Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,986
- 12,685
"In time of difficulties, we must not lose sight of our achievements."
– Mao Zedong (1956)
– Mao Zedong (1956)
HOW IT STARTED & HOW IT ENDED:
1958 – Soviet Union ilijitoa na kukataa kuisaidia China kutengeneza silaha zake za nyuklia.
- 1964 – China yafanya jaribio lake la kwanza la bomu la nyuklia na kufanikiwa.
1993 - Marekani ilifunga GPS iliyolenga meli ya kontena ya China Yinhe, iliyokuwa inaelekea Iran na kuiacha meli hiyo ikiwa imekwama baharini na kushindwa kusafiri kwa siku 33. Baada ya kulaumiwa kwa uwongo na Marekani kuwa ilibeba silaha za kemikali kwenda Iran.
1996 – Marekani ilizima GPS yake katika Bahari ya China Kusini, na kulazimisha China kushindwa kutrack kombora lao walilokuwa wanalifanyia majaribio.
2003 – China iliomba kujiunga na mfumo wa satelaiti wa Galileo wa EU, na ilikuwa tayari kuchangia €230 milioni lakini ilikataliwa na EU.
1996 – Marekani ilizima GPS yake katika Bahari ya China Kusini, na kulazimisha China kushindwa kutrack kombora lao walilokuwa wanalifanyia majaribio.
2003 – China iliomba kujiunga na mfumo wa satelaiti wa Galileo wa EU, na ilikuwa tayari kuchangia €230 milioni lakini ilikataliwa na EU.
- 2007 – China wazindua satellite yao BeiDou navigation satellite na kuanza kufanya kazi nchini China.
- 2020 - Mfumo wa satellite wa BeiDou wa China waanza kutoa huduma kamili za kimataifa. Mfumo ambao ni wa hali ya juu zaidi kuliko GPS.
1994 - China iliomba kujiunga na Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS), lakini ilikataliwa na Marekani ikisema kuwa China ni "untrustworthy."
- 2011 – China ikaanzisha kituo chake cha anga za juu Tiangong Space Station (TSS). Miaka si mingi ijayo mpango uliopo ni kituo cha kimataifa cha anga za juu ISS kuacha kutumiwa hivyo kitabaki cha China tu TSS.
2011 - Marekani ilipitisha Sheria iliyoitwa Wolf Amendment Law, ambayo inakataza NASA kushirikiana na China katika masuala ya utafiti wa anga za juu.
- 2020 – China yapeleka chombo cha kwanza cha anga za juu sayari ya Mars.
- 2024 – China yaweka rekodi kuwa nchi ya kwanza kubeba sampuli ya udongo kutoka upande wa mbali wa mwezi.
2019 - Serikali ya Marekani yaizuia Huawei kutumia Android OS na Google Mobile service.
- 2021 – Huawei yazindua simu ya kwanza inayotumia HarmonyOS
- 2025–Huawei wazindua HarmonyOS PC
2019 – Kwa kushinikizwa na serikali ya Marekani kampuni ya ASML ya Uholanzi ilipigwa marufuku isiiuzie China mashine za EUV za kutengeneza semiconductors za hali ya juu.
- 2025 – Mashine ya kwanza ya EUV kutengenezwa nje ya Uholanzi yazinduliwa China inatumia teknolojia ya LDP badala ya LPP ya ASML, yafanyiwa majaribio katika kituo cha Huawei cha Dongguan. Wataanza mass production ya mashine hizo 2026.
China is unstopable! Marekani sio mwanafunzi mzuri wa historia kuhusu China, huwezi kuizuia China hata siku moja kiteknolojia au kiuchumi iwe ni trade au tech war.