CHADEMA wamdhalilisha Wema Sepetu

hawa wasanii washafanya siasa kama bongo movie, sababu kipindi cha kampeni Kuna bongo movie wawili walikuwa damu sana na mgombea uraisi wa chadema kwenye kampeni utaona wao ndo icon, asee walikuja kugeuka hadi nkashanga wakaenda kwa kijani kibichii anyway time will tell
 
NAWAZA TU:

Kuna vitu Nimeshindwa kuelewa kuhusu Wema Sepetu hivi mtu anayeonekana mashuhuri tena mwenye wafuasi Wengi,Kwanini press conference afanyie nyumbani kwao na siyo ofisi ya Chama walau hata mkoa?

Hivi kwanini mtu mwenye wafuasi Wengi Kama Wema Sepetu Kama ambavyo wafuasi wa chadema wanavyojinadi asipewe kadi hata na Naibu katibu mkuu wa Chama wala hata kuhudhuria shuguli na kumuachia meya?

Hata mwenyekiti wa Chama mkoa ameshindwa kuhudhuria Sherehe kumkabidhi kadi msanii mwenye wafuasi milioni mbili kama wafuasi wa chadema wanavyojinasibu?

Naona kama CHADEMA wamemdhalilisha Wema Sepetu Kwa kumtuma meya Ndiyo apokee kadi
Wema Sepetu Pamoja na umaarufu wako wote unakabidhiwa kadi na Diwani wa Kata?

Nikitazama Ili Ndiyo Naona kupotea kwa wema Sepetu ktk siasa inaonesha kuwa viongozi wakuu wa chadema hakumwamini wema Ndiyo maana wamejitenga naye.

Stay tuned
Na Frey Cosseny
Du pole sana. Nahisi umeumia sana na hizo development. Get a life....
 
Kwahiyo Rais Magufuli anapokuwa na Ugeni wa Rais mwenzie kisha anamtuma Waziri Mkuu Majaliwa au Waziri wa Mambo ya Nje Mahiga waende kumpokea nae anakuwa amemdhalilisha huyo Rais mwenzie? Wewe ratiba za Viongozi Wakuu wa CHADEMA unazo? Kwani Wema Sepetu alikuambia kuwa akiwa leo anahamia huko CHADEMA anataka Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA awepo? Nachukia sana Watu hopeless na wasio na Hoja zenye Mashiko mbele ya Great Thinkers wa JF.
Umemjibu inavyostahili, japo wewe ni ccm pure umeweka mihemko kando!!..
 
Haiendani na mtu mwenye wafuasi m 2 apokelewe na diwani. Sisi kwetu alikuwa mwanachama wa kawaida Sana. Kwenu ndio habari Ya mjini. Nawapa wiki mbili story za wema zitakuwa kwishiney. Watz tutakuwa na kitu kingine cha kuongelea.
Wiki mbili zote za nini Mkuu??

CDM ipo busy na mambo mengi ya msingi.
Imuongelee Wema kwa wiki 2??

Tunataka kujua majina halisi ya rc wa Dar. Ni Daudi Albert Bashite au Paul Christian Makonda??
Hii ndio habari hot kwa sasa.

Na wala haihusiani na vita ya madawa ya kulevya, afterall vita yenyewe ya madawa ya kulevya ni hewa.. Rather hii ni case ya FORGERY...
Duu kumbe Dsm inaongozwa na kilaza..!!
 
hawa wasanii washafanya siasa kama bongo movie, sababu kipindi cha kampeni Kuna bongo movie wawili walikuwa damu sana na mgombea uraisi wa chadema kwenye kampeni utaona wao ndo icon, asee walikuja kugeuka hadi nkashanga wakaenda kwa kijani kibichii anyway time will tell
....
....tulia na maumivuu
 
Wafuasi 12M wa Wema sio lazima wote wawe shabiki wa chama anachokipenda kisiasa. Wengi wao ni wanawake ambao ndio mtaji wa wale jamaa wa mavazi ya kijani. Chadema ijipange isibwete na tukio hili lazima wajifunze kupitia umati ule wa babu Mamvi wakati wa kampeni na matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2015. Sio kila shabiki atawapa kura yake.
 
Umemjibu inavyostahili, japo wewe ni ccm pure umeweka mihemko kando!!..

Huwa sipepesi, sitikisi wala simung'unyi kulisemea jambo fulani liwe shubiri Kwangu au tamu kwa wengine bali siku zote nitabaki kuwa katikaki. Kuna zaidi ya kuwa Mwana CCM au CHADEMA ila muhimu ni Tanzania yetu itoke hapa ilipo na tukimbizane na waliotuacha siku nyingi sana.
 
NAWAZA TU:

Kuna vitu Nimeshindwa kuelewa kuhusu Wema Sepetu hivi mtu anayeonekana mashuhuri tena mwenye wafuasi Wengi,Kwanini press conference afanyie nyumbani kwao na siyo ofisi ya Chama walau hata mkoa?

Hivi kwanini mtu mwenye wafuasi Wengi Kama Wema Sepetu Kama ambavyo wafuasi wa chadema wanavyojinadi asipewe kadi hata na Naibu katibu mkuu wa Chama wala hata kuhudhuria shuguli na kumuachia meya?

Hata mwenyekiti wa Chama mkoa ameshindwa kuhudhuria Sherehe kumkabidhi kadi msanii mwenye wafuasi milioni mbili kama wafuasi wa chadema wanavyojinasibu?

Naona kama CHADEMA wamemdhalilisha Wema Sepetu Kwa kumtuma meya Ndiyo apokee kadi
Wema Sepetu Pamoja na umaarufu wako wote unakabidhiwa kadi na Diwani wa Kata?

Nikitazama Ili Ndiyo Naona kupotea kwa wema Sepetu ktk siasa inaonesha kuwa viongozi wakuu wa chadema hakumwamini wema Ndiyo maana wamejitenga naye.

Stay tuned
Na Frey Cosseny
Nani amekwambia Wema ameshakabidhiwa kadi? Acha kujiaibisha.
 
Siasa za chuki za nini?kama kweli malengo yenu ni kupigania ustawi wa wananchi wote?sisi sote ni ndugu moja matusi na uhasama siyo dira yetu
 
Mzee Isaack Sepetu angejua angebaki tu njia kuu na mkewe wa kizungu na watoto wake akina Kiranga pale Oysterbay mtaa wa India. Hii sinema aliyoanzisha kwa mpango wa kando pale Uswazi Kijitonyama isingekuwepo leo. Mama na mtoto haijulikani nani afadhali maana sio class ya waziri wa Mwalimu na Balozi.
 
Kwakweli isee
 
Back
Top Bottom