Chuo Kikuu cha Morogoro kinadidimia kitaaluma

Muslim University of Morogoro (MUM) nikama kimewashinda ndugu zetu waislamu kukiendesha, inasikitisha sana. Hivi mkiacha kikafa na kufungwa kabisa mtamlalamikia nani?.

Dalili za kushindwa kukiendesha chuo hicho.

1. Idadi ya wanafunzi imekuwa ikipungua kwa kasi siku hadi siku

2. Waalimu (lecturers na tutors) wengi wamekuwa wakiacha kazi ya kufundisha chuoni hapo.

3. Chuo kinashindwa kuwalipa Lecturers na tutors kwa wakati; Ni jambo la kawaida sana kwa chuo hicho kukaa miezi MINNE (4) bila ya kuwalipa waalimu wao mishahara.

4. Chuo hiki cha kiislamu kwa sasa kinategemea sana Part time lecturers kufundisha wanafunzi wao japo pia uwezo wa kuwalipa hata hao part time lecturers nao ni mdogo sana. Part time lecturers nao wanakikimbia chuo hicho.

5. Majengo ya chuo yamechakaa sana, yaani hayana mvuto wa ki-UNIVERSITY.

NDUGU ZANGU waislamu, ingilieni kati kukinusuru chuo chenu vinginevyo chuo hicho kinaelekea kufa. Nahisi Uongozi wa chuo hicho hauna maono ya namna ya kukiendesha chuo hicho na kukifanya kuwa chuo kilicho bora kitaifa na kimataifa.
Asante mleta mada. Mimi naombea kutangaza interest kuwa ni Mkristo mkatoliki. Ktk hili suala naomba watu wasilitazame kwa jicho la udini bali kwa jicho la utaifa maana chuo kinaweza kuwa kinaendeshwa na watu wa imani fulani lakini wataalam wanaozalishwa wanalisaidia taifa. Kwahiyo kama chuo kinahitaji maboresho wahusika wachukue hatua . St.Josef university tawi la Songea tulisema palikuwa pa hovyo hapakuwa na hadhi ya kuwa hata secondary watu wakalitazama kwa jicho la udini , kilichotokea wahindi wale wakatoliki walibanwa na Kanisa pamoja na Serikali na sasa wamekifunga mpaka wafanye maboresho. Pale MUM nilikwenda mwaka 2012 nilikuta wimbi kubwa la wanafunzi wa pale wanahamia Jordan University na vyuo vingine nikauliza kulikoni? Nikaambiwa mambo ambayo mleta mada ameyasema.
 
Muslim University of Morogoro (MUM) nikama kimewashinda ndugu zetu waislamu kukiendesha, inasikitisha sana. Hivi mkiacha kikafa na kufungwa kabisa mtamlalamikia nani?.

Dalili za kushindwa kukiendesha chuo hicho.

1. Idadi ya wanafunzi imekuwa ikipungua kwa kasi siku hadi siku

2. Waalimu (lecturers na tutors) wengi wamekuwa wakiacha kazi ya kufundisha chuoni hapo.

3. Chuo kinashindwa kuwalipa Lecturers na tutors kwa wakati; Ni jambo la kawaida sana kwa chuo hicho kukaa miezi MINNE (4) bila ya kuwalipa waalimu wao mishahara.

4. Chuo hiki cha kiislamu kwa sasa kinategemea sana Part time lecturers kufundisha wanafunzi wao japo pia uwezo wa kuwalipa hata hao part time lecturers nao ni mdogo sana. Part time lecturers nao wanakikimbia chuo hicho.

5. Majengo ya chuo yamechakaa sana, yaani hayana mvuto wa ki-UNIVERSITY.

NDUGU ZANGU waislamu, ingilieni kati kukinusuru chuo chenu vinginevyo chuo hicho kinaelekea kufa. Nahisi Uongozi wa chuo hicho hauna maono ya namna ya kukiendesha chuo hicho na kukifanya kuwa chuo kilicho bora kitaifa na kimataifa.
Hiyo yote sababu hakluna viongozi bora katika hicho chuo kazi yao Waislam wa Tanzania kuilalamikia Serikali haiwasaidii kitu wakati waislama wa ulaya au uarabuni wanajiendesha wao wenyewe wana miradi yao ya kukuza Elimu na Uislam tofauti na Waislam wa Ki-Tanzania kazi yao kubw ani kupigana vita na kurogana tu. Kitafika wakati hicho chuo kitafungwa na Serikali ndio mwisho wake.
 
Ahsante ndg. COARTEM ....... kwa taarifa..
Ndg. WaIslamu tujifunze kusikia... huu ni ujumbe !! na Lisemalo lipo!! Sasa tufuatilie na kuhakiki..hata tukikuta powa... Tuongeze Maono na malengo!! upgrade!!
Ndg. Waislam tuache kudharau na kupuuza mambo madogodogo!!
Mkuu umekuwa mwerevu sana. Allah akupe fungu Jena na darja ya juu inshallah
 
Kile chuo ukitoka nje kula chips.....ukirud ndani unaulizwa umekula chips wapi?? Na ulikuwa na nan?? Km ni binti akitoka pale nje ya geti kuna mashushu wanakufatilia kuona unaenda wapi na kufanya nn.....mhhhh no freedom of living pale na kwa style hiyo inabinya mindset ya mtu kupanuka kichuo....hilo ni tatzo namba moja
 
Ahsante ndg. COARTEM ....... kwa taarifa..
Ndg. WaIslamu tujifunze kusikia... huu ni ujumbe !! na Lisemalo lipo!! Sasa tufuatilie na kuhakiki..hata tukikuta powa... Tuongeze Maono na malengo!! upgrade!!
Ndg. Waislam tuache kudharau na kupuuza mambo madogodogo!!
Dah! Umeongea kwa busara ya ajabu mpaka nimeshangaa. Kama kweli kuna matatizo yanayosemwa katika chuo hicho hata wewe jivike jukumu la kufikisha ujumbe huu kwa wahusika. Huwezi jua. Pengine mwanafunzi atakayesoma hapo kesho na kesho kutwa ndo atakuja kugundua dawa ya saratani au portal ya kuingilia kwenye malimwengu mengine yenye kanuni tofauti za Fizikia. Kama taifa elimu ni kwa faida yetu sote.
 
Hawa watu kwa kulalamika..hawajambo
Sasa chuo chao wanakikimbia wamejazana
Tumaini university.
 
mtoa mada jitahid kufanya research kabla ya kuleta uongo humu ndani .huna facts no right to speak. MUM ni chuo kilichojidhatit ktk uendeshaji wake na utoaji elimu yenye kiwango, hakuna lecture anae kimbia wa kususa mean kuhusu kupungua Kwa wanafunzi sio chanzo ni chuo hapana,kwani uchaguz wa wanafunz kujiunga na chuo ufanyika moja Kwa moja kupitia TCU hvo wao ndo wanajua ni vp kla chuo kitapata wanafunzi idadi iliyopangwa. Mfano toka mwaka 2010 SAUT ilikua ikichukua zaid ya wanafunz 9000 lkn baada ya utaratibu kubadilika mpaka mwaka Jana Saut imepewa wanafunz chin ya 4000 je hio ni kutokana na ubora wa chuo..........? Em tafakar kabla ya kutoa mada
 
Mara mwisho kuingia mle ndani ni mwaka 2007, niliona hali si nzuri ....ila hata ukiwa pale nje Edema utahisi hali si shwari ,hata stationary za pale nje zimelala ,tofauti na vyuo vingine ! !
hivii ni kwanini sisi watanzania kwenye mambo ya mhimu tunaendelea udini? watanzania tubadilike kwa kwelii
 
Kwa nini hukushauri chuo chenu kule Songea mpaka kimefungiwa kabisa na TCU na sasa wanafunzi wanafanyiwa transfer kama secondary
inawezekana mtoa ni muisilamu ambaye amesoma hapo na kujionea mazingira, so badala ya kugeuza kila kitu kuwa ligi kati ya uisilamu na ukristo fuatilieni kama ni kweli mchukue hatua
 
Haya mmemaliza? Semeni tu hadi mshibe. Kama si kodi zetu hivyo vyuo mnavyoringia vingelikuwepo?? Mnapewa mifedha kusomesha mfumo kristo wenu ili uzidi kuwa imara halaf mnaringa. Mnyimwe rusuku tu tiyari kelele
Tunahitaji MUM iendelee kuewpo kuzidi kutoa elimu kwa watoto wa kiislamu. Tunapoleta changamoto humu muwe mnazikubali na kufuatilia ili kuboresha chuo chenu. Hakuna sehemu iliyotajwakwenye mada kuwa MUM haifai, hebu jaribuni kuwa wasikivu.
 
Elimu inayotoka chuo cha morogoro ni ya juu sana..MZUMBE.UDSM. TUMAINI hawaifikii acha uongo wako wewe
HAJALINGANISHA!amesema idadai ya wanafunzi inapungua na akitaja sababu kuwa ni ishu ya kulipa mishahara lecturers,na kutoa tahadhari kuwa huenda uongozi hauna jipya kuhusu njia za kupata fedha za mishahara na kulipa kwa wakati.
 
kife au kisife ,kiwepo au kisiwepo. Uislam utabaki hata upigwe vita kiasi gani. Kafiri akikusifu ujue hauko sawa ktk dini yako. Taarifa iliyoletwa ni muendelezo wa vita dhaifu inayosimamiwa na watu waoga ambao Mungu wao ni America na Israel. Alete ushahidi wa madai yake, vinginevyo ni uongo na watu kama hawa ndo huwa nawatafuta ila basi
Yaani wewe si mtu mwema kwa Elimu ya watoto wa kiislamu. Jitahidi kubadilika.
DVC wa Muslim University of Morogoro ndiyo JIPU kuu litakalokiangusha chuo kile. Uliza ugomvi uliotokea mwezi wa March, 2016 kati ya huyo DVC na wafanyakazi wa pale chuoni. Ingilieni kati kukinusuru chuo hicho mkuu.
Hapa hatuzungumzii UDINI wa mtu, tunataka ELIMU tu.
 
Back
Top Bottom