CHADEMA mmefikia wapi mpango wenu wa kumshtaki JK Mahakama ya ICC?

pale walikuwa wanawapooza wanachama waliokuwa wanafatilia juu ya kuuzwa chama hawana lolote
Sasa hao wanachama wanashindwa kweli hata kuhoji.

Wanadhani mahakama ya ICC kama vile makahamaa ya ndizi kila mtu anaweza kwenda kufungua kesi.

Uwa napata wasiwasi sana na uelewa wa wafuasi wa Chadema Mbowe kawashikia akili mpaka wanatia huruma.
 
Dr.Dau ni mteule wa Benjamin Mkapa unamuingiza Mungu kwenye uongo wako acha mara moja.
Message sent and delivered.

Enzi za JK zilishapita Magufuli kasema tusifukue makaburi, unachofanya wewe ni kuyafukua na kuyapaka rangi.
 
Message sent and delivered.

Enzi za JK zilishapita Magufuli kasema tusifukue makaburi, unachofanya wewe ni kuyafukua na kuyapaka rangi.

Ni kweli hizi zama za Dr.Magufuli mpaka boss wako anaisoma namba yeye kahamua kwenye kumshtaki Rais Dr.Magufuli Kanisani siyo ICC tena msome kiduchu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemshitaki Rais John Magufuli mbele ya maaskofu kadhaa wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Mbowe amedai kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano imekuwa ikiwatimua watumishi mbalimbali wa umma bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza kupitia kampeni ya kupambana na ufisadi, inayotambulishwa kwa kaulimbiu ya ‘utumbuaji majipu’.

Akizungumza jana katika ibada maalumu ya shukrani kwa kumaliza uchaguzi mkuu salama, iliyofanyika kwenye Usharika wa Nshara wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT na kuhudhuriwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Frederick Shoo, na maaskofu wastaafu Dk. Erasto Kweka na Dk. Martin Shao, Mbowe alisema (wapinzani) hawaridhishwi na hatua ya serikali ya Rais Magufuli kuendeleza timuatimua na kuwasimamisha kazi watumishi wa umma 160 tangu aingie madarakani bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema wapinzani wako tayari kuipongeza serikali wakati wowote inapofanya mambo mazuri kwa manufaa ya taifa, lakini kwa sharti kwamba mara zote iwe inahakikisha sheria za nchi zinasimamiwa, mali na rasilimali za umma zinalindwa na kila kitu kinafanyika kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

"Kutokana na hali ya sintofahamu kutamalaki katika taifa kwa sasa, hakuna mtumishi wa umma aliye na amani kutokana na mfumo unaoitwa kutumbua majipu. Tunasikia watumishi wa umma wakifukuzwa kazi bila kusikilizwa.

“Mpaka sasa kuna watumishi 160 wamefukuzwa na wengine kusimamishwa. Lakini pia zaidi ya taasisi na idara za serikali zipatazo 20 hazina uongozi…hii si sahihi,” alisema.

Hahahahahahaa!!
 
Adhabu mnazopata toka kwa Magu zinawatosha. Kumbuka mlimpata Magu baada ya upinzani mkali...

Tumbuaneni mkichoka tunakuja kuwatumbua wenyewe....nchi mliifanya shamba la bibi...oneni aibu!
 
Ni kweli hizi zama za Dr.Magufuli mpaka boss wako anaisoma namba yeye kahamua kwenye kumshtaki Rais Dr.Magufuli Kanisani msome kiduchu.!!
Pro JK siku hizi mnatia huruma mnaanzisha vi thread vya kujifariji, hamjaamini tu kuwa enzi zake zimekwisha?

He has gone and he will never come back.
 
Ni kweli sijui Dau aliteuliwa na nani ila ninachojua alijenga msikiti ndani ya ofisi ya umma.

Sasa ya nini kudanganya kuwa eti aliteuliwa na Kikwete.

Safi sana kama kajenga msikiti ofisi za umma, kwani misikiti yote si inajengwa viwanja vya umma? Au na hilo ulikuwa hujuwi?
 
Pro JK siku hizi mnatia huruma mnaanzisha vi thread vya kujifariji, hamjaamini tu kuwa enzi zake zimekwisha?

He has gone and he will never come back.
Tamko lenu leo hii mnaita vi thread kweli hali tete msome tena hapa Mwenyekiti wenu mpya anavyoisoma namba.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amemtaka Rais Magufuli apunguze utumbuaji majipu. Adai inadhalilisha Watumishi wa SerikaliAlisema pamoja na kuwa CHADEMA wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawako tayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi.

“Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji.

“Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.

Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake.

“Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani lakini niwaulize sukari imeshuka bei au mchele umeshuka bei lakini kila siku tunasikia watu wametumbuliwa bila kuwa na tija kwa taifa,” alisema.
 
Chadema ndiyo walishaanda mpaka barua ya kumshtaki JK mmefikia wapi usiwaingize wananchi.
JK alijishitaki mwenyewe kwa wananchi kwa kitendo chake cha kuwaacha wananchi wanyonge wanyanyaswe na matajiri yanayoficha sukari, leo anahukumiwa na umma kupitia kwa Magufuli.
 
Adhabu mnazopata toka kwa Magu zinawatosha. Kumbuka mlimpata Magu baada ya upinzani mkali...

Tumbuaneni mkichoka tunakuja kuwatumbua wenyewe....nchi mliifanya shamba la bibi...oneni aibu!
Ni kweli bakora wanazopata pro JK hawatasahau ngoja Magu apate na kofia ya pili lazima waombe po.

Walipokuwa wanaimba wataisoma namba hawakujua what goes around comes around.
 
JK alijishitaki mwenyewe kwa wananchi kwa kitendo chake cha kuwaacha wananchi wanyonge wanyanyaswe na matajiri yanayoficha sukari, leo anahukumiwa na umma kupitia kwa Magufuli.
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mh. Freeman Mbowe ameitaka serikali kusitisha kutoa vibali kwa wafanyabiashara wakubwa vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani ambavyo vimetoa ajira kubwa kwa watanzania.Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mwamala, Bukene, Choma, Igurubi na mjini Igunga mkoani Tabora katika mikutano ya hadhara, mwenyekiti huyo wa Chadema amesema hatua ya waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kutoa vibali kwa wafanyabiashara wakubwa kuagiza sukari nje ya nchi huku akijua kuwa fika kuwa viwanda vya sukari vya hapa nchini vinayo akiba kubwa ya sukari kwa mahitaji ya ndani inalenga la kuviua viwanda hivyo. Akiwa katika kijiji cha Choma wilayani Igunga, mwenyekiti huyo wa Chadema ameilaumu serikali kwa kushindwa kusimamia bei ya mazao ya wakulima ikiwemo pamba na tumbaku na kusababisha wakulima kuwa maskini huku mwenyekiti wa taifa wa baraza la vijana wa Chadema ( Bavicha ) Patrobas Katambi akisema laiti utajiri wa raslimali za gesi na madini uliopo nchini ungetumika vizuri, hakuna mwananchi ambaye angebaki katika lindi la umaskini uliotokea.

Hapo Mbowe alikuwa na sura ingine leo hii tena ana sura ingine.

Teh teh teh!
 
Hahahahah ndiyo basi tena hawana hoja za kumshitaki jk hata wafanye nini watapata aibu sana.

Tangu mwanzo CHADEMA hawakuwa na nia ya kumshtaki JK huko ICC ila ilikuwa ni geresha tu kuwafanya mashabiki wa Lowassa wasifikirie kushindwa uchaguzi bali waanze kufurahi kuwa kuna kesi itafunguliwa dhidi ya serikali. Ni sawa kabisa na uongozi wa timu ya Simba baada ya kufungwa na kukosa matumaini ya ubingwa mwaka huu wakaja na madai kuwa watamrudisha Okwi wakati wanajua fika kuwa hilo hawatafanya. Na hapo kweli baadhi ya mashabiki wakafarijika na wakaacha kuongelea kufungwa.
 
Mkikosa majibu mnahamisha mada,ikihamishwa ya kwenu mnataka wanamjadala wasitoke nje ya mada. Mliahidi kumshtaki JK ,mmefikia wapi? JPJ hawezi kugombana na JK kwa ushawishi wa kipumbavu maana bila JK mgombea wenu angesalia CCM. Shikamoo Jakaya.

Jibuni swali mmefikia hatua ipi au utamaduni wa kubadili gia angani unaendelea ? na mwenye akili timamu aendelee kuwaamini ?
 
Hatumdharau kama si yeye kuwapa changamoto wala sahizi tusingekuwa hapa Maji I km wewe Mngeendelea kuiba by the way magu anakimbizana kwa ajili ya lowasa **** changamoto........... Hahaha anajua akienda kinyume wananji tunazungusha mikono..... And of course kura yangu na kizazi changu ni upinzani wazalendo sio mijizi ya ccm
Wananji - wananchi. Au labda ni wa kule kule Moshi?
 
Back
Top Bottom