Chonde chonde Rais Magufuli, usiguse hii Katiba tuliyonayo

Hujaonyesha uhusiano uliopo kati ya maandamano unayoyasema na kabita yao binafsi sijakuelewa!


Wanaandamana (Raila Odinga &Co.) ili kuitoa Tume ya uchaguzi kwa nguvu, yaani wanakwenda kuvamia ofisi za tume ya Uchaguzi kwa lengo la kuwafukuza Viongozi wa tume hiyo na ndiyo maana wanapigwa mabomu ya machozi na askari!
 
huku Arusha tumeanza kupewa kibali kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa ili kununua sukari kwenye maduka maalum,kila kaya kilo moja, ninachojiuliza haya yanafanyika hapa katikati ya mji wa Arusha huko vijijini si hatari, kweli naungana na yule aliyesema anaiona Zimbabwe inakuja
 
Wanaandamana (Raila Odinga &Co.) ili kuitoa Tume ya uchaguzi kwa nguvu, yaani wanakwenda kuvamia ofisi za tume ya Uchaguzi kwa lengo la kuwafukuza Viongozi wa tume hiyo na ndiyo maana wanapigwa mabomu ya machozi na askari!
Ahsante kwa maoni yako. Katiba ya warioba ndio jibu. Matatizo ya Kenya yanaongezwa na ukabila.
 
Inaitwa arbitrary thinking. Huwezi kuwa na katiba ya hovyo ukategemea utawala bora na wenye mafanikio. Hayo ni matamanio ya hovyo. Ni sawa na kusema maneno ya hovyo hovyo kisha ukatarajia watu wakuunge mkono.
 
Hii Katiba tuliyonayo ndiyo itakayotuletea maendeleo ya haraka nchini mwetu, na ndiyo najua mtanikodolea mimacho, naongelea madaraka makubwa ya Raisi kwa kifupi Raisi ambaye ni Mungu mtu, kwamba anachoongea kinafanyika bila ya kupingwa popote!

Ikumbukwe kwamba sababu hasa ya vyama vya upinzani kulilia hii wanayoita Katiba mpya wala haiko kwenye maendeleo ya nchi yetu bali iko hasa kwenye ubinafsi zaidi, wanataka kuwa na Katiba ambayo itawawezesha kuingia madarakani kwa njia yoyote ile isipokuwa ya kura!

Hii Katiba yetu kwa jinsi ilivyo hakuna jinsi wanavyoweza kutumia mbinu zao kuingia madarakani kwani Raisi anaweza kuzizima na kuwacrash mara moja,
lkn tukishaleta mambo ya Katiba kama ya Kenya au AK huwo ndiyo mwisho wa nchi yetu na hata hawa Wapinzania wenyewe kama wangekuwa wao ndiyo wako madarakani na Katiba hii wala wasingeigusa!

Hivyo chonde chonde, Hakuna kuigusa Katiba yetu, ibakie jinsi ilivyo kwani kwa nchi changa na masikini kama TanZania tunahitaji Raisi mwenye nguvu na aliye juu ya Sheria!


Anayetaka Katiba mpya ahamie Kenya, kwetu ni Nope!

kimtazamo upo sahihi, japo sio kweli kuwa raisi anauwezo wa kufanya lolote, naye anafuata sheria kama kawaida, ila alicho nacho raisi wetu ni 'power of order' akitoa agizo linatekelezeka.
kuhusu katiba mpya sidhani kama hilo lipo kwenye mipango yake, wala mm sitamdai katiba mpya koz sikuwahi msikia wakati wa kampeni akiahidi katiba mpya. nitayadai yale aliyo yaahidi tu, na naona anamwelekeo wa kuyatekeleza. mungu amtangulie
 
Tatizo watu wengi wanaangalia mguu unapotua,angalia na mita kadhaa mbele mzee.Namaanisha sasa hivi tuna Magufuli so far ni mzuri,Je baadae tukijakupata mtu wa ajabuu!!si atatutumbukiza tusipohitaji??Hebu tuache ushabiki kwenye mambo ya msingi..
 
Nimesikitishwa mno na maneno ya mwanajukwaa,wewe mleta mada unaijua hiyo Kenya unayo ihubiri hapa?
 
Naona mmesahau kumshauri...mwambieni magu aandike kitabu chake cha kuongoza nchi kama cha yule jamaa wa libya ...halafu akiite the hapakazi book
 
Mleta mada hajajua kwamba matatizo yote anayopambana nayo raisi wetu hata katiba inachangia?Kwanini kilajambo lichukuliwe kisiasa?Kwani mzee Warioba alikua upinzani?Au Warioba unadhani nae alikua na shida ya cheo?Hebu tafakari kwa kina
 
Dah tata nzi hajipendekezi kama wewe sasa umeandika hii hili akupe ukuu wa mkoa? Dah ukute na wewe mzazi wako alitoa ada akalipa shule usome? Si bora angekunywa pombe ikajulikana? Hata kichaa hawezi kuandika utumbo huu!
 
Hata Wapinzani waliitaka na ndo mana wakaingia kwenye Uchaguzi Mkuu.Wakakubali na Waliambiwa before sembuse leo Wapiga kelele.
 
Back
Top Bottom