Charles Kitwanga: Wauza madawa ya kulevya ndio walioniondoa kwenye nafasi ya uwaziri

Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi ndugu Kitwanga amelieleza gazeti la Majira leo tarehe 5 Julai kuwa wauza unga ndio walio muondoa katika nafasi yake ya uwaziri na taarifa zilizotolewa na ikulu ni uongo mtupu.

Hii sio kauli ya kawaida, ni nzito na ya kuogofya inatia Shaka pia kujua hao wauza unga wenye mamlaka makubwa namna hii ni akina nani? Kwa hiyo wamemshugulikia yeye ili biashara iendelee kushamiri hapa nchini?

Taarifa Kama hii ni fedheha kwa Mtukufu na mamlaka yake. Ingekuwa kama kule Marekani Kitwanga angeitwa na kuhojiwa na shirika la ujasusi la F.B.I ili atoe taarifa muhimu juu ya mtandao huo hatari unaoangamiza taifa wakati yeye kumbe anawajua vizuri.

Mimi naona Kitwanga anayo mengi ya moyoni toka huko Israel alikoenda kupata mafunuo ya kimungu.
Kwani walimnywesha pombe aache uongo visingizio vya uongo kama wenzake
 
katiba hairuhusu wauza madawa ya kulevya kumtimua kazi waziri...cjui anamaanisha nn labda kwa kauli yake hio sasa bwana kitwanga
 
katiba hairuhusu wauza madawa ya kulevya kumtimua kazi waziri...cjui anamaanisha nn labda kwa kauli yake hio sasa bwana kitwanga
Mkuu nankumene ulitegemea kuwa katolewa ili kulinda maslahi ya mtu?
 
Sisi wapiga kura wake tumesha inote hiyo,pamoja na kutuletea magodoro na boda boda hatubadilishi maamuzi,tupo tayari kumpiga chini
Msimpige chini bana angalau mtafaidi hayo magodoro na bodaboda wengine wawakilishi wetu hawana hizo fursa za kupiga mahela!
 
Kwani ALIYEMTUMBUA ni nani??
Kwahiyo amemaanisha au anatania??
 
Dah ngoja ni reserve comment yangu unaweza kuta Kitwanga kasema hivyo huku ashapiga Kitwanga kadhaa
 
Hayo maneno ya Kitwanga niyakuudhi.
Ila najiuliza maswali haya

Je hao wauza unga walimnywesha pombe kwa nguvu?

Lakini swali la msingi zaidi ni je,kuna watu wenye ushawishi wameishauri mamlaka yake ya uteuzi imuondoe kazini?

HAKIKA KAULI YAKE INAUKAKASI NASHAURI AITWE AHOJIWE ILI TUPATE KUWA NA UELEWA NA TAFSIRI YA PAMOJA KAMA TAIFA KWA MASLAHI YA NCHI
 
Ina maana wauza unga ndiyo waliomnunulia hiyo mipombe au ndiyo waliomshawishi Rais amwondoe?

Kwa kauli hii kama kweli kaitoa inaonyesha jinsi ambavyo hakuwa mtu sahihi wa kushika nafasi hiyo. Yaani akashindwa kuwashughulikia wauza unga wao ndiyo wakamshughulikia. Basi arudi aendelee kunywa.
 
Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi ndugu Kitwanga amelieleza gazeti la Majira leo tarehe 5 Julai kuwa wauza unga ndio walio muondoa katika nafasi yake ya uwaziri na taarifa zilizotolewa na ikulu ni uongo mtupu.

Hii sio kauli ya kawaida, ni nzito na ya kuogofya inatia Shaka pia kujua hao wauza unga wenye mamlaka makubwa namna hii ni akina nani? Kwa hiyo wamemshugulikia yeye ili biashara iendelee kushamiri hapa nchini?

Taarifa Kama hii ni fedheha kwa Mtukufu na mamlaka yake. Ingekuwa kama kule Marekani Kitwanga angeitwa na kuhojiwa na shirika la ujasusi la F.B.I ili atoe taarifa muhimu juu ya mtandao huo hatari unaoangamiza taifa wakati yeye kumbe anawajua vizuri.

Mimi naona Kitwanga anayo mengi ya moyoni toka huko Israel alikoenda kupata mafunuo ya kimungu.
Hayo ni maneno ya Kitwanga? Basi ana maana hao wauza madawa wameweka presha kwa Rais ili aondolewe? Au walimnywesha madawa akiwa nao?

Maneno kama hayo ni kutapa tapa na kuonyesha kwamba ilikuwa nafasi isiyomstahili. Ana maana siku hiyo hakulewa? Kama hali iliyorekodiwa ndo hali yake bila kulewa, basi hakustahili hata kuwa mbunge.
 
Mwigulu tunataka utukamatie wauza madawa ya kulevya na sio kuzurula na kombati zako mipakani
 
Back
Top Bottom