Changamoto zikikunyoosha ili zikufunze usikimbilie kusema umerogwa kwani utakuwa unajiroga zaidi

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Feb 4, 2024
329
874
Maisha yamekuwa na kaida ya kutupitisha kwenye changamoto mbalimbali iwe kwa kuzivutia mwenyewe au ziwe zimejivutia zenyewe ila hakuna namna waweza ishi pasi na changamoto.

Kuna changamoto zinakuja tu hata utulie vipi hakuna namna unaweza kuzuia na kuna ambazo zinakujia ila ukitulia zaidi unaona kabisa kuna moja mbili ukifanya utazuia aina hiyo ya changamoto.


Kinachonishangaza kwa sasa ni hili wimbi la ongezeko la watu kukimbilia kusema WAMEROGWA kwa kila changamoto yaani fikra za kishirikina zinakuwa karibu zaidi ya fikira nyingine , Kwanini?

Ushirikina upo ila tukianza na wewe nani kakuroga na una kipi cha kumvutia huyo mchawi mpaka aamue kakuroga wewe? Jichunguze upya isiwe umerogwa na mtindo wako wa maisha ila hutaki tu kukubali.

Ni mwajiriwa una mke yupo nyumbani tu, watoto sita na huna biashara yoyote ile sasa kipindi uko peke yako mshahara ulikutosha sasa mpo saba unataka uishi kama vile kabla hujawa na familia unaona haiwezekani maisha yanakukumbusha uwekeze wewe unakimbilia kusema UMEROGWA 😊 Nani kakuroga kama sio mfumo wako ndio umekuroga.

Ukianza tu kuona kuna watu wanakuroga usifanikiwe ndio mwanzo wa kutoka Kigoma kwenda Dar es salaam kumtafuta Mwaposa uombewe , ikishindikana hapo utaanza kuwa muumini kwa waganga wa kienyeji sasa huko utaambiwa umeibiwa Nyota yako ya mafanikio utaanza tena nenda rudi za mganga ilihali ungetulia akili tu tayari muda huo wote jumlisha gharama hizo tayari ni mtaji wa biashara wa kuongeza chanzo cha kipato.

Mchawi ni kipato chako kimoja hicho ilihali mahitaji yameongezeka sasa ongeza chanzo kingine na punguza matumizi yasiyo na lazima utakuwa umetibu kwa sehemu changamoto yako hiyo.

Mwanasayansi Saul kalivubha
Mitandaoni Fikia Ndoto Zako
 
Mentality ya kulogwa Ni mbaya sana, mtu akiwa na hayo mawazo, hata akijikwaa atasema ni uchawi, akiona paka atasema ametumwa..
 
Ni kweli kabisa
FB_IMG_1700516513047.jpg
 
Ukisha amini kila kitu ni kurogwa ujue umekwisha. Waganga wa jadi watacheza na saikolojia yako utapulurwa kila kitu.
 
Back
Top Bottom