Wanaukumbi.
Muda umepita sasa toka CHADEMA watoe tamko la kumshtaki Rais mstaafu Jakaya Kikwete ICC.
Tamko la CHADEMA hili hapa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kumshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mahaka ya uhalifu wa kivita wa ya ICC.
Taarifa ya kufikishwa ICC imetolewa na wakili wa CHADEMA, John Mallya ambapo alisema Rais Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kutokana na madai kwamba anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi .
Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Rais Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.
Mashitaka hayo yanakuja siku kadhaa tangu Rais Kikwete ailaumu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC.
Ameongeza kuwa barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Rais Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.