The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 1,141
- 1,944
Serikali imeeleza sababu za kukamatwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, katika eneo la Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema Heche amekamatwa kutokana na kuendesha mkutano katika eneo lisiloruhusiwa kisheria.
Chalamila amesema ni muhimu wanasiasa kuheshimu taratibu za kufanya mikutano ya hadhara na kwamba sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayekiuka.
Aidha, Chalamila amezungumzia tetesi za kuwapo kwa kundi la watu wanaopanga kufanya maandamano tarehe 24 mwezi huu, akisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuhakikisha amani inadumishwa. Ametoa wito kwa wananchi kufuata sheria na kuepuka kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali.
Serikali imesisitiza kuwa haitafumbia macho vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa nchi.