bokassa
JF-Expert Member
- May 19, 2007
- 401
- 11
Kwanza hata Lowasa kuna habari kuwa alionewa na inabidi arudishwe kwenye U-PM tu.
Mhn, mi sipo!!!!!!
Kwanza hata Lowasa kuna habari kuwa alionewa na inabidi arudishwe kwenye U-PM tu.
Nilisema kuwa jamaa alishindwa kupata uenyekiti UVCCM mkoa wa Dar-es-salaam sikusema Dodoma,amekuja kukanusha na kukubali kwa pamoja kuwa 'niligombea sikushindwa kwa vile jina lilikatwa sababu nilionekana mpinzani',sababu hiyo hakupewa na CCM ameitunga, walikatwa kina Malecela,Malima na Lowassa kwenye michakato ya namna hiyo hawakuambiwa wana chembe za upinzani.
Kitila hakuomba 2005 uenyekiti ilikuwa nyuma baada ya kuukosa uenyekiti wa mkoa wa Dar-es-salaam, akaenda NCCR na TLP, wewe ni mwandishi wa habari za utafiti ukipewa dondoo basi unachimba deep, kukusaidia wapi uanzie muulize Zitto Kabwe.
Jk ni mwenyekiti wa CCM sote tunamiini hivyo kama Ilivyo kwa Mbowe na Mbatia ni wenyeviti wa Taifa lakini sidhani kama wewe au mimi tunajua kadi namba zao kuthibitisha hilo.
John Komba ni mwanaccm au John Mnyika lakini mimi na wewe hatujui namba zao ila kuna ushahidi mwingi wa kimazingira kuthibitisha hoja hii.
vyama vyote vina regista ya wanachama wake ukienda huko utapata hadi kadi namba ya Kitila Mkumbo, alikuwa rais wetu wa UDSM kwa kauli hii ujue kuwa alikuwa mtu maarufu na anachofanya tulikifuatilia kwa makini.
Siasa inahitaji uvumilivu chama anachosema Tishio hivi(Chadema) ni nguvu na jasho la watu la miaka zaidi ya 14 hadi wamefika kwenye peak, kama kina Mtei au Mbowe wangekuwa nao wanabadilisha vyama kila mara leo tusingekuwa tunajadili Chadema wamefanya nini, 1995 Chadema walikuwa hawana mgombea wa urais na 2000 ilikuwa hakuna mtu na 2005 ilibidi Mbowe ajitose kufungua milango.
Ushauri kwa wanaoingia kwenye siasa kuwa kunahitaji uvumilivu na subira tusikimbilie kula bila kulima historia ipo na tutaitumia kuweka rekodi sawa pale zipopindishwa.
Fikiria, ndio washachukua innji. Kisha wanaanza kutimuana ktk baraza la mawaziri!! ikulu hapatoshi!!!!!. Duh!!!!!!
Kitila ameshasema ukweli wake hapa.....kwa nini tunamng'ang'aniza uwongo?
Kama issue ni kuwa mfuasi wa Mrema, hiyo haiwezi kuwa hoja. hata hivyo, ameikubali, lakini hajasema alikuwa mwanachama NCCR-Mageuzi.
Watanzania wengi wenye akili nzuri waliokuwa watu wazima enzi za Mrema walimuunga mkono, siyo kwa sababu ya uzuri wake hasa, lakini sana sana kwa sbabu walichoshwa na ufisadi wa CCM na Mrema ndiye alionekana mtu jasiri aliyeweza kuthubutu kuwatikisa CCM.
Tusisahau pia kwamba enzi za kuvuma kwa Mrema ndizo zilikuwa za wananchi kwa mara ya kwanza tangu 1965 kujisikia huru kuwapinga watawala. Kama wewe hukuwa upande wa Mrema enzi hizo, sitashangaa kukusikia leo bado uko nyuma ya mafisadi.
Mheshimiwa.
Sijasema kuwa ni ubaya kuhama vyama nimetoa mfano wa Mtemvu Abbas ni mbunge wa Temeke alianza Tadea 1992 akaenda UMD,NCCR,CUF na hatimaye CCM,Mtikila yuko DP na Ndesamburo yuko Chadema toka mwanzoni, James Mbatia hajabadilisha vyama kama Kitila.
mjadala wa Kitila umekuja baada ya mmoja wa wapenzi wa Chadema kusema kuwa Wangwe alikuwa NCCR na aliwasumbua huko. nikamjibu kwa kusema kuwa kwani Kitila Mkumbo alikuwa NCCR na TLP anasumbua?
Ni demokrasia kila mtu kuhamia chama anachokitaka hata iwe kila mwezi ila utulivu na subira vinahitajika sana kwenye siasa hata kwenye kazi za kawaida unaenda kwenye interview na kusema kuwa ndani ya miaka miwili umebadili kazi kumi, unawapa nafasi ya kukunyima kazi wakiamini utawakimbia kama ulivyokimbia huko kwingine.
somo hili litawasaidia wengi sana wanaopania kuingia kwenye ulingo wa kiasia kuwa kunahitajia uvumilivu na subira na tuwekeze sana kuliko kutegemea kuvuna, leo hii Mtemvu anaingia kundi la wanasiasa walizuunguka kwenye vyama vingi labda akifuatiwa na Kitila inaweza kuwa ni ishara ya kuonesha juhudi zao za kutaka mambo yaende vizuri ndani ya nchi yetu.
Kubwa jinga samahani sana kwa hili na wala sina maslahi na Wangwe ila haki lazima itendeke hata Saddam Hussein waliotaka kumuua waliweka mazingira ya kuhalalisha mauaji yao kama kumpeleka mahakamani wakati wamesha muhukumu.
naomba nishie hapa sitamjadaili zaidi RAIS wetu wa Daruso lakini kuyakimbia haya ndio baadae mtakuja kusema kuwa 'alikuwa mzigo' au alikuwa mvuta bangi au alikuwa ...... wa kisiasa.
Mi sisemi hivyo lakini najua muda si mrefu kuna watu wakiingia humu watasema ni kwa kuwa tu si mchaga!
hivi kweli mnafikiri ccm itaondolewa madarakani na vyama vya upinzani,labda miaka kumi na tano ijayo.watanzania waliowengi naweza kusema 90% hajajua kuwa maisha yao iliyaboreshwa ni lazima pawe na uongozi imara na uliobora,wengi wanapiga kura bila kujua kwa nini wanapiga kura.
huku kweli kusafisha maana sasa mtakuwa weupe kiasi ambacho hamchaguliki. au hamuuziki
ndugu zetu siasa si lelemama, sasa nnategemea mtafahamu wananchi watanzania wako makini ktk kuchagua nani awakilishe taifa.
hivi ikiwa mmeshindwa kuvumiliana na kuekana sawa kwa haya madogo ingekuwaje mbowea angekuwa rais na wange waziri mkuu ?
nnaamini mzee wa wapuki na kikundi chake hawana sifa za uongozi ni watu wanaoongoza kwa kutumia hisia badala ya maaarifa, poleni sana
wazee wengi wa chama chenu walikihama tukazungumza hapa mkajidai ooh ccm imewanunua. tumehonga mapesa.
oo makamba kachaguliwa ili awanunuwe wapinzani, sasa semeni na huyu tumemnunua.
nyinyi wenzetu kwanza kubalini bado ni wadogo nakwa kukusaidieni 2010 tutakuwekeni benchi nyote na kisha mtajifunza siasa huko nje maana kupata hivyo vijiruzuku kidogo tu mshaanza kuvutana mashati na kutofautiana kiasi hicho
kufa kwa chadema ni faida kwa ustawi wa demokrasia
wenyeviti wa vyama vingi vya upinzani ni kama miungu ukitaka ukione cha moto wakosoe, hivyo demokrasi ni ndogo ndiyo maana CCM itaendelea kongoza tu. Demokrasi ndani ya CCM IPO JUU na jamaa wanaweza kukosoana kwa kiasi kikubwa kulinganisha upinzani.
huo ni mtazamo wangu tu
Masaa machache baada ya Kamati Kuu ya Chadema kufanya uamuzi wa kumsimamisha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Chacha Wangwe (Tarime) KLHN ilipata fursa ya kuzungumza kwa kirefu na wahusika wote wakuu.
Mahojiano yangu na Bw. Tundu Lissu (Mkurugenzi wa Katiba na Sheria wa Chadema na Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania) yalielezea kwa kirefu ni kwanini Chadema walifikia uamuzi huo na nini kilichojiri. Mara baada ya kuzungumza na Lissu nilipata pia nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Bw. Chacha Wangwe kuhusu kufungiwa kwake na zaidi ya yote kuhusu madai yaliyoainishwa dhidi yake kwenye Tamko la Kamati Kuu hiyo.
Mahojiano hayo ambayo yamechukua karibu saa nzima yatarushwa kwenye KLH News exclusive kesho ili kila mtu aweze kufanya uamuzi wake yeye mwenyewe baada ya kuwasikia.
We bring the news, from the news makers!
Ungeweka ushahidi usingekuwa na sababu ya kuandika kitabu kizima. Watu hapa wakiona ushahidi huwa wanakubali. Sasa wewe unaeleza mengi lakini ushahidi hakuna na ndio maana bado watu wanakuuliza ushahidi wa madai yako hapa.
Masaa machache baada ya Kamati Kuu ya Chadema kufanya uamuzi wa kumsimamisha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Chacha Wangwe (Tarime) KLHN ilipata fursa ya kuzungumza kwa kirefu na wahusika wote wakuu.
Mahojiano yangu na Bw. Tundu Lissu (Mkurugenzi wa Katiba na Sheria wa Chadema na Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania) yalielezea kwa kirefu ni kwanini Chadema walifikia uamuzi huo na nini kilichojiri. Mara baada ya kuzungumza na Lissu nilipata pia nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Bw. Chacha Wangwe kuhusu kufungiwa kwake na zaidi ya yote kuhusu madai yaliyoainishwa dhidi yake kwenye Tamko la Kamati Kuu hiyo.
Mahojiano hayo ambayo yamechukua karibu saa nzima yatarushwa kwenye KLH News exclusive kesho ili kila mtu aweze kufanya uamuzi wake yeye mwenyewe baada ya kuwasikia.
We bring the news, from the news makers!