Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 54
- 73
Habari wanajamvi,
natumaini mmeamka salama. Mimi pia, nipo kwenye computer yangu nachapisha haya maneno.
Katika pitapita zangu, nilikutana na hili swali leo asubuhi, kwenye X account ya rafiki yangu mafolebaraka
Nkatamani kulijibu kwa post kadhaa, kuanzia hili la leo.
Binafsi, sijaajiriwa hapa nchini tangu 2019, kabla ya Korona. Na nina familia ya watoto watatu, mke mmoja na watu wengine wanaonitegemea.
Miaka hiyo yote nimegundua kuwa kufanya kazi mtandaoni (online work) ni mojawapo ya sulihisho kwa upungufu wa ajira hapa nchini. Leo, ntakupa baadhi ya vitu vya kuzingatia ili kufaniniwa. Twenzetu...
Mtandao umebadilisha namna tunavyofanya kazi na kupata pesa. Kwa kujua hili, tuangalie ujuzi wenye faida na unaohitajika sana unaolingana na mabadiliko haya ya kidijitali.
Hii ni pamoja na uelewa wa jinsi ya kutumia computer, mtandao kwa ujumla na upekee wake, na software (programu mbalimbali) kikamilifu.
Utahitaji kujua namna ya kuwasilisha bidhaa na huduma unazotoa, kwa namna itakayowavutia watu wengine. Aidha, unaweza kujifunza lugha zaidi ya moja (endapo unatamani kufanya biashara/kazi nje ya mipaka ya nchi hii).
Jua namna ya kuandika meseji kwa weledi. Jinsi ya kuandika barua za kuomba kazi. Namna ya kujibu maswali. Jua jinsi ya kuwasiliana kwa mara ya kwanza na mteja mtarajiwa unayetegemea kumuuzia bidhaa baadaye (cold pitching to a prospective client). Fahamu namna ya kuuliza maswali ili kupata unachokitafuta.
Na, kuna wengi walisema "Kiingereza ni Janga la Taifa". Lakini kumbuka kuwa maisha yako yanategemea sana namna unawasiliana na watu wa kwenu (hata kiswahili huwatatiza wabongo wengi) na wasio wa kwenu.
Kumbuka: Chochote anachoweza kujifunza mwenzako Uganda na Kenya, na wewe unaweza kujifunza.
Tambua vitu unavyoweza kuvifanya kwa uzuri. Hapa nazungumzia digital soft skills (uwezo wa kidigitali). Zipo nyingi na siwezi kukuamulia. Ila kuna moja aisee naomba uanze nayo.
Prompt engineering (kutumia mfumo wa akili mnemba wa kuuliza maswali).
Kabla hujaenda mbali, nakushauri sana sana kutumia muda wako kupata ujuzi wa kutumia platform za AI, na jinsi ya kuuliza maswali. Hii ni kwa sababu zifuatazo:
Sasa, hili siwezi kukuamulia. LinkedIn wametoa post moja hapa. Na nyingine hii hapa. Skills kama vile copywriting, digital marketing, ecommerce na local language creation zina nguvu kubwa katika kukusaidia kufikia malengo yako.
Amua skill inayokufaa. Halafu...
KOMAA NAYO.
Kuna kitu kinaitwa "The Valley of Disappointment. Mwandishi James Clear ameielezea vizuri:
Iko hivi. Unapoanza chochote kwa mara ya kwanza, unakuwa kama anayeyeyusha barafu. Utapasha wee, usione tofauti. Ila kuna nyuzi joto fulani ukigonga, unaanza kuona matokeo. Maji! Ni mwa sababu ulikomaa kutia joto, vinginevyo hungeyeyusha hilo jiwe.
Line yii ya kazi (na line yoyote ya mafaninio) ipo hivyo. Komaa mpaka uishinde. Usihame hame. Shika kitu kimoja, jifunze vizuri, komaa nayo. Ukishindwa jiulize "kwa nini". Jaribu tena. Na tena. Siku moja, barafu itayeyuka...
Hii skill ni MUHIMU. Kuna wengi (imenikuta) wanapata kazi nzuri halafu inayeyuka kwa sababu ya kupoteza njozi ya kazi. Kuelewa kinachohitajika. Kukifanya kwa wakati, na weledi.
Kwa bahati mbaya ajira zetu za humu (hasa serikalini), zinawaponza vijana. Wengi wanapenda hizo kazi kwa sababu hazina mambo mengi. Anakaa katika ofisi fulani wilayani miaka 5, lakini self management haipo. Anaingia kazini kwa kuchelewa. Anatoka kabla ya wakati. Kazi zenyewe zinacheleweshwa kwa kuwa kuna baadhi ya ofisi hazina usimamizi mzuri.
Nidhamu binafsi ni ngumu, lakini ni muhimu. Hasa pale ambapo hakuna anayekufuatilia. Pale ambapo huna ofisi ya kuripoti saa2 na kuaga saa11.
Itabidi ujifunze kutumia software kama Trello, Infinity, Monday, na zingine kama hizo ambazo zina time management components. Jifunze kuweka malengo na kuyafikia.
Fahamu namna ya kupush bidhaa, huduma na skills ulizo nazo. Unaweza kutumia website yako (somo la siku nyingine), mitandao ya kijamii, whatsapp na email.
Chukua muda wa kuelewa wapi wateja wako huweka vijiwe, halafu wafuate huko. Washindani ni wengi. Soko ni pana na lenye ushindani mkali. Kitakachofanya watu waje kwako ni utofauti wako katika ushindani hii (Unique Selling Point).
natumaini mmeamka salama. Mimi pia, nipo kwenye computer yangu nachapisha haya maneno.
Katika pitapita zangu, nilikutana na hili swali leo asubuhi, kwenye X account ya rafiki yangu mafolebaraka
Nkatamani kulijibu kwa post kadhaa, kuanzia hili la leo.
Binafsi, sijaajiriwa hapa nchini tangu 2019, kabla ya Korona. Na nina familia ya watoto watatu, mke mmoja na watu wengine wanaonitegemea.
Miaka hiyo yote nimegundua kuwa kufanya kazi mtandaoni (online work) ni mojawapo ya sulihisho kwa upungufu wa ajira hapa nchini. Leo, ntakupa baadhi ya vitu vya kuzingatia ili kufaniniwa. Twenzetu...
Cha 1: Embrace Digital Literacy (Tafuta Uelewa wa Masuala ya Kidigitali)
Dodoso: Uchumi wa kidijitali duniani unatarajiwa kufikia dola trilioni 4.8 ifikapo mwaka 2025.Mtandao umebadilisha namna tunavyofanya kazi na kupata pesa. Kwa kujua hili, tuangalie ujuzi wenye faida na unaohitajika sana unaolingana na mabadiliko haya ya kidijitali.
Hii ni pamoja na uelewa wa jinsi ya kutumia computer, mtandao kwa ujumla na upekee wake, na software (programu mbalimbali) kikamilifu.
- Angalizo: Hatua hii ni muhimu mno. Ndo utimgongo wa kazi za mtandaoni. Bila uelewa mzuri, utapata taabu katika mawasiliano, na kujifunza vitu vipya.
- Takwimu: Hapa Africa, chini ya asilimia 50 za shule zetu zinakazia ufundishaji wa stadi za kompyuta (ikilinganishwa na 85% ughaibuni).
Cha 2: Learn Communication Skills (Jifunze Mbinu za Mawasiliano)
Kuna haja ya kujua namna ya kuwasiliana kwa maandishi na kwa maneno (digital and verbal communication).Utahitaji kujua namna ya kuwasilisha bidhaa na huduma unazotoa, kwa namna itakayowavutia watu wengine. Aidha, unaweza kujifunza lugha zaidi ya moja (endapo unatamani kufanya biashara/kazi nje ya mipaka ya nchi hii).
Jua namna ya kuandika meseji kwa weledi. Jinsi ya kuandika barua za kuomba kazi. Namna ya kujibu maswali. Jua jinsi ya kuwasiliana kwa mara ya kwanza na mteja mtarajiwa unayetegemea kumuuzia bidhaa baadaye (cold pitching to a prospective client). Fahamu namna ya kuuliza maswali ili kupata unachokitafuta.
Na, kuna wengi walisema "Kiingereza ni Janga la Taifa". Lakini kumbuka kuwa maisha yako yanategemea sana namna unawasiliana na watu wa kwenu (hata kiswahili huwatatiza wabongo wengi) na wasio wa kwenu.
Kumbuka: Chochote anachoweza kujifunza mwenzako Uganda na Kenya, na wewe unaweza kujifunza.
Cha 3: Have a Specialized Skill (Bobea kwenye Ujuzi Fulani)
Nina uhakika kwamba unaposoma haya, una umri zaidi ya 18. Maana yake, huenda ushamaliza form 4, au form 6, au upo chuoni.Tambua vitu unavyoweza kuvifanya kwa uzuri. Hapa nazungumzia digital soft skills (uwezo wa kidigitali). Zipo nyingi na siwezi kukuamulia. Ila kuna moja aisee naomba uanze nayo.
Prompt engineering (kutumia mfumo wa akili mnemba wa kuuliza maswali).
Kabla hujaenda mbali, nakushauri sana sana kutumia muda wako kupata ujuzi wa kutumia platform za AI, na jinsi ya kuuliza maswali. Hii ni kwa sababu zifuatazo:
- Dunia imehama: Mpaka 2030, mfumo wa akili mnemba itachangia dola trilioni 15.7 kwa uchumi wa ulimwengu. Kila atakayemega kidogo humo anashuriwa kuzamia na kujua namna ya kuitumia na kuifaidi.
- Prompt engineering (namna ya kuuliza maswali ya AI) itakusaidia kupata idea ya vitu mbalimbali (kama nnavyofanya sasa nnapoandika makala haya), kupiga kodi (nilitengeneza programu ndani ya siku mbili. Programu kama hiyo ilinichukua wiki tatu 2019), kudadavua data nk.
- Waandishi hello! Akili mnemba itakusaidia katika uandishi. Umeamka hujui cha kupost kupromote bidhaa insta. Iulize ChatGPT. Unataka kuanzisha kampeni ya barua pepe? Mwambie Gemini. Na vingine kama hivyo...
- Kuwa mbunifu na chukua hatua za haraka. Zamani za boda za baiskeli, waendeshaji walihangaika kupanda mlima. Lazima ungeshuka na jamaa akokote hadi itakapokuwa rahisi kukupakia.
Siku hizi? Pikipiki zinapenya popote. Wajanja wa baiskeli walilazimika kujifunza kuendesha pikipiki ili kuendana na mabadiliko. Mfano huu utoshe kukushauri cha kufana.
Sasa, hili siwezi kukuamulia. LinkedIn wametoa post moja hapa. Na nyingine hii hapa. Skills kama vile copywriting, digital marketing, ecommerce na local language creation zina nguvu kubwa katika kukusaidia kufikia malengo yako.
Amua skill inayokufaa. Halafu...
KOMAA NAYO.
Kuna kitu kinaitwa "The Valley of Disappointment. Mwandishi James Clear ameielezea vizuri:
Iko hivi. Unapoanza chochote kwa mara ya kwanza, unakuwa kama anayeyeyusha barafu. Utapasha wee, usione tofauti. Ila kuna nyuzi joto fulani ukigonga, unaanza kuona matokeo. Maji! Ni mwa sababu ulikomaa kutia joto, vinginevyo hungeyeyusha hilo jiwe.
Line yii ya kazi (na line yoyote ya mafaninio) ipo hivyo. Komaa mpaka uishinde. Usihame hame. Shika kitu kimoja, jifunze vizuri, komaa nayo. Ukishindwa jiulize "kwa nini". Jaribu tena. Na tena. Siku moja, barafu itayeyuka...
Cha 4: Self Management (Kujitawala)
Hapa sasa. Nidhamu ya kazi ni muhimu sana sana. Unapaswa kuwa na: nidhamu ya kazi (discipline), utunzaji wa muda (time management), kuweka malengo na kuyafikia (goal settting and achievement).Hii skill ni MUHIMU. Kuna wengi (imenikuta) wanapata kazi nzuri halafu inayeyuka kwa sababu ya kupoteza njozi ya kazi. Kuelewa kinachohitajika. Kukifanya kwa wakati, na weledi.
Kwa bahati mbaya ajira zetu za humu (hasa serikalini), zinawaponza vijana. Wengi wanapenda hizo kazi kwa sababu hazina mambo mengi. Anakaa katika ofisi fulani wilayani miaka 5, lakini self management haipo. Anaingia kazini kwa kuchelewa. Anatoka kabla ya wakati. Kazi zenyewe zinacheleweshwa kwa kuwa kuna baadhi ya ofisi hazina usimamizi mzuri.
Nidhamu binafsi ni ngumu, lakini ni muhimu. Hasa pale ambapo hakuna anayekufuatilia. Pale ambapo huna ofisi ya kuripoti saa2 na kuaga saa11.
Itabidi ujifunze kutumia software kama Trello, Infinity, Monday, na zingine kama hizo ambazo zina time management components. Jifunze kuweka malengo na kuyafikia.
Hatua ya 5: Sales and Digital Marketing (Elewa Mfumo wa Kuuza na Kununua Mtandaoni)
Mtu aliwahi kusema humu "NO SALES NO BUSINESS". Bila mauzo, hamna biashara. Kila kampuni yenye mafanikio huwa na vitengo vya masoko na mauzo.Fahamu namna ya kupush bidhaa, huduma na skills ulizo nazo. Unaweza kutumia website yako (somo la siku nyingine), mitandao ya kijamii, whatsapp na email.
Chukua muda wa kuelewa wapi wateja wako huweka vijiwe, halafu wafuate huko. Washindani ni wengi. Soko ni pana na lenye ushindani mkali. Kitakachofanya watu waje kwako ni utofauti wako katika ushindani hii (Unique Selling Point).
Hoja za Ziada
Wakati umekuja wa kutatua matatizo yetu ya Afrika kutumia uwezo wa mtandao na teknolojia. Ukiangalia na kuchunguza, shida za Afrika zina upekee sana ukilinganisha na nchi za wenzetu zilizoendelea.Tovuti 5 zinazotoa Kozi za Mtandaoni
- Coursera: Inatoa kozi kutoka vyuo vikuu na taasisi maarufu duniani, nyingi kati ya kozi hizi hutolewa bure.
- edX: Inatoa kozi za bure kutoka vyuo vikuu vya juu kama MIT na Harvard.
- Khan Academy: Inatoa mafunzo ya bure kwa masomo mbalimbali, kuanzia sayansi, hesabu hadi historia na sanaa.
- Alison: Inatoa maelfu ya kozi za bure katika nyanja mbalimbali kama vile teknolojia, afya, na biashara.
- Udemy Ingawa kozi nyingi ni za kulipia, Udemy pia inatoa kozi nyingi za bure katika nyanja mbalimbali.