Christina ni Mwanamke Shujaa, apongezwe

GTs,
Nimekuwa nikiona wana jukwaa mnavyomsema vibaya Christina kisa kuachana na mume wake Mzee Shusho.

Wengi wenu ni wanaume ambao hamjui hali aliyoipitia Christina ktk maisha yake ya kuolewa ktk umri mdogo.

Historia ya Christina inawakilisha kundi kubwa sana la wanawake ambao wazazi wao walikataa kuwasomesha na kuwalazimisha waolewe kisa tu wazazi wao waliamini kumsomesha mtoto wa kike ni kupoteza hela kwa sababu anaweza kushika mimba akiwa shule.

Christina ni shujaa kwa sababu kaamua kulisemea kundi kubwa la wanawake wenye maumivu ya kukatiliwa ndoto zao na wazazi kwa kulazimishwa kuolewa.

Tuungane kuukemea utaratibu wa kumuoza mtoto wa kike badala yake watoto wa kike wawe na haki sawa ya kusoma.

Tumpongeze Christina kwa kujitokeza kuwatia moyo wanawake wote ambao ndoto zao za maisha zilikatishwa na ndoa za lazima.

Pia tukumbuke, mbinguni hatuendi kwa sababu tunandoa au hatuna ndoa bali ni roho safi inayoamini ktk Yesu Kristo, inayoamini na kumtegemea Mungu. Tuache dhihaka zidi ya Christina, tumtie moyo ili sauti zizidi kupazwa kuzuia ndoa zinazokatiza ndoto za wasichana kisa ndoa iliyolazimishwa na wazazi.

Pia soma: Anayofanya Christina Shusho ni matokeo ya Wanaume wengi kuoa Wanawake Watumwa wasio huru. Siku wakipata Uhuru wao hayo ndio hutokeaga
Wewe ni ME au KE?
 
Inaonesha jinsi gani mwanamke Tanzania hajakombolewa, yaani mnaakili za kishenzi sana. Hivi ni wanawake wangapi waliopo kwenye ndoa za kulazimisha??? Tena nchi za kiislam wanauawa wasichana wakikataa kuolewa kwa lazima, leo hii mjinga ka wewe unatetea mwanamke agandamizwe tu kisa wmanamke.
We ndo mjinga,yaani ndoa ngumu baada ya kuwa maarufu?ndoa hiyohiyo imekufanya unazurura kila mahali,kila nchi inakuwaje leo ndo shida ionekane
Alafu unauliza mimi nikombolewe?mimi sihitaji kukombolewa kama mjinga wewe
 
Back
Top Bottom