SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,082
- 11,676
Leo kuna jambo nitalisema kwa sababu nimelitafakari muda mrefu hasa baada ya msimu uliopita kuisha.
Katika msimu wa 2022-23, msimu wa mwisho wa Che Malone Fondoh akiwa na Coton Sport ya Cameroon, timu hiyo ilishika nafasi ya mwisho katika kundi lake kwenye CAFCL, ikiongoza kwa kuruhusu magoli mengi kuliko timu katika makundi yote, ikiruhusu magoli 16 (Simba iliruhusu magoli 7 tu).
Msimu huo huo, Simba iliyokuwa na Babu Onyango tuliyekuwa tunamtuhumu kwa makosa mengi yaliyoigharimu timu, ilikuwa timu iliyoruhusu magoli machache zaidi katika ligi ya NBC (kuwa fair kwa Che Malone, hata Coton Sport iliongoza kwa kuruhusu magoli machache katika ligi ya ndani).
Tukija msimu wa 2023-24, msimu wa kwanza wa Che Malone akiwa na Simba, beki ya Simba imeonekana kuvuja sana. Katika AFL, Simba iliruhusu magoli 3 katika mechi mbili. Katika robo fainali ya CAFCL, Simba kwa mara ya kwanza kabisa ilifungwa ndani nje na Al Ahly, ikiruhusu tena magoli 3.
Katika ligi ya NBC, Simba ni moja ya timu zilizoruhusu magoli mengi msimu uliopita, ikiwa imefungwa magoli mengi kuzidi Azam na Coastal Union, na ikiwa imezidiwa magoli na Namungo kwa goli 4 tu.
Nimalizie kwa kusema Che Malone ni mchezaji mzuri sana na Simba ina bahati kuwa naye. Ana utulivu, ana nguvu, anatumia zaidi akili katika uchezaji wake na kikubwa zaidi ana nidhamu uwanjani.
Msimu huu kutokana na kuondoka kwa Inonga na ujio wa wachezaji wengi wapya, Che Malone atakuwa ni kama kiongozi wa timu uwanjani pamoja na kwamba huu ni msimu wake wa pili tu akiwa Simba na naamini ndiye mchezaji wa Simba atakayecheza mechi nyingi zaidi. Uongozi wake na usimamizi wa wenzake uwanjani na hasa kuwasimamia mabeki wenzake utaamua hatma ya Simba msimu huu wa 2024-25.