Chalamila, serikali wanapotutaka kulipia huduma za serikali wanajua malipo tunayolipa serikalini bila kupewa risiti ni kwa maslahi ya nani?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
31,673
41,711
Hii ni mifano halisi kwa malipo ya serikali bila risiti:

1. Huduma za afya hospitali ya wilaya Sengerema.

2. Kupita juu ya daraja la Busisi ili kuepuka adha ya ferry hasa nyakati za usiku.

Kwamba huu kumbe ndiyo ulio utaratibu wa kawaida Sengerema huku!

Kulipishwa huduma kwa niaba ya serikali bila kupewa aina yoyote risiti, na maisha yanaendelea, business as usual?

Hivi TRA wanaosema kutodai au kutokutoa risiti kwa huduma au manunuzi madukani huko au wahusika wowote hawayaoni haya?

Kwamba hali hizi zinaendelea hivi bila vigogo haswa, kunufaika?

Kwamba pesa kiasi gani zinapotelea mifukoni mwa wajanja kwa siku?

Kwamba daraja la Busisi litakamilka kweli, kwa mtaji huu?

Kwamba huduma zipi za afya hata zitakuwa endelevu?

Ama kweli:

"Viva Donald Trump kwa kutambua hatustahili hisani ya watu wa Marekani wakati kumbe, vitulacho vi nguoni mwetu!"

Brazaj J,
Mapumzikoni
Sengerema
 
Back
Top Bottom