wa sasa wa kila taasisi kufanya uchunguzi wake hautakuwa na manufaa yoyote.Alisema ni vyema na ikaundwa tume itakayoishirikisha wajumbe kutoka Taffa, Taasisi ya Usalama wa Taifa(TISS), Mamlaka ya Bandari (TPA), Benki ya CRDB na Polisi ili kuchunguza nani hasa walihusika na utolewaji wa kontena hizo bila kulipiwa tozo za bandari na kusababisha upotevu wa mamilioni ya fedha za umma.Katibu huyo alisema katika hali ya kawaida, wakala wa forodha hawezi kutoa kontena kwenye bandari kavu bila mmiliki wa bandari hiyo kuthibitisha malipo yaliyofanywa kwenye benki ya CRDB.“Mwenye ICD akishajiridhisha kwamba umelipa tozo ya TPA ndipo nayeye anakupa gharama za kuhifadhi mzigo wako kwenye bandari yake kisha unachukua mzigo wako," alisema Swai."Sasa cha kujiuliza waliruhusu vipi kontena (11,000) zitoke bila kulipiwa tozo za TPA? Nani wanahusika na walifanyaje fanyaje? "Tume huru pekee ndiyo itakuja na majibu ya mchezo wote huu.”
 
CRDB juu ya maozo yote yaliyotokea hutosikia kabisa hapa JF au kwenye magazeti wito wa kutaka aondolewe kwa sababu ni mwenzeti kutoka kuleee North na Sadaka yake ni muhimu sana kwa Congregation yetu na hata dua za kuiombea Bank basi hufanywa palee....
 
CRDB juu ya maozo yote yaliyotokea hutosikia kabisa hapa JF au kwenye magazeti wito wa kutaka aondolewe kwa sababu ni mwenzeti kutoka kuleee North na Sadaka yake ni muhimu sana kwa Congregation yetu na hata dua za kuiombea Bank basi hufanywa palee....
Umeanza uchokozi, Teh Teh
 
Duh! Kumbe, kwa muda mrefu nimekuwa nikijua ni privately owned commercial bank. Kuna muda nilijipa ka homework kujua background ya crdb sababu nilipeleka barua ya maombi ya kazi, maeneo mengi ilielezewa kama benki binafsi.
Mfano hii site, zipo na zingine:

CHEKI HII LINK.

Kimei labda alifuata greener pasture!
CRDB ni benki binafsi ila kunapokua na interest ya Serikali mfano ukusanyaji wa mapato serikali ana haki kikatiba kuingilia kati kujua ukweli kupitia ukaguzi wa idara ya Serikali itakayoteuliwa
 
Hao jamaa kama hauangalii salio mara kwa mara wanapiga panga account yako kidogokidogo.
 
CRDB mpsipo angalia mnaweza kuwa kati ya mabenki yaliyoanguka kwa kushindwa kuhudumia wateja!
Haiingii akilini kila siku ATM zenu ndo hazina network!

Watu watakimbia maana hata ukienda ndani watu ni wengi teller mmoja!

Au mnaona raha pale watu wanapokuwa katika msururu mrefu?

Nasikitika kama hamtajirekebisha mtabaki wasindikizaji
Kichekesho ingawa sio kizuri ile ATM ya Tangi Bovu ukitoa laki 4 unatakiwa uwe hodari wa kun'gan'gania fedha maana uwa ina bana fedha na ukizembea m inazirudisha!
 
Back
Top Bottom