Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,093
- 13,934
Chuo cha Uhasibu Arusha – Institute of Accountancy Arusha (IAA) kimedaiwa kufanya udahili kwa idadi kubwa ya wananafunzi kuzidi uwezo wake, jambo linalosababisha uongozi wa chuo kuhamishia wanafunzi wa baadhi ya kozi katika hoteli ya Ngurdoto.
Baadhi ya Wanafunzi hao ambao wamepelekwa Ngurdoto kusoma na kuishi ni kutoka katika kozi za:
•Bachelor in Business Management (BBM)
•Basic Technician Certificate in Business Management (BTCBM)
•Ordinary Diploma in Business Management (ODBM) mwaka wa 1
•Bachelor of Accountancy (BA) mwaka wa 1 & 2
•Basic Technician Certificate In Accountancy (BTCA)
•Ordinary Diploma In Accountancy (ODA) mwaka wa 1 & 2
Baadhi ya Wanafunzi wamelalamikia suala la kupelekwa Hotelini kwani awali waliomba kusomea Main Campus ambapo walishakodi vyumba karibu na chuo na kununua mahitaji ya kujikimu kama vile magodoro, majiko nk.
Wamesema sasa wanalazimika kulipa kiasi cha Tsh. 400,000 kama malipo ya Hosteli (huko hotelini).
“Kama chuo kimejaa kwanini wanachukua idadi ambayo wao hawawezi kumudu na kuanza kutusumbua wakati tumeomba main campus?” amehoji mwanafunzi mmoja.
Wanafunzi wameomba kama Idadi imezidi ni bora baadhi ya Wanafunzi wahamishiwe Vyuo vingine.