`Vunja Baraza la Mawaziri`
Ladaiwa kushindwa kuwajibuka pamoja
Changamoto nyingi hazijapatiwa majawabu
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Chadema, John Mnyika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa Baraza la Mawaziri wa Serikali ya awamu ya nne limedhihirisha kutokuwa na uwezo, umakini na uwajibikaji wa pamoja hivyo kimemuomba Rais Jakaya Kikwete kulivunja.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Chadema, John Mnyika, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari akielezea maamuzi ya kikao cha kawaida cha Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kilichofanyika siku mbili kuanzia Machi 3 hadi 4, mwaka huu wilayani Arumeru, Arusha. Mnyika alisema ili kunusuru hali tete ya uchumi wa nchi, migomo isiyokuwa na kikomo ya wafanyakazi na ugumu wa maisha unaowakabili Watanzania, Rais.
Kikwete avunje Baraza la Mawaziri kwa sababu mawaziri wameshindwa kuwajibika katika kukabiliana na hali ilivyo sasa nchini. "Serikali haielekei kuchukua hatua za haraka kunusuru uchumi wa nchi, kuongeza uzalishaji na ajira na kudhibiti mfumuko wa bei na ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi hali ambayo ni kinyume cha ahadi ya CCM ya maisha bora kwa kila Mtanzania na ni tishio kwa usalama wa nchi," alisema Mnyika, ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo.
Alisema inashangaza kuona kuwa wakati hali inazidi kuwa tete kutokana na kuongezeka kwa migogoro ya kijamii kama ardhi, madai ya madaktari, wanafunzi, walimu na makundi mengine ya kijamii, serikali imekuwa ikiendelea kushughulikia matokeo badala ya vyanzo vya migogoro inayoendelea yenye kuathiri ustawi wa nchi na maisha ya wananchi.
"Maamuzi ya Kamati Kuu katika mikutano iliyopita ya kutoa rai kwa Rais Kikwete kuziba ombwe la uongozi lililopo na kufanya mabadiliko ya msingi katika serikali yanapaswa kutekelezwa kwa haraka katika kipindi hiki ambapo vyombo vya serikali likiwemo Baraza la Mawaziri vinadhihirisha kutokuwa na uwezo, umakini na uwajibikaji wa pamoja," alisema Mnyika.
Alisema kutokana na hali ilivyo, Kamati Kuu imeielekeza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chadema kuisimamia kwa karibu serikali kupitia Mkutano wa Saba wa Bunge unaotarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 10, mwaka huu na kuwasilisha taarifa kwenye mkutano ujao wa Baraza Kuu la chama kwa ajili ya hatua zaidi iwapo mabadiliko ya msingi hayatafanyika kwa njia za kawaida za kibunge na kiserikali.
HALI YA KISIASA Huhusu hali ya kisiasa nchini, Mnyika alisema bado hatua kamili hazijachukuliwa na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuwawajibisha watuhumiwa mbalimbali wa ufisadi na kushughulikia udhaifu wa kiutendaji katika serikali na chama tawala pamoja na kutetereka kwa utawala wa sheria. Alisema Chadema inakemea tabia inayoanza kushamiri hapa nchini ya viongozi wakuu wa serikali kuchanganya shughuli za kiserikali na kazi za kisiasa za CCM kwa kutumia rasilimali za umma.
MABADILIKO YA KATIBA Kuhusu suala la sheria ya mabadiliko ya katiba, Mnyika alisema Kamati Kuu inaalika maombi na mapendekezo yatakayowasilishwa na Chadema kwa Rais kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba la mwaka 2012. Aliongeza kuwa hata hivyo, marekebisho mengine muhimu yanapaswa kufanyika katika awamu nyingine kuhusu Bunge Maalum la Katiba na hatua ya kutunga katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.
Alisema Chadema kitaendelea na mchakato wake wa kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuhusu haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi katika hatua zote ili kuwezesha umma kushiriki ipasavyo kutoa maoni kwa lengo la kuwa na katiba mpya na bora.
UCHAGUZI ARUMERU Kuhusu uchaguzi wa Arumeru Mashariki, Mnyika alisema Kamati Kuu imefanya mapitio ya bajeti na kuelekeza kuwa kampeni husika zigharamiwe kwa sehemu kubwa kwa kuunganisha nguvu ya umma badala ya kutegemea ruzuku ya chama. Aidha, alisema kiwango cha ukomo wa fedha zitakazotumiwa na Chadema katika uchaguzi huo kitatajwa baada ya kamati maalum iliyoundwa kushughulikia masuala ya matumizi ya fedha kwa kushirikiana na timu ya kampeni kutambua michango itakayopatikana kama zana, vifaa na nguvu kazi ya kujitolea kufanikisha ushindi kwa falsafa ya nguvu ya umma.
Alisema Kamati Kuu pia imeelekeza hatua hizo zichukuliwe pia kwa chaguzi za marudio za udiwani katika kata za Vijibweni (Temeke), Kiwanga (Bagamoyo), Kirumba (Jiji la Mwanza), Lagangabilili (Bariadi), Kiwira ( Rungwe), Chang'ombe (Dodoma), Msambani (Jiji la Tanga) na Liziboni (Songea). MBOWE KUZINDUA KAMPENI Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, atazindua kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Jumamosi wiki hii.
CHANZO: NIPASHE
Makamanda endeleeni kwa kuanzia Arumeru tupo pamoja.