CIA ya wamarekani yatoa takwimu ya wakristo/waislam TZ ktk website ya

Hizo data CIA wamezipata wapi? au wamebuni!!? Mbona mimi sijawahi ona CIA wakija kuniuliza dini yangu?
 
Lini walikuja kufanya sensa ,ndio maana hata Trump aliwadharau kwa kusema hawa ndio waliosema Saddam ana silaha za maangamizi
 
Hao CIA si ndo walisema Saddam ana silaha za maangamizi Wakati siyo kweli!. Hao ni wa kupuuza tu, ni lini wamefanya sensa nchini?

Tungeweza kujua ukweli kama serikali ingekubali takwa la masheikh la kuweka kipengele cha dini za watu ktk sensa!

Hizi speculation za aina hii ndiyo maana Masheikh wakataka kukatwa mzizi wa fitina, kiwekwe kipengele cha dini za watu, ukweli ujulikane!
shida iko wapi kaka kama za kwao sio zakweli toa za kwako zilizo za kweli..........
 
Data zinaweza kuwa kweli kwani si research zinafanyika kila Siku ?..

Au kuna tatizo gani wewe kushangaa....

Halafu nani kakwambia kuwa serikali haina data za dini za watu wake wakati sensa iliyofanyika 2012 kila kitu kipo wazi?......
.
 
Taarifa hii inawiana na data za tohara kwa wanaume Tanzania. Imani moja tohara lazima kwa waumini wao lakini Imani nyingine tohara si lazima. Na ramani ya kuonesha tohara (waliofanyiwa kwa mila au kidini au wasiofanyiwa kimila)inaonesha wapi kuna iidadi kubwa ya watu Tanzania. Pamoja na Donald Trump kutilia mashaka baadhi ya Taarifa za kiintelejensia lakini Taarifa hii kuhusu Tanzania inakubalika kisayansi kutumika kama takwimu ya uwingi na pia Watu was sekta ya afya wataikubali.
 
Kipengere hiki cha dini katika Takwimu hakitusaidii Watz. Ni mbinu tu ya wasiotutakia mema kuendelea kutugawa ili tujione kuwa sisi sio ndugu na sisi sio wamoja. Ndio maana hata kwenye sensa ya taifa kiliondolewa. Binadamu wote ni ndugu zangu bila kujali rangi, dini, kabila, jinsia, uwezo wa kifedha, wala kanda wanayotoka, na Afrika ni moja.
 
Taarifa hii inawiana na data za tohara kwa wanaume Tanzania. Imani moja tohara lazima kwa waumini wao lakini Imani nyingine tohara si lazima. Na ramani ya tohara inaonesha wapi kuna iidadi kubwa ya watu Tanzania
Wamasai, wabarbaig, wambugwe.
 
Taarifa hii inawiana na data za tohara kwa wanaume Tanzania. Imani moja tohara lazima kwa waumini wao lakini Imani nyingine tohara si lazima. Na ramani ya tohara inaonesha wapi kuna iidadi kubwa ya watu Tanzania. Pamoja na Donald Trump kutilia mashaka baadhi ya Taarifa za kiintelejensia lakini Taarifa hii kuhusu Tanzania inakubalika kisayansi kutumika kama takwimu ya uwingi na pia Watu was sekta ya afya wataikubali.
Tembeeni Basi Kidogo Na Mikoa Mingine Mjifunze, Tanzania Ni NChi Kubwa, Nyie Ndo Mnaohubiriana Misikitini Hii Nchi Waislamu Ni Wengi Wakati Tangu Mmezaliwa Pwani Mnafikiri Watu Wote Wanaishi Kama Ninyi. Anyway Mimi Kwetu Mara - Mila Na Desturi Zetu Ni Kutahiriwa Na Kisu Mbele Ya Kundi La Watu Bila Ganzi Na Bila Kutikisika, Asiyetahiriwa Tunamwita Mrishya. ( Makabila Mengine Yenye Tamaduni Hii Ni "Wakurya, Wangoreme, Wazanaki, Wakabwa, Wanandi" Sasa Ninyi Mmekuwa Completely Assimililated Na Waarabu Na Ndio Wamewafunza
 
Aisee wamarekani C watu wa mchezo mchezo, nimeingia katika WEB library ya Central intelligence Agency Nimekuta data ambazo hata Serikali ya TZ hawana, nimeona data mbalimbali kila aina, kilichonistua ni hizi takwimu za wakristo na waislamu tanzania hizi hapa chini

Christian 61.4%, Muslim 35.2%, folk religion 1.8%, other 0.2%, unaffiliated 1.4%
note: Zanzibar is almost entirely Muslim (2010 est.)

Kwa data zaidi ingia link hii hapa
The World Factbook — Central Intelligence Agency

Je hizi data za wamarekani ni za kweli????
Hii habari ya dini gani ni wengi itasababisha battle mbaya sana
 
Aisee wamarekani C watu wa mchezo mchezo, nimeingia katika WEB library ya Central intelligence Agency Nimekuta data ambazo hata Serikali ya TZ hawana, nimeona data mbalimbali kila aina, kilichonistua ni hizi takwimu za wakristo na waislamu tanzania hizi hapa chini

Christian 61.4%, Muslim 35.2%, folk religion 1.8%, other 0.2%, unaffiliated 1.4%
note: Zanzibar is almost entirely Muslim (2010 est.)

Kwa data zaidi ingia link hii hapa
The World Factbook — Central Intelligence Agency

Je hizi data za wamarekani ni za kweli????
 
Kwamba wao ndio wengi; sisi ndio wachache au kinyume chake inasaidia nini? Is there any advantage or disadvantage based on your number? Vyovyote iwavyo ila fact moja ni dhahiri kuhusu idadi ya dini hizo mbili nchini.

Dini moja it's population size is slightly increasing kutokana na "kuvuna" wasiokuwa wa dini hiyo hususan kutoka kundi la wasiokuwa na dini, kuzaliana (now at a decreasing rate), na kutoka dini nyingine.

Dini ya pili inaongezeka although at a decreasing rate compared to the past. Miaka ya nyuma wanaume walioa wake wengi lakini kadiri miaka inavyokwenda hii trend ya kuoa wake wengi inapungua - elimu, hali ya maisha, ardhi, n.k. Source kubwa ya waumini wa dini hii ni "kuzaliana" kuliko njia nyinginezo hivyo itaathirika zaidi. Hizo ndio facts.
 
... Ni mbinu tu ya wasiotutakia mema kuendelea kutugawa ili tujione kuwa sisi sio ndugu na sisi sio wamoja. ...
Hizi statistics za CIA sio kwa Tanzania peke yake ndugu. Kwenye website yao wameweka za nchi zote duniani; labda useme wanataka kuigawa dunia yote na sio Tanzania peke yake. Na pia wameenda mbali zaidi, sio dini peke yake hadi "men and women fit for military service (war)" zimewekwa sembuse dini!
 
Back
Top Bottom