Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam walaani kitendo cha udhalilishaji na shambulizi lililohusisha wanafunzi

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
4,121
7,390
1745168951691.jpg

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: KULAANI KITENDO CHA UDHALILISHAJI NA SHAMBULIZI LILILOHUSISHA WANAFUNZI

Dar es Salaam, 20 Aprili 2025
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinasikitika na kulaani vikali tukio la kushambuliwa, kudhalilishwa, na kudhuriwa kwa msichana mmoja (jina lake bado halijatambulika) linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia picha mjongeo, linalodaiwa kuwa wahusika ni wanafunzi.

Tayari, Chuo kinafatilia taarifa za tukio hilo kwa kiini ili kubaini uhalisia wake; na utambulisho wa wahusika. Endapo itabainika kuwa wahusika ni wanafunzi wa UDSM, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya UDSM. Aidha, Chuo kitashirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa Sheria za nchi zinazingatiwa.

UDSM inapinga aina yoyote ya ukatili, udhalilishaji au uvunjaji wa haki za kibinadamu ndani na nje ya mazingira ya Chuo. Pia, UDSM itasimama imara kulinda utu, usalama, na hadhi ya kila mwanafunzi na wanajumuiya wengine wa Chuo bila upendeleo. Kwa mantiki hiyo, Chuo kinatoa rai kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu, na miongozo ya chuo; na maadili ya Kitanzania.

Prof. William A. L. Anangisye
MAKAMU MKUU WA CHUO
 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinasikitika na kulaani vikali tukio la kushambuliwa, kudhalilishwa, na kudhuriwa kwa msichana mmoja (jina lake bado halijatambuliwa) linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia picha mjongeo, linalodaiwa kuwa wahusika ni wanafunzi.

Tayari, Chuo kinafuatilia taarifa za tukio hilo kwa kiini ili kubaini uhalisia wake; na utambulisho wa wahusika. Endapo itabainika kuwa wahusika ni wanafunzi wa UDSM, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya UDSM. Aidha, Chuo kitashirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa Sheria za nchi zinazingiatiwa.

UDSM inapinga aina yoyote ya ukatili, udhalilishaji au uvunjaji wa haki za kibinadamu ndani na nje ya mazingira ya Chuo. Pia, UDSM itasimama imara kulinda utu, usalama, na hadhi ya kila mwanafunzi na wanajumuiya wengine wa Chuo bila upendeleo. Kwa mantiki hiyo, Chuo kinatoa rai kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu, na miongozo ya chuo; na maadili ya Kitanzania.

Snapins.ai_491439638_531562189818116_5799046177907947352_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom