Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 795
- 501
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda (MCC) ampokea Vyerehani 125 vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha uchumi wa wanawake nchini.
Akizungumza katika Hafla ya upokeaji wa Vyerehani hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema vifaa hivyo vitaenda kuinua uchumi wa wanawake na kuwafanya wajitegemee kwa shughuli zao ikiwemo za kisiasa.
“Sote tunatambua kuwa, katika mapambano ya kuitafuta 50/50 moja ya nyenzo muhimu ya kumsaidia mwanamke kufika huko ni uchumi imara katika hili la kupewa vyerehani hivi ni chachu ya kumuongezea mwanamke kuwa na uchumi mzuri “Amesema Mwenyekiti Chatanda na kuongeza
“Uchumi wa mwanamke ukiimarika anaweza kufanya vizuri katika siasa na hata hata ya kijamii kwani inamuongezea kujiamini lakini pia anakuwa na uwezo wa kujisimamia pasipo kutegemea mahali popote na kuondokana na utumwa wa kipato”
Mwenyekiti Chatanda amesema ubalozi wa China kupitia all China women federation mmelitambua hilo na mmeamua kumuwezesha mwanamke kiuchumi kwa kugawa vyerehani na mashine za kutotolea vifaranga”
“Kipekee nachukua fursa hii Kuushukuru ubalozi wa China kwa kuikumbuka Jumuiya ya UWT kuwa kati ya wanufaika wa zawadi hizi, wanawake tuna jukumu la kuiendeleza miradi hii kwa ustadi mkubwa ili kuwa na uchumi imara na hatimaye tuweze kujisimamia na kujitegemea kijamii, kisiasa na kiuchumi.”
Aidha Chatanda amemshukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT Taifa kwa kusimamia upatikanaji wa vyerehani na mashine za kutotolea vifaranga Kwa ajili ya Wanawake wajasiriamali wa Tanzania.
📍Dar es Salaam
🗓️29/4/2024