CHADEMA Siwaelewi mnachokisimamia

Wakuu nmeamua kufunguka kwa hawa ndugu zetu CHADEMA kufuatia kukithiri siasa za matukio na kubadili gia angani. Yafuatayo ni baadhi ya matukio ambao aidha walibadili gia angani au yalipotea bila utekelezaji:
1. UFISADI; Mkiwa mwembeyanga mlituaminisha Lowassa ni fisadi, mlisimamia hilo kwa takribani miaka saba lakini ndani ya masaa mkataka kutuaminisha sio fisadi
2. ILANI YA UCHAGUZI; mlituaminisha kuwa Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA lakini hata mwaka mnasema ni dikteta. Nawasubiri mtengue kauli kwamba JPM hakuiga sera zenu
3. MSIBA WA ARUSHA. Mnatuaminisha kwamba RC wa Arusha amekula rambirambi lakini akihamia CHADEMA mtasema hajala rambirambi ila amekula pilau.
MY TAKE: Kuweni makini na watu wasiokuwa na hoja wala misimamo thabiti....Amini amini nawaambia Makonda akihojiwa Star TV ndo unakua mwisho wa stori za Mrisho gambo na upepo utabadilika itakua ni Makonda na Star TV.
Tujifunze kuweka akiba ya maneno
Acha kuleta hoja zilizo pitwa na wakati juha' wewe na unaacha mambo ya msingi ,tujadili kwanza kipaombele cha taifa na maendeleo ya watanzania kwa ujumla katika utawala huu wa sasa sio unakaza mk kujadili upuuzi wa wapuuzi wenzio maana hao chadema kwa sasa hawana serikali na wala hawana sera inayo ongoza taifa na kujadili kitu ambacho hakina tija ni ujinga pia.

ni mpuuzi pekee atakaye jikunja kujadili upuuzi wako na kuacha mambo ya msingi , labda wenye akili watakukosoa kwa ujinga ulio uleta hapa ila wajinga wenzio maana mnafahamiana watakuunga mkono maana elimu zenu wote za kuokoteza KK
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tumekusikia mla rambi rambi. Nyie mnakoelekea mtahamisha hata reli ili mpate rambi rambi.
Mejichokea sana mpaka mnavizia rambi rambi mziingize kweny matumiz ya serikali km kujenga hospital, kujenga shule n.k
Increment mkalala nazo mbele, watoka pabaya nyie. Kweli nyie Mafisi
Hii nchi ishakuwa ya ovyo sana. Hongera mkuu naona Rambi rambi za watu unazifanyia fujo humu na bundle za internet.
Wazee wa rambi rambi
 
Boss Barbarosa kwa maelezo yako, Tanzania hatuna haja ya kuwa na Chaguzi na Mfumo wa Vyama Vingi. Nilitegemea ungesema Upinzani watashindwa na sio hawawezi kushinda ukaenda mbali hata kwa miujiza.

My Take: Pelekeni Mswada Bungeni mfute Mfumo wa Vyama Vingi. Tunapoteza MaBillion kwa Mabillion kwa Chaguzi. Hizi pesa zingetumika kwenye matumizi mengine.

Hamuwezi kushinda Uchaguzi TanZania hata iweje, hata kama ikitokea Miujiza labda Watanzania siku moja wakawaamini na kuwapigia kura nyingi lkn bado hamtaweza kuiondoa CCM kwa maana mfumo wa Tanzania hauko tayari kwa hilo, na huwo ndiyo ukweli anzieni hapo kwanza, mengine yote ni kupoteza muda tu, ...
 
Tanzania siyo Nigeria, jaribu kuusoma mfumo wa Tanzania kwanza, CCM ni zaidi ya Chama cha Siasa!
Basi hakuna haja ya kûwa nauchaguzi na vilevile serikali inatoa ruzuku bila kumaanisha halfu mh tukisema tz hakuna democracy mbona mnakuja juu sasa yamekukuta yepi
 
Wagojwa wa akili mnashirikisha wenye akili.

Mimi nasema sawa na iwe hivyo . Muda utasema
 
Hamuwezi kushinda Uchaguzi TanZania hata iweje, hata kama ikitokea Miujiza labda Watanzania siku moja wakawaamini na kuwapigia kura nyingi lkn bado hamtaweza kuiondoa CCM kwa maana mfumo wa Tanzania hauko tayari kwa hilo, na huwo ndiyo ukweli anzieni hapo kwanza, mengine yote ni kupoteza muda tu, ...
Mkuu huenda una nia njema sana kulisemea hili, nimekuelewa sana. Hujakosea hata chembe kwa reference ya Zanzibar 2015. Asante sana mkuu!! Unachomaanisha ni kwamba kuna wang'anganizi wa madaraka na walafi hawako tayari juu ya hili. Iko siku Wapinzani watashinda,wananchi wataikataa CCM kwa wingi sijui watafanyaje, watatumia nguvu ipi? Yahya Jamee alijaribu hilo lakini leo yuko uhsmishoni.
 
Hamuwezi kushinda Uchaguzi TanZania hata iweje, hata kama ikitokea Miujiza labda Watanzania siku moja wakawaamini na kuwapigia kura nyingi lkn bado hamtaweza kuiondoa CCM kwa maana mfumo wa Tanzania hauko tayari kwa hilo, na huwo ndiyo ukweli anzieni hapo kwanza, mengine yote ni kupoteza muda tu, ...
Vipi umekalia nini hapo saizi? Sio rungu nyama kweli wewe Lumumba.?
 
Halafu mleta mada anaweza kuwa ni msomi na elimu yake haisadii nchi, ukweli ni kuwa humo serikalini ndiyo hakuna mawazo ya kuisaidia nchi zaidi ya kuendekeza ukereketwa wa chama na kuifanya kama dini.

Yoote uliodai dhidi ya CDM ni kinyume chake. Bali uongozi uliotoka uvccm wa kina Gambo na Bashite ni wa visasi.
 
Achana nao MWENYE Enzi MUNGU hadhihakiwi hata siku moja, APANDALO MTU NDIYO ATAKALOVUNA, YEYE NA KIZAZI CHAKE! Its about time and starting now! Tick tock!
 
Kauli zilizowahi kutolewa na mmiliki mwenza wa Chadema Lowassa kwamba yeye ameshikilia amani ya nchi kwani watu kwa kauli yake wanaweza kuingia mitaani siyo kauli ndogo

Namhusisha pia na Maalim Seif kwamba vijana wanamsumbua wakitaka awape ruhusa walianzishe hiyo kauli aliitoa alipokuwa anahojiwa na kituo kimoja cha luninga.

Lowassa amekuwa akiirudia kauli hii kila apatapo nafasi kuelezea uchaguzi wa 2015 alivyotolewa kamasi.

Kinachoendelea Arusha kuhusu suala la watoto wetu waliofariki ni jambo la aibu kubwa ambapo Watanzania wenzetu viongozi wa siasa za upinzani wameshiriki kwa kiwango kikubwa kwenye aibu hii. Badala ya kuwafariji wafiwa na kuwaacha watoto wapumzike kwa amani watu hawa wamekuwa wakielezea umma propaganda za rambirambi za wafiwa huku wakijipa kazi ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu za rambirambi hio.

Sasa maombolezo yamegeuka mtaji wa kisiasa. Nakumbuka kauli ya Lema alipokuwa anaelezea kutopata nafasi kusema lolote uwanjani, alisema ....Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama nchi na Syria ni wakati.... (Mwisho wa kunukuu). kwa wenye akili ya kutafakari unajua anachokitafuta Lema ni kuona nchi inaingia kwenye machafuko.

Mchungaji Msigwa (Mbunge) aliwahi kuonyeshwa katika video mitandaoni akitaka kutekeleza kwa vitendo sera ya chama chake kutaka kumpiga mkuu wa Wilaya Richard Kasesera....

Turudi kwa Sugu (Mbunge) amekuwa mara kwa mara akitaka kupigana ndani ya Bunge pale anapoona jambo analolazimisha kukataliwa.

Halima Mdee naye hivi karibuni amejadiliwa na Kamati ya Nidhamu na Hadhi ya Wabunge kwa kauli zenye uchu wa vurugu na kulivunjia heshima Bunge alizozitoa wakati Bunge linaendelea.

Inawezekana haya yanayofanyika leo watu wasijue nini hatima yake lakini ni wazi hawa ndugu zetu hawapo tayari kudumisha amani na mshikamano wa nchi yetu. Wapo tayari kuona watu wakifarakana na inawauma sana wanapoona serikali inatimiza wajibu wake ndiyo maana wanajitahidi kuchafua hali ya hewa kila inapobidi ili kuondoa utulivu wa kisiasa.

Mitandaoni hali ni tete kabisa, vitisho, kebehi hata wananchi ambao wengine walionyesha kushangilia pale polisi wetu walipopoteza maisha wakiwa kazini hata wengine waliokamatwa kwakuwatukana viongozi walijitokeza mawakili kutoka upinzani kuwatetea mahakamani.

Sijasema ya Tundu Lisu maana kila mmoja anajua nini mefanya, anafanya na matarajio yake kwa amani ya nchi yetu.

Ni wakati sasa wa Watanzania kupitia viongozi wao kuungana kuleta maendeleo chanya ikiwemo kushiriki shughuli za kiuchumi na kuhakikisha wanatekeleza sera za umoja wa kitaifa.

Kinyume na hapo, nawaambia CHADEMA kuwa roho za watanzania wasiziweke rehani kwa uchu wao wa madaraka. Wafanye siasa safi
Takataka! Nonsense
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wakuu nmeamua kufunguka kwa hawa ndugu zetu CHADEMA kufuatia kukithiri siasa za matukio na kubadili gia angani. Yafuatayo ni baadhi ya matukio ambao aidha walibadili gia angani au yalipotea bila utekelezaji:
1. UFISADI; Mkiwa mwembeyanga mlituaminisha Lowassa ni fisadi, mlisimamia hilo kwa takribani miaka saba lakini ndani ya masaa mkataka kutuaminisha sio fisadi
2. ILANI YA UCHAGUZI; mlituaminisha kuwa Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA lakini hata mwaka mnasema ni dikteta. Nawasubiri mtengue kauli kwamba JPM hakuiga sera zenu
3. MSIBA WA ARUSHA. Mnatuaminisha kwamba RC wa Arusha amekula rambirambi lakini akihamia CHADEMA mtasema hajala rambirambi ila amekula pilau.
MY TAKE: Kuweni makini na watu wasiokuwa na hoja wala misimamo thabiti....Amini amini nawaambia Makonda akihojiwa Star TV ndo unakua mwisho wa stori za Mrisho gambo na upepo utabadilika itakua ni Makonda na Star TV.
Tujifunze kuweka akiba ya maneno
Upepo mbona ulishabadilika, wazee wa pepo za kusi
 
Back
Top Bottom