Chaguo la MUNGU Linalohitaji Mizengwe ya Mwanadamu Kufanikiwa

Wanasiasa kuiona mbingu ni jambo gumu sana maana siasa zilivyokaa kinafiki na kiujanjaujanja kwakweli ni ngumu, kama hujawahi shiriki siasa hutalielewa hili ila siasa na ucha mungu ni ngumu sana haviungani kuna mambo utaenda kinyume na chama cha siasa ulichopo na utafukuzwa kama utakua mcha mungu.
Maana vyama vya siasa kupanga hila ni jambo la kawaida
Mkuu sisi wanasiasa wengine hatuna shida , tatizo ni wanaccm .
 
Nionyeshe kokote kuliko na utawala kamilifu hapa duniani, utawala usio na dhambi, utawala usiodanganya raia ili kutawala. Nionyeshe hata sasa nitafunga virago na kuhamia huko hata iwe Mars!
Sina hakika kama kwenye maelezo yangu nimeonyesha kuwa kuna utawala usio na dhambi, nchi au mtu! Hata hivyo sina maana kwa kuwa tawala zote hutawala kwa dhambi basi tawala hizo hubarikiwa na Mungu. Moreover, hatupaswi kuhalalisha dhambi kwa sababu hata tawala au mtawala mfulani pia anatawala au alitawala kwa dhambi. Kuna misemo, hata maandiko yaliandikwa ili kuhalalisha uovu wa viongozi kama, viongozi huchaguliwa na Mungu, Chaguo la wengi ni chaguo la Mungu, Ya kaisari mpe kaisari nk!
 
Mungu aliumba vitu vyote.
Mada inakosa mwelekeo. Ni kwamba kama kuna kiongozi ni chaguo la Mungu kutuongoza kweli ina hitajika nguvu ya ziada, ghiliba, ubabe na wizi wa kura ili awe yeye?
Alichokichagua yeye kutushawishi kusema ndio haihitaji kupiga ramli au kuloga
 
Back
Top Bottom