Watanzania wenye kuweza kununua sukari basi tununue kwa wingi tuwasaidie ndugu zetu wa vijijini kule sukari bado ni bei juu na vipato vyao viko chini.
Nawashauri tu Chadema. Wasiige mbinu mufilisi kama za CCM badilisheni Mbunu za kisiasa.
Nawashangaa sana CHADEMA. Naona kwa sasa hakuna vijana kama enzi za Kina Zito Kabwe na Enzi za kina Mbowe. Serikali ya CCM haijawahi kuwa rafiki kwa wapinzani. Wala msifikiri Magufuli ni dikteta la hasha huo ndio utawa wa CCM. Utawala unaotumia nguvu kuliko akili.
Utawala wa nguvu hauangushwi kwa nguvu unaangushwa kwa akili.
Tumieni akili kuirudisha serikali ya CCM kwenye mstari wa kuomba poo.
Wamevurunda mno mwaka huu hao CCM na wabunge wao ,wamepitisha bajeti mzigo mkubwa kwa mananchi. Sijui walikua wanajadili nini bungeni.
Serikali inaweka VAT kwenye pato la watoa huduma wa mitandao bila kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wake na namna hiyo VAT itaiavyolipwa.
VAT siku zote inamwangukia mteja sasa sijajua sheria imebadilika lini.
BAVICHA wapange mikakati mikubwa zaidi za kumkomboa mtanzania kifikra.
Bado watanzania wanaishi kishabiki.
Bado tuna ushabiki wa kidini dini.Ushabiki wa kikabila kabila . Ushabiki wa Kikanda kanda. Na ushabiki wa kichama chama bila kuweka mbele maslahi ya wananchi na Taifa.
BAVICHA wamesahau namna ya kuendelea kuwaunganisha wamachinga na watu wa bodaboda nchi nzima na jukumu hili sasa limebaki kwa UVCCM. Hili kundi ni la muhimu sambamba na wasomi wa vyuo na masekondari. Wasitumike tu kwenye maandamano na migomo inayoonekana kwa macho bali tafuteni mbinu za kisayansi.
Nakumbuka wakati fulani wanawake kenya walifanya migomo ya ajabu sana ili tu kufikisha ujumbe wao.
Sio lazima mfanye migomo ya kukimbizana na polisi.
Kwa sasa Polisi na CCM lao ni moja.
Na hata suala la Lugumi lilivyomalizwa kule bungeni ni dalili ya kuwabeba mafisadi ndani na nje ya mfumo huo. Usitegemee polisi wawapende wapinzani. Wapinzani nia adui mkubwa wa wezi wa rasilimali za umma. Tulisikia gazeti moja likiwataja baadhi ya vigogo wa polisi kumiliki mashamba zaidi ya heka mil.1 na nyumba 40 za kifahari Dsm lakini hakuna hata Mbunge mmoja wa CCM aliyesimama bungeni na kusoma lile gazeti na kumuliza waziri kuhusu ukweli wa tuhuma hizo. Na hatua gani zimechukuliwa kwa mmiliki wa gazeti kama ni uongo.
CCM Walikaa kimya mana aliyetuhumiwa ni msaidizi wa kuwapigania wazidi kutawala nchi kwa ujanja ujanja.
Chadema kianzi kujiimarisha kwenye uongozi wa Mikoa ,wilaya ,Kata,vijiji na vitongoji.
Wanze pia kujenga ofisi ya makao makuu ya taifa.
Tena Rais aliwapa wazo zuri sana kwamba wahamishie makao Makuu ya CDM Dodoma. Ushauri ule ni wa muhimu sana.
Ukipita huko vijiji na hata mawilayani CHADEMA hawana ofisi kabisa. Sasa wanazungumzia mambo yao wapi? Mikakati yao inafanyikia wapi?
Chama hakiwezi kujengwa barabarani.
Kwa kweli itakuwa ni vigumu sana kwa polisi na Bavicha kwenda kwenye jengo la CCM na kuzuia mikutano ya ndani ya CCM. Mikutano inafanyika kwenye jengo lao la chama. Hapo ndio nyumbani kwao huwezi kuwazuia wasiingie kukaa kwenye majengo yao.
CHADEMA jengeni kumbi zenu za kitaifa na ofisi kila kijiji. Ni rahisi kwani watanzinia wanajitolea sana kujenga maabara na madawati ,wanakua tayari pia kujenga ofisi za chama hasa wakimtumia Lowasa na Sumaye kuhamasisha michango ya ujenzi wa maofisi ya chama inawezekana.
Ofisi za Chama huwa ni alama ya umoja na sehemu ya kuweka vijiwe huko vijijini hata vya kuuza na kunywa kahawa, kucheza drafti, kucheza bao wakati wa jioni na kujadili masuala ya kimaendeleo na sera za chama.
Ni ushauri tu wa bure kabisa. Ni kutokana na mahaba yangu kwa Demokrasia na utawala bora.
Tusipoishauri CHADEMA na wapinzani namna bora ya kuendesha siasa basi kuelekea 2020 hivi vyama vitakufa vyote isipokua vile vichanga kabisa visivyo naadhara kwa CCM vitanufaika kwa kushirikiana na CCM kuua vile vikubwa.
Demokrasia ikitoweka Tanzania ni mwanzo wa kuingia kwenye machafuko kwani kuna kila dalili ya wachache wenye nguvu kuwatawala wanyonge wengi kimabavu.
Demokrasia kwanza.