bangi tupu
" CHADEMA IACHE UPOTOSHAJI KUHUSU MGOGORO WA CUF" TATIZO KUBWA KABISA LA CUF NI MAALIM SEFU"
Na Salum Chilwa.
-------------------------------
Kumekuwa na Taarifa Zinazotolewa Mara Kwa Mara na Baadhi ya Viongozi wa Chadema na Kuonekana Kuungwa Mkono na Baadhi ya Wanaojiita Viongozi wa CUF Upande Unaopingana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi - CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Hata Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye kwa Sasa amesitishiwa Majukumu yake na Kutakiwa Kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Chama hicho.
Taarifa hizo zimekuwa Zikidai na kuhusisha Mgogoro Uliopo ndani ya CUF na Mkono Wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Jambo ambalo Si Kweli na linafanywa Kwa Lengo la Kumchafua na Kumuondolea Heshima Profesa Ibrahim Lipumba na Kundi linalomuunga Mkono Kwa Kulijengea dhana itakayo aminisha Jamii ya Kitanzania Kwamba Kundi hilo linatumiwa na Serikali ya CCM na Vyombo Vyake Vya Ulinzi na Usalama ili Kubomoa Upinzani.
Katika Taarifa Iliyonukuliwa na Vyombo mbali mbali Vya Habari Vikimnukuu Mmoja Kati ya Wabunge wa Chadema na Naibu Katibu Mkuu wake Upande wa Tanzania Bara aliyoitoa Jana Katika Mkutano mkuu wa Kanda ya Kaskazini Unaoendelea Mkoani Tanga :
NANUKUU :
Mgogoro Unaoendelea Sasa ndani ya Chama Cha Wananchi - CUF Unasababishwa na Serikali na CCM na Una Lengo la Kudhoofisha Umoja Wa Katiba ya Wananchi ( UKAWA ) .
MWISHO WA NUKUU .
Katika Maneno Kama haya Watanzania Wana Mambo Memgi Sana ya Kujiuliza Kabla hawajakubaliana na CHADEMA na Vibaraka wao ndani ya CUF.
(1) CCM ndiyo Iliyoituma CHADEMA Ikamtukane Lowasa Majukwaani Nchi nzima na kisha Kumsafiaha ?
(2) Utaratibu Wa Kumteua Lowasa Kuwa Mgombea wa Ukawa ndiyo Ule Uliokuwa Ukifanyiwa Vikao na Kamati ya Kuratibu Umoja huo Kwa Takriban Mwaka Mzima ?
(3) Ni Lini Vikao Vya Maamuzi ya Kupata Mgombea Uraisi Vilikaa na Kulipitisha Jina la Mliyemwita Fisadi Papa ?
(4) Iko Wapi Taarifa yake Iliyowapa Ubavu wa Kumtakasa iliyowqtoa Hofu kwamba Lowasa si fisadi ?
(5) Kama !Mgogoro wa CUF Unachochewa na CCM ni nini Kilimuondoa Katibu Mkuu wa Chadema dakika za Mwisho ?
(6) CCM ndiyo Ilimtuma Maalim SEFU Kupuuza Maamuzi ya Kikao Cha Baraza Kuu Kilichoketi Zanzibar Mwezi wa August 2015.
(7) He ' CCM Ndiyo ilimtuma Maalim SEFU Kumdanganya Profesa Ibrahim Lipumba Kwamba anakwenda Kushauriana na Wanasheria wa Chama kisha anakwenda Kuitisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ?
(8)Au CCM ndiyo Ilimtuma Maalim SEFU Kukaa na Barua ya Kujiuzulu Bila Kuijadili Kwa Miezi Kumi na Kisha Kuitisha Mkutano wa Kujaza nafasi ya Mwenyekiti Kinyume na Katiba ya CUF ya Mwaka 1992 Toleo la 2014 na Kusababisha aliyejuzulu Kuandika Barua ya Kutengua Kulinda Matakwa ya Katiba ?
NI Busara tuwaache watanzania Watafakari na Kuamua na Si kutumia midomo ya Upotoshaji kuwafikirisha watanzania mambo ambayo hayana Ukweli , CUF na CHADEMA ni Vyama vya Siasa vilivyosajiliwa kwa Mujibu wa sheria za nchi na Vinazo Katiba ambazo zinapaswa kusimamia uendeshwaji wa Vyama hivi na Si Mabavu kana kwamba Vyama hivi Vilianzishwa ili Viongozi na Wanachama Wake wavitumikie Kwa Maslahi ya Wanaojiona Wamahaki navyo Zaidi Kuliko Wemgine.
Ni Busara Mnaochukia Mgogoro Unaoendelea CUF Wakatafakari na Kutoka na Lugha Zitakazosaidia Kufubaza na Ikiwezekana Kumaliza na Si Kupotosha Kama Wanavyofanya CHADEMA Hali inayozidisha Shaka Kwamba Mgogoro Unaoendelea CUF ni Mpango wa CHADEMA Kukimaliza Chama Cha CUF na Kamwe Mpango huo hautofanikiqa ,
TUKUTANE 2020 TUKIWA NA CUF MOJA NA YENYE NGUVU MPYA.