CHADEMA yaiiga ODM kuhusu Sera ya Majimbo

Umeona eeh? kuna thread mbili tatu hivi hadi zinachekesha.

Hizi mimi nazichukulia kama attacks personal
Kutokana na hilo basi mimi sina muda mchafu wa kutukanana.
Therefore nina honest posting moja kwenye mjadala huu halafu basi!
 
Kwa wale wote ambao wameona kuwa nimewa disrespect...Then nawaomba wanisamehe.
Nawaomba pia wajue kuwa i am used to debates!
Na sijawahi kwenda personal huwa nakwenda kwa hoja!

Nina oni langu la mwisho kabla sijaacha rasmi kuchangia kwenye thread hii!

Naomba wakati mkiendelea na mjadala huu muzingatie jambo moja kuu ambalo limewaamsha watanzania walio wengi wakati huu wa mpito.

Mojawapo ambalo ndilo limepelekea baadhi yetu kujiunga na hii forum toka ikiwa Jambo Forums ni UFISADI!

Lolote tutakalojadili mustakabali wa Taifa letu lizingatie nyenzo muhimu zitakazo weza kuuzika UFISADI once and for all.

Kuna watu ambao nimepingana nao humu ndani ambao wanadai kuwa system ya sasa si mbovu bali ni viongozi.
Naomba nitoe mfano mmoja wa Marekani!
Rais hawezi tu kufanya maamuzi muhimu yanayowagusa wananchi kabla ya kupeleka issue kujadiliwa kwenye House na Congress. Tukiwa na utaratibu kama huo basi hatuwezi kuwa na dikteta labda sisi wenyewe tukubali!
Chochote anachokifanya Bush si yeye wa kulaumiwa!
Bali wote wale waliokubaliana naye na kuzi endorse ideas zake.
Hivi sasa mafisadi hawawezi kuwajibishwa na mtu tunayemuangalia ni Muungwana!
Sasa kama marekani ingekuwa the same..Yule swahiba mkuu wa Bush aliyekuwa bilionea wa marekani Ken Lay si angekuwa anadunda mtaani leo kama system ingekuwa kama yetu? Mtu aliyewahadaa wananchi na sheria ikachukua mkondo wake huku swahiba wake mkuu Bush akitumbua mmimacho tu!

Kama siasa zao zingekuwa kama zetu...Then swahiba wake Bush,na Cheney na pia kingozi mwandamizi mwenye ushawishi mkubwa Karl Rove asingekuwa matatani hivi sasa.

Mifano iko mingi tu!
Ila kwa sasa naishia hapa na kila la kheri kweye mjadala!
Mimi niliuchagua mjadala huu licha ya kwamba kuna ule wa Chenge ambao kila mtu yumo humo hivi sasa.
Na mimi pia nimeanzisha mijadala mingine ambayo watu wanaitikia mwito..Ila bado huwa nasimama kwenye mijadala mingine na kudondosha mawili matatu!
Ila ule usemi wa wakikosa hoja.....
Usije kuendelea pindi mnapoendelea na mjadala huu!
 
Asante kwa kugundua hilo, na mimi naongeza Zanzibar itakuwa jimbo gani?Halafu ni vyema CHADEMA wakasema wanatarajia uundaji wa serikali hii uchukue muda gani kukamilika?

Kwa kifupi iwapo serikali ya CHADEMA haina mpango wa kuwa ya kidikteta basi fikra zao hizi zitaishia kwenye maandishi tu.

Yaani mwandishi wa mapendekezo haya anaandika kama mtu aliyekuwa anasafiri na ngalawa akakuta kisiwa ambacho hakuna mtu anayeishi akaamua kuwaita watu wakae na waunde serikali!

kwanini nasema hivyo? je mwandishi anajua hatua zitakazotakiwa kupitiwa ili kuondoa cheo cha waziri mkuu?amejiandaa vipi na hatua hizo mpaka anaahidi kukiondoa cheo hicho kama si dikteta?
Katika hizo wizara nne ni ipi itashughulikia hospitali za rufaa?

Maswali ni mengi,ila kila atakayesoma mipango hii ya CHADEMA ataelewa vizuri ni kwa kiasi gani hawako tayari kuongoza nchi.

The fact that Ruvuma and Zanzibar were ommited from this master plan, it tells me that whomever created the plan and those who reviewed it and endorsed the plan were reckless and careless just as the plan itself appears to be.

This is not good for Chadema at all. Na hili mmewapa CCM nafasi ya kuwachafulia jina wakati tunajiandaa kwa uchaguzi wa 2010!
 
Mabadilko ya current system ni YA LAZIMA!
Sisi tuwasubiri tu hawa viongozi wetu wailete mijadala hapa na tuijadili..Tusiende nje ya hapo!

What is wrong with current system? could you outline what are the problems of current system and how can the new system fix these problems?

Please give us details and specifics and not simple generalization of issues.
 
Lakini hii system ambayo fisadi hawezi kuguswa hadi JK aamue ndiyo mnayoitetea wewe na Kishoka?

Mushi,

Tatizo la Tanzania si kukosekana sheria au mfumo mbovu. Tatizo la Tanzania ni Uongozi mbovu period!

Tukiwa na uongozi makini ambao unafuata sheria zilizopo, unatumia haki na kujali utu, basi tusingekuwa na matatizo tuliyonayo leo hii.

Sheria za kunyonga mafisadi zipo, tatizo la Uongozi na Serikali ya CCM ni kuwa wamenufaika na kuingia madarakani na kuendelea kuongoza kutokana na kunufaika kwa uvunjaji sheria na kanuni ambao wameufungia macho kwa muda mrefu na sasa hivi wanaogopana maana wataangamia wote.

Mimi simtetei JK au kusema anachosema ni sawa. Hiyo kauli yako hapo juu kuwa Mkandara na mimi tunamtetea JK ni ya UONGO!

Kama si ya uongo, basi mwenzetu huelewi kwa kina matatizo ya Taifa letu na kinachotokea sasa hivi ndio maana unakimbilia kudai tupewe mfumo mpya bila kujua chimbuko la matatizo na kwa nini matatizo haya hayapatiwi ufumbuzi. Ukisoma ile thread yangu ya Illegitimate Kingdom utaelewa ni kwa nini kuna ubutu kutoka serikali kuu kusafisha ufisadi.

Kinachohitajika kuleta mabadiliko Tanzania ni mabadiliko ya Uongozi na si mfumo mzima wa utawala.

Tanzania ikipata Kiongozi makini, mchapa kazi mwenye kujali maslahi ya Taifa, hizi kero zitaanza kuondoka.

Kikwete aliletwa kwa makusudi madarakani na wale wote ambao wamehusika na ufisadi na uhujumu kwa kuwa walikuwa wanajua fika hana uwezo wa kuchukua hatua kali. Kitu ambacho "mafia" hawa hawakukifikiria ni mwamko wa wananchi na kuwepo na kundi na jumuia kama JF ambayo iko mstari wa mbele kupiga vita dhuluma na hujuma.

Kikwete aliutaka Urais kwa mbwembwe, lakini sasa yanamtokea puani! Ni sawa na kumumunya samaki mtamu halafu kamfupa kanaingia kooni chubwi! ni kazi kuutoa huo mfupa!
 
Huwezi kumlaumu mwizi wakati hujafanya jitihada za kujilinda na mwizi ambaye saa nyingine ni watu ambao tunawaamini? Wako miongoni mwetu!
Huwezi kumwanini kila mtu!
System ikiwa nzuri tutaweza kujilinda na mawazo mabaya ya mafisadi ambao huwezi kutegemea kuwa ni watu wazuri na hivyo kusema kuwa system ni nzuri so hawata i missuse! Wamekuja madarakani wakitangaza mali na wakiondoka wanatutisha na vyombo vya dola huku wakituacha hoi kwa"Absolutely Poverty"
Maana yangu kamili ni kuwa huwezi kusema kiongozi/viongozi wasipowekewa taratibu ambazo zitawabana kufanya ufisadi basi watakuwa malaika na kuacha ufisadi under he same system!
Sytem ndiyo mtego unaowafanya waibe!
Wengine wana nia nzuri lakini system ni sawa na "PAJA NJE MZEE!"
SYSTEM=UNA'NTEGA?

Mushi,

Let say Chadema wanashinda Uraisi, wanapata 30% ya viti vya Bunge, je watawezaje kubadilisha mfumo? Ama Upinzani mzima unapata 55% ya viti vya Bunge, je watabadilishaje mfumo ikiwa katiba na kanuni za uendeshaji wa Bunge vinasema ni lazika kura ya kubadilisha kitu iwe 66%?

Let say Chadema wanafanikiwa kubadilisha mfumo kama Mushi anavyoutaka, lakini watendaji wanabakia ni wale wale. Baada ya miaka mitano Chadema wanapoteza uongozi wa nchi Ikulu na Bunge, CCM inarudi kwa nguvu mpya au CUF inaingia madarakani, je kutatokea nini?
 
Zitto,

Kwa nini Chadema isifanye msukumo wa kutaka kuundwa kwa Katiba Mpya ya Tanzania ili kukidhi mahitaji ya Tanzania na kwa mazingira yetu na si kukimbilia kuiga ya Afrika Kusini au Canada?

Je hili suala la majimbo ni njia moja ya kukwepa kutangazia umma kuwa Chadema inataka mchakato wa Katiba mpya?

Je kuna ubaya gani mkirekebisha mfumo uliopo sasa hivi wa mikoa na kuondoa mamlaka ya kuteua watendaji na wakuu wa mikoa na wilaya kuota kwa Raisi na kuyafanya yawe mikononi mwa wananchi kwa kupigiwa kura?

Je mkishaunda hayo majimbo, yatakuwa na sheria zao binafsi na kuwa na mabunge yao ya kimajimbo ziada ya Bunge la serikali ya shirikisho?

Pemba wanadai uhuru wao wawe na serikali yao ndani ya Muungano tofauti na Zanzibar, je itakapofikia Kagera wakasema hawataki kuwa jimbo moja na Shinyanga mtawapa ruhusa?

Je hii ndiyo njia pekee ambayo Chadema inafikiri itakuwa suluhisho la
matatizo ya Tanzania?

Moelex kaongea vizuri sana kuhusu CCM kwenda uchagani na kusema Chadema wanataka kuzuia mapato ya madini yasitumike nchi nzima, yatumike Usukumani pekee, je mlipokuwa mnaandika hii sera mlilifikiria hili? maana katika sera hamna mahali mnapoonyesha ni jinsi gani serikali kuu ya shirikisho itapata mapato yake na ni jinsi gani Serikali kuu itajiendesha na kusimamia maendeleo ya Taifa.

La mwisho ni la sheria, ikiwa kila jimbo litakuwa na sheria zake, hivyo mnatutamkia wazi kuwa kunaweza kuwa na mgongano wa kisheria kati ya majimbo na hata serikali kuu, je ni sheria gani zitakuwa na nguvu bila wananchi kuona wanaonewa?
 
Rev,

Maswali yako mengi na magumu sana. Kiukweli tumetafakari sana juu ya mfumo huu wa majimbo na tukaona kuwa itasaidia sana nchi kuendelea kwa haraka kwa kutumia rasilimali zilizopo maeneo ya majimbo. Mlicholetewa hapa ni rasimu sifuri ili kupata michango na baadae kupata rasimu ya kwanza na kisha kuipitisha katika vikao na kuwa sera rasmi.

Madai ya Katiba Mpya ndio ajenda ya kwanza ya chama chetu na ushirikiano wa vyama vya upinzani. Sera ya majimbo tukitaka ipite ni lazima iingie katika mfumo mzima wa katiba na hivyo katiba mpya ni suala la lazima.

Sasa kuna mawazo kadhaa kuhusiana na katiba mpya. Kuna wanaosema ni vema katiba mpya iwe ni ajenda yetu ya uchaguzi na kuahidi wananchi katiba mpya mara tukishinda. Kuna watu wanasema inabidi kuidai sasa na kuingia katika uchaguzi na katiba mpya. Tukipigania sasa maana itakuwa ni katiba iliyoletwa na CCM kwa matakwa yao ya kukaa madarakani zaidi. Tukisubiri ni nini maana yake kama tusiposhinda kufuatia wananchi kutoona umuhimu wa katiba mpya.

Njia ya kati hapo ni kuwa na minimum demands ili uchaguzi uwe huru, kubadili mfumo wa uchaguzi na kuweka uwanja wa kisiasa sawa. Tukifanikiwa hili ndio tuanze kazi ya katiba mpya.

Kiukweli tunataka mfumo wetu uwe ni wa Kitanzania zaidi. Uzingatie umoja wa Taifa letu, Muungano wetu na juhudi za kuondoa ukabila zilizofanikiwa sana. Mifano ya Kanada tumetoa tu. Mfano wa Afrika Kusini ni mzuri kwetu kwani wao licha ya kuwa sio Shirikisho lakini wana majimbo yaliyo na uhuru

Kwamba mapato yoote yatabaki majimboni sio kweli. DRC wamegawana Taifa 60% na Majimbo 40. Kuna kodi zitakusanywa na majimbo na nyingine zitakusanywa naTaifa na pia hata serikali za mitaa zitakuwa na ushuru zinaokusanya.

Kwa vyovyote vile majimbo yatakuwa na mabaraza yake ya wawakilishi na watakuwa na uwezo wa kutunga sheria zinazohusu Jimbo husika. Watakuwa na Mkuu wao wa Mkoa (Premier) atakaetokana na chama chenye wabunge wengi ndani ya Baraza la Wawakilishi la Mkoa.

Zanzibar itakuwa na Serikali yake kama sasa bila ya kuwa na Rais maana Rais atakuwa ni wa Muungano tu. Lakini Pemba itakuwa na Premier wake na Unguja Premier wake na mabaraza yao ya kutunga sheria. Mji Mkongwe utakuwa ni city-state kama itakavyokuwa Dar es Salaam.

Kishoka, we mean it. Help us
 
Zito

Rev,ameuliza very clear cut question "nini ubovu wa system tulionayo sasa?"

Ni ufahamu wangu kwamba unapotaka kufanya mabadiliko tena makubwa kama yaho, nilazima uweke wazi mapengo yaliopo sasa ndio , halafu uonishe na hiyo system yrnu mpya na ni jinsi gani itafanikiwa kuziba mapengo hayo.

Kwa mfano angalia tu hoya yako kwamba; kila jombo liwe na balaza lake la kutunga sheria, huo tu ni kuuongezea mzigo serikalii kwani mtafanya muwe na very big government ambayo kuindesha kwake itakuwa ni mzigo mkubwa kwa wananchi.

Kuhusu umoja wa nchi utakuwa very week,majimbo tajiri hayataona umuhimu wa kuendelea kusaidia majimbo yasiokuwa na kitu hivyo serikali kuu ikizidi kilibada jimbo hilo kunauwezekano likaamua kujitoa.

Maoni yangu nomamba mkae chini muingalie kwa undani systerm tulionayo sasa
mkipata makosa yako wapi mtakuwa na more than one option, kama mzibe mapengo yaliopo to which I think will be easy and cost effective , au mo introduce the whole new system amboyao nadhani kama mko madarakani mtatumia sio chini ya miaka mitatau ya mwanzo kuwafanya wananchi to get used to it

Ushauri wa bure:Wakati mwingine tusifikilie mabadiliko for just a sake of madaliko.(change just for the sake of change)
 
Very big government kwa kuwa na Majimbo na Baraza la wawakilishi na Jimbo? Hii si kweli. Hii maana yake ni kuwa tunashusha utawala kwa wananchi. Majimbo yatashindana kuvutia wawekezaji wa ndani na wa nje. Majimbo yatatumia 'comparative advantage' na pia competitive advantage katika kujipanga kimaendeleo. Shughuli za kiuchumi zikiwa kubwa zaidi kodi inayokusanywa inaongezeka na hivyo kupanua shughuli za miradi ya maendeleo.

Mfumo wa sasa una mapungufu makubwa sana. Mfumo huu unaifanya mikoa itegemee kila kitu kutoka Dar. Mtu mmoja pale wizara ya fedha ndie anayeamua mkoa gani upate nini na katika mradi gani. Hakuna ushirikishwaji wa wananchi na viongozi wa mikoa katika upangaji wa maendeleo na hata Bajeti.

Kuna vyanzo vingi vya mapato katika 'informal sector' lakini TRA haiwezi kufika huko kwani haina uwezo. Mikoa itakapokuw aiankusanya baadhi ya mapato yake yenyewe itakusanya mapato yote.

Leo mkoa ukitaka walimu au mabwana shamba au mabibi afya ni lazima wapate kibali kutoka utumishi dar es salaam na hivyo inachukuwa miaka mingi sana. Serikali za Mikoa zilizo na uhuru kiasi zitaondoa urasimu huu. Kimsingi serikai ya majimbo inafanya maamuzi kwa haraka na kwa kuzingati mahitaji ya Mikoa husika. Ninatumia neno mikoa kwa kubadili badili na majimbo ili kuonesha kuwa jina sio hoja sana bali mfumo wa utawala.

Hayo ni baadhi ya mapungufu na ni vipi mfumo mpya waweza kuyaondoa. Tuangalie mapendekezo ya chadema in broader picture tafadhali. Nadhani mfumo huu ni mzuri sana na utatufaa iwapo tutazingatia umoja wa Taifa letu, Muungano wetu na mshikamano wa kitaifa. This is not change for the sake of change. It is change for development and emancipation of the people!
 
Rev,

Maswali yako mengi na magumu sana. Kiukweli tumetafakari sana juu ya mfumo huu wa majimbo na tukaona kuwa itasaidia sana nchi kuendelea kwa haraka kwa kutumia rasilimali zilizopo maeneo ya majimbo. Mlicholetewa hapa ni rasimu sifuri ili kupata michango na baadae kupata rasimu ya kwanza na kisha kuipitisha katika vikao na kuwa sera rasmi.

Zitto,

Nafurahia kuwa unanielewa na unajua ni kwa nini kuna maswali magumu na si kama ndugu wengine humu ambao wanafikiri kuwa kuhoji ya Chadema au upinzani ni kuwa vibaraka wa CCM na Kikwete.

Safari ya kulijenga Taifa upya ni ngumu sana na inahitaji ushirikiano wa kila mtu. Kama Chadema wanaanza safari hii na wanashirikisha wananchi katika mchakato mzima, basi Mungu akitujalia, tutajiunda upya na kuwa na mfumo ulio bora (Katiba, Sheria, Dola, Utawala na Uongozi) ambao utatusaidia katika safari yetu ya kusukuma gurudumu la maendeleo na vita dhidi ya Ujinga, Maradhi na Umasikini.

Azimio la Arusha lilisema tunahitaji kujenga jamee yenye kutumia Juhudi na Maarifa ili kushinda hao maadui watatu na kutufanya tuwe Taifa la watu wenye kujitegemea.

Ni wajibu wenu Chadema kulikumbuka hilo na kuhakikisha ushirikishi kwa wananchi na uafiki pamoja na utekelezaji.

TUnaomba isiishie kuwa kama Ilani za CCM ambazo ni nzuri na zinafaa kutuondoa katika umasikini ila ni utashi binafsi na wa makusudi ilani hizo zimebakia kuwa ni mapambo badala ya kufanyiwa kazi.
 
Rev

Ilani ya CCM haijawahi kuwa nzuri. Ni wish list tu. Ilani ni policy pronouncement in five years sio orodha ya miradi. Hapa kaka sikabaliani nawe. Ilani za CCM is a mere wishlist! Umemsoma Jenerali wiki hii?

Mtindo huu umetumika wakati wa mfumo wa chama kimoja, na unatumika hadi leo. Kinachojitokeza kutokana na mtindo huu ni kile kinachoitwa wish list, au orodha ya matamanio. Matamanio kila mmoja anayo yake, lakini hayawezi yakawa ilani ya uchaguzi.

Ilani ya uchaguzi haina budi kurejea kwanza misingi yake ya kifalsafa inayokifanya kiwe chama, ndiyo kusema jumuiya ya wananchi waliojiunga pamoja kutokana na ya imani ya kimsingi inayowaweka pamoja, kwa lengo la kuchukua uongozi wa nchi ili watekeleze malengo ya falsafa yao kwa kutenda yale wanayoamini ni ya msingi katika kuleta maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
 
Zitto,
Naomba kidogo niulize kitu hapa.. Unaposema Zanzibar itakuwa na Serikali yake kama sasa! hapa mkuu una maana gani kwa sababu huwezi kuwa na nchi inayoitwa Tanzania lakini ndani yake kuna serikali mbili tofauti zenye serikali ndogo tofauti ktk majimbo, unless mnachojaribu kubadillisha hapa ni kuondoa neno mikoa kuipa jina la MAJIMBO na kitakacho badilika sana ni ukubwa wake...Nikipiga mahesabu nashindwa kwanza kuelewa ukubwa wa bunge zake halafu utawalka wenyewe kuhusiana na serikali kuu.
Nimeuliza hivyo kwa sababu nashindwa kuelewa uzito wa kiuongozi kati ya jimbo moja la serikali ya Muungano na ile ya serikali ya Zanzibar.. Hapa kutakuwa na serikali kuu, kisha serikali ipi kati ya majimbo na serikali ya Zanzibar inayofuatia kwa daraja maanake sioni nafasi ya serikali hii ya Zanzibar ktk mfumo mzima wa serikali kuu na majimbo yake..

Pamoja na yote haya mkuu tumekuwa tukiongeza mikoa kila baada ya muda kwa malengo kama haya lakini kama leo utaniuliza mimi tofauti iliyopo kati ya wakati wa mkoloni, Nyerere na baada ya kuongeza mikoa hiyo...Mabadiliko yapo lakini kama lengo ni KIUCHUMI kungeza ufanisi wa maendeleo kwa wananchi ktk maeneno yaliyokuwa makubwa... Mkuu hatujapata kitu kabisa kufikia malengo hayo.
Hii ndio hofu yangu kubwa kuwa sera zinaweza kuonyesha mwanga mkubwa ktk upangaji lakini kama viongozi wake ni watu wasiowajibika, wanaolindwa na nguvu ya dola kukiuka sheria hapa mkuu tutakuwa tunapoteza muda kujenga sera sifuri.

Binafsi nimeona nafasi kubwa ya Chadema sasa hivi ni kuweka mawazo yao ktk swala linalotingisha nchi sasa hivi...UFISADI kuwa slogan ya kupigia debe kwa wananchi. Imeweza kufanikiwa wakati wa hoja yako ya Buzwagi na ile ya EPA ya Dr.Slaa.. Wananchi vijijini leo hii wnamfahamu Zitto nani na Dr.Slaa nani hivyo kwa mtaji huo vyama vyote vya Upoinzani ni kukusanya data ambazo zitatumika wakati wa uchaguzi kuwaangusha viongozi wa CCM iwe ktk Wabunge ama kiti cha Ikulu kwa sababu wote hawa wamekwisha jenga sanamu za kuabudu fedha.. wengi wao wana scandal zilizokuwa dormant zinasubiri tu kulipuliwa. Nina hakika mkikusanya data muhimu basi bila shaka asilimia 75 kama sio 80 ya Bunge mtakamata kwani kati ya Wabunge wengi wa CCM ndio hao viongozi wa wizara zetu zinazochemka na tender za Ulaji..

Na kwa rehma zake mwenyezi Mungu mkichukua kiti cha kutawala kwanza ni muhimu kuhakikisha mnaondoa kabisa vitu kama Azimio la Zanzibar!.. huwezi kuwa na malengo ya kupeleka maendeleo kwa wananchi kwa kuunda Majimbo ikiwa viongozi wenyewe wanaruhusiwa kufanya biashara.. hii ni temptation moja kubwa sana ambayo imewakumba CCM. Binafsi ninaamini kabisa kwamba ni Azimio la Zanzibar ndilo limetuletea hawa Mafisadi, hivyo ni muhimu kwa Chadema na vyama vyote vya Upinzani kuchukulia upungufu huu wa Azimio hilo baya ambalo limekuja waumbua CCM...Hakuna mtu yeyote kama binadamu tena maskini anaweza kuacha kutumia nafasi kama hiyo mahala ambapo wadhifa na sheria zinamruhusu..Kwa bahati nzuri CCM wenyewe wametuonyesha udhaifu wao ktk hilo mopja ya mazimio yao na litakuwa kaburi lao.

Mengine mkuu achaneni nayo kwa sasa sio wakati wake hata kidogo kwani hili moja tu la Muungano hadi leo linatushinda...Zanzibar hadi kesho wanajiona wangekuwa mbali kama sio Muungano na hayo Majimbo kuna mikoa kama Shinyanga watakuja sema hivyo kuwa wangekuwa mbali kama wangebakia mkoa hali wakijua kabisa kuwa mfumo wa mikoa haukuweza zaa matunda miaka yote iliyopita..Watazuka wanasiasa wa kisukuma wenye uchungu na Unyantuzu, will come up with something unajua tena Politicians ulaghai ndio somo kubwa.
 
WanaJamii!

Nimerejea toka ziara fupi ya Mwanza, kule tumezindua ofisi ya Vijana wa Vyuo Vikuu Mwanza, iko pale Nyegezi. Tumezindua pia Ofisi ya Baraza la Vijana wa CHADEMA(BAVICHA) wilaya ya Magu. Lakini kadhalika, tumeanza mjadala wa Sera Ya Mfumo Mpya wa Utawala alias Sera ya Majimbo, vizuri sana. Katika Kongamamano tulilolifanya ndani ya chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, ziadi ya wasomi 1000 walikubali kukaa njaa kuanzia saa tatu mpaka karibu saa 10 jioni wakilisikiliza hoja na kutoa hoja mbalimbali kuhusu sera hii. Kwa ujumla waliozungumza wameonyesha kuikubali sera yenyewe lakini pia pameulizwa maswali na hoja nyingi, mengi ya maswali hayo ndiyo hayo hayo niyaonayo hapa kwenye huu mjadala. Lakini pia tulipokea maoni kwa maandishi na maswali mengi mengi, tunaendelea kuhesabu! Ni ishara ya mapambano ya fikra!

Leo ni blue Monday, hivyo sitaweza kutulia hapa na kujibu hoja kadhaa na kuchangia maoni yangu kuhusu mjadala huu unaondelea. Mimi mtizamo wangu kwa ujumla kuhusu suala hili katika maeneo kadhaa uko tofauti sana.

Lakini nimeona kwa sasa nikumbushe masuala mawili:

Mosi; kwamba hii ni rasimu sifuri kwa lengo la kuibua mjadala; si sera kamili iliyozinduliwa na CHADEMA kwa ujumla wake- kwa hiyo, hata wanaCHADEMA wanapaswa kuwa huru tu kuichambua na kupendekeza fikra mbadala- bado katika hatua ya sasa si msimamo wa chama. Pengine naweza kueleweka nikinukuu maneno yaliyomo katika kila ukurasa wa footnote ya kabrasha la rasimu hii: Rasimu hii ya Sera ya Mfumo Mpya wa Utawala imeandaliwa na Timu Maalum kwa kukusanya na kuchambua sampuli ya maoni ya viongozi/wanachama wa CHADEMA, wadau mbalimbali na wadau mbalimbali. Idara ya Sera ya Utafiti inasambaza rasimu hii ili kupata maoni mbalimbali kabla ya Sera rasmi ya chama iliyofanyiwa marejeo(reviews) kupitishwa kwenye vikao vya kikatiba vya CHADEMA na kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka 2008. Maoni kuhusu rasimu hii yawasilishwe kupitia S.L.P 31191.

Pili: nirejee Makala zangu zangu mbili nilizoandika miaka kadhaa nyuma mara baada ya uchaguzi wa 2005 kuhusu Sera hii. Wakati ule niliandika Makala- Sera ya Majimbo ni Siri ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania; Naamini makala hizi zinajibu baadhi ya maswali ambayo yameulizwa humu- kwa anayetaka kuchambua vizuri michango yangu itayofuata humu kuhusu suala hili, ni vyema kwanza akasoma hizi makala mbili, ambazo zinapatikana hapa:

http://www.chadema.net/makala/mnyika/mnyika_18.html

na Hapa:

http://www.chadema.net/makala/mnyika/mnyika_19.html

Naomba kutoa hoja

JJ
 
Mtu wa pwani,
Chadema hawajachelewa hata kidogo, kwani ifikapo 2010, huenda sera zao zitakuwa muafaka ktk jamii yetu kipindi hiki wajaribu kuelimisha jamii japo kuna changamoto ktk hili, tuombe mola ili siku hizo zije timia.
 
Zitto,
Naomba kidogo niulize kitu hapa.. Unaposema Zanzibar itakuwa na Serikali yake kama sasa! hapa mkuu una maana gani kwa sababu huwezi kuwa na nchi inayoitwa Tanzania lakini ndani yake kuna serikali mbili tofauti zenye serikali ndogo tofauti ktk majimbo, unless mnachojaribu kubadillisha hapa ni kuondoa neno mikoa kuipa jina la MAJIMBO na kitakacho badilika sana ni ukubwa wake...Nikipiga mahesabu nashindwa kwanza kuelewa ukubwa wa bunge zake halafu utawalka wenyewe kuhusiana na serikali kuu.
Nimeuliza hivyo kwa sababu nashindwa kuelewa uzito wa kiuongozi kati ya jimbo moja la serikali ya Muungano na ile ya serikali ya Zanzibar.. Hapa kutakuwa na serikali kuu, kisha serikali ipi kati ya majimbo na serikali ya Zanzibar inayofuatia kwa daraja maanake sioni nafasi ya serikali hii ya Zanzibar ktk mfumo mzima wa serikali kuu na majimbo yake.

Mkandara,

Suala hili ni jepesi sana kuliko unavyodhani. Wala usifikiri sana. Haya ni maoni yangu binafsi kama muumini wa sera ya Mikoa yenye uhuru kiasi (ita Majimbo). Pia mimi ni muumini mkubwa sana wa Muungano ambao haufuti Utaifa wa Zanzibar. Hivyo pendekezo langu ni kuwa na Serikali ya Muungano yenye nguvu Kimamlaka na serikali mbili za Tanganyika na Zanzibar chini ya Mawaziri wakuu (Pure Parliamentary Democracy). Rais wa Muungano ndiye atakuwa anasaini Miswada ya Pande zote kuwa sheria baada ya miswada hiyo kupitiwa na Bunge la Juu (wengine huita Senate, wengine Upper House na kule kwa Madiba wanaita National Council). Bunge la Muungano (senate) litakuwa na wajumbe sawa kutoka Tanganyika na Zanzibar na pia Premiers wa Mikoa yote (Wakuu wa Mikoa wa kuchaguliwa). Ili kulinda maslahi ya Pande zote za Muungano, maamuzi fulani fulani ya Bunge la Muungano yatahitaji 'majority' ya pande zote kwa sheria na theluthi mbili ya Wabunge wa pande zote kwa masuala ya Katiba.

Premiers wa Mikoa (Gavana wa Majimbo) watakuwa wanawajibika kwa Baraza la Wawakilishi la Mikoa. Wawakilishi watapatikanaje? Hili suala la kufikriria kidogo. Mimi ushauri wangu ni kuwa Tarafa za sasa ziwe ni majimbo ya kuchagua wawakilishi katika Baraza la Kutunga sheria la Mkoa.

Hivyo kwa ufupi tutakuwa na vyombo vifuatavyo vya kutunga sheria kutokana na maeneo husika.
1. Bunge la Muungano - Dogo lenye wajumbe sawa kutoka Tanganyika na Zanzibar + Wakuu wa Mikoa (Provincial Premiers). Rais wa Muungango na Makamu wake (Makamu wa Rais kuwa Mkuu wa shughuli za Serikali ya Muungano katika Bunge la Muungano- Senate/National Council)

2. Bunge la Zanzibar na Bunge la Tanganyika. Waziri Mkuu Zanzibar na Waziri Mkuu Tanganyika
3. Baraza la Wawakilishi la Mkoa. Premier (Mkuu wa Mkoa)
4. Halmashauri ya Wilaya. Meya Mtendaji (Executive Mayor)

Mkandara umenielewa au nimekuchanganya zaidi? Tuendelee kutoa mchango na yale nitakayoweza nitajibu, nitakayoshindwa nitasema siwezi
 
Heee, Nisaidieni jamani.
Naona kama mfumo wa majimbo hauko mbali sana na utaratibu tulionao wa 'Decentralization by Devolution" yaani D by D. Mfumo huu nao ni vile vile unapeleka madaraka karibu na wananchi. Mfano, halmashauri kwa sasa ndizo zinazopelekewa fedha nyingi kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika halmashauri husika. Labda mnisaidie, mfumo huu mzuri wa majimbo unakwenda mbali zaidi kuliko huu wa 'D by D'?
 
Back
Top Bottom