China inapanua uwekezaji Afrika huku Marekani ikiizuia kuongeza uwezo wake wa uzalishaji

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,094
1,094
VCG111255062575.jpg

Kutokana na kuimarishwa kwa uhusiano kati ya China na Afrika, katika miaka ya karibuni, uwekezaji wa China umeendelea kuongezeka barani Afrika. Hivi karibuni serikali ya China ilitoa taarifa inayosema kwamba uwekezaji wa China barani Afrika mwaka 2023 ulikuwa dola za kimarekani bilioni 3.96, mara 2.2 zaidi ya mwaka uliotangulia, kasi ambayo iliongoza katika uwekezaji wa moja kwa moja wa China na nje. Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani kama vile CNN na New York Times "kwa wivu" vilipotosha uwekezaji wa China barani Afrika.

Pamoja na kurudia uwongo wa "mtego wa madeni", pia walisema "China inaibembeleza Afrika ili kujipatia uungaji mkono". Hasa baada ya China kutangaza kuwa itatoa ufadhili wa Yuan bilioni 360, sawa na kiasi cha dola za kimarekani bilioni 50 kwa Afrika katika miaka mitatu ijayo, shutuma hizi zisizo na msingi zimeenea zaidi.

Ni wazi kuwa, kuusemea vibaya uwekezaji wa China barani Afrika ni mfano hai wa Marekani kukandamiza ushirikiano wa Kusini Kusini. Inajaribu kuzuia China kusaidia nchi za Afrika kuinua uwezo wao wa uzalishaji viwandani, ili kuibakiza Afrika kuwa chini kabisa kwenye mlolongo wa uzalishaji viwandani kimataifa, na hivyo kudumisha nafasi ya Marekani katika uhusiano wake na Afrika.

Kwa hakika, hakuna tofauti kati ya kile kinachofanywa na Marekani leo na kile ambacho baadhi ya nchi za Magharibi zilifanya barani Afrika wakati wa ukoloni na kuizuia Afrika kupanda nafasi ya juu kwenye mlolongo wa viwanda kimataifa. Hata hivyo, iwe ni mafuta au madini adimu, mapato ya mauzo ya nje ya bidhaa hizi za msingi ni kidogo na yanaathiriwa sana na hali ya uchumi wa dunia, hali ambayo imesababisha Afrika kuendelea kuwekwa pembeni katika mfumo wa uchumi na biashara duniani. Mbali na hayo, Marekani kwa muda mrefu imekuwa na nafasi muhimu katika kuunda vigezo na sheria za biashara za kimataifa, na kwa nchi za kusini ambazo bado zinatarajia kuinua uwezo wa uzalishaji viwandani, itachukua hatua za kuzikandamiza, haswa kwa kupitia nguvu zao kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, nchi za Afrika haziwezi daima "kushinikizwa" na Marekani na kushika mkia kwenye mlolongo wa viwanda. Kwa sasa, China imekuwa nchi inayoendelea yenye uwekezaji mkubwa zaidi barani Afrika, na Kwa kuimarisha ushirikiano wa Kusini Kusini na kuinua kwa pamoja uwezo wa teknolojia na uzalishaji viwandani, nchi za Afrika bila shaka zitaweza kuinua hadhi yao katika mfumo wa uchumi wa kimataifa na nafasi kwenye mnyororo wa viwanda duniani.

Ikiwa mshirika wa kimkakati wa nchi 53 za Afrika ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia nayo, China imechangia maendeleo ya kisasa ya Afrika kwa mipango madhubuti ya ushirikiano na mafanikio yanayoonekana. Jukumu la pamoja la China na Afrika la kuleta mambo ya kisasa si kurudia njia ya zamani ya nchi za Magharibi, bali ni kukuza maendeleo ya pamoja ya dunia ya kusini na kujenga muundo wa kisasa wa kimataifa uwe na haki zaidi, ujumuishi zaidi na ustawi wa pamoja. Kwenye mwelekeo huo usiozuilika, "kuikandamizi Afrika kiviwanda" kutashindikana kabisa!
 
Back
Top Bottom