Eric Ongara
Senior Member
- Sep 19, 2006
- 165
- 8
- Thread starter
- #21
- Ni kama vile ambavyo sijaona sababu ya huu ubora wa Chadema unaosemwa hapa, ubora wa chama cha siasa ni kwenye kura za uchaguzi mkuu kwanza, mara ya mwisho uchaguzi wa taifa ulipofanyika CCM ilishinda kwa miaka mitano, sasa tupo kwenye wa tatu na CCM imekuwa ikishinda for the last 47 years, huo ndio ubora wa chama cha siasa.
- Kama kuna ubora wa the last three years, tutauona kwenye uchaguzi wa 2010, kwenye uchaguzi uliopita ni CUF ndio walioshika namba mbili sio Chadema, CCM ndio chama tawala kilichochaguliwa na wananchi wengi wa Tanzania for the last 47 years, we can talk kuhusu viongozxi wachache ndani ya chama chochote cha siasa bongo, lakini as far as CCM so far hao viongozi wachache hawajaathiri mtizamo mzima wa chama,
- Ukweli ni kwamba mijadala ya namna hii ndani ya hii forum ni very low, lakini hatuna njia ila kujibu tu, ingawa ni very low kwa taifa!
FMES, natofautiana sana na wewe katika mjadala huu. Pamoja na kutambua uwezo wako wa kujenga hoja na uwezo mzuri wa kuchagua maneno sahihi katika kuyapa maandiko yajo mvuto, katika mjadala huu, kwa mtazamo wangu umepwaya sana kimantiki.
Ni kweli kuwa uchaguzi mkuu wa mwisho ulifanyika mwaka 2005 na kwamba ndio rejea ya mwisho ya uchaguzi mkuu.Unachosahau katika siasa kuna maisha baada ya uchaguzi mkuu, mara nyingi huwa tunavisakama vyma vya upinzani kuwa ni vyama vya uchaguzi na kuwa havifiki vijijini leo CHADEMA inajitokeza inafanya kazi yake vizuri sana, ni vizuri tuka waunga mkono kwa minajili ya kukuza demokrasia Tanzania.
Kumbuka mjadala ni kutathmini kazi ya vyama vya siasa mwaka 2008, kwa chama cha upinzani kina kuwa na wajibu wa kujiimarisha(kimuundo na ki-uwenezi) na pia kuiwajibisha serekali pale ambapo inajikwaa, CHADEMA wametekeleza vizuri sana wajibu wao huu. Lazima tuwe tayari kupima ufanisi wa vyama wakati ambapo hamna uchaguzi mkuu, je umihimu wao katika ustawi wa taifa unakuwa umehairishwa mpaka kipindi cha uchaguzi mkuu?
Pia umesema mijadala kama hii ni milaaini na haina umihimu wa uzito wa kutosha kujadiliwa katika eneo hili na kwamba haina umuhimu kwa taifa!Naomba kutofautiana nawe hapa pia.Napinga hoja zako kwa mtazamo kwamba:
1. Hili ni jukwaa la siasa, si rahisi kuepuka mijadala ya taasisi zinazofanya siasa!
2. Nakubalina nawe kwamba tunapaswa kujadili maswala mazito ya kitaifa na kwamba tutangulize maslahi ya taifa mbele. kuanzisha mjadala huu ni sehemu ya kuetekeleza hoja hii. Naamini kuna umuhimu mkubwa sana wa kukuza vyama vya siasa ili kuweka mazingira mazuri ya ushindani wa kisiasa na ukuaji wa demokrasia nchini kwetu.
Haya maswala mazito unayotaka tujadili yanapaswa kupokelewa na taasisi imara za kisiasa ili yaweze kufanyiwa kazi. Ikiwa tuna taasisi dhaifu za kisiasa hata tujadili mambo mazito kiasi gani bado hakutakuwa na matokeo tarajiwa, hivyo ni sehemu muhimu sana ya maslahi ya taifa kukuza taasisi zetu za kisiasa.Kutambua mchango wao na kuvipongeza vinapofanya vema ni sehemu ya kuvikuza!
Tunaweza kuwa na mijadala mizito sana ya masuala mbalimbali lakini kama hatutajenga taasisi imara za kisiasa kuweza kusimamia masuala haya tutakuwa tunafurahisha genge, kujiumiza kihisia na kutotoa mchango wetu kwa taifa kama inavyopaswa.
Kama wanaharakati wa demokrasia na wazalendo wa nchi, sambamba na kujadili masuala mazito kama ulivyopendekeza(na ninakubaliana nawe), tunawajibu wa kutengeneza mazingira mazuri ya demokrasia na kuimarisha vyama vyetu.Kutambua na kuwapongeza pale wale wanapofanya vizuri ni sehemu ya kujenga taasisi imara za kisiasa ambazo zitaweza kubebea vizuri masuala mazito tunayoyajadili hapa.
Leo hata bunge letu linapwaya kutokana na ubabe na uwiano mbaya baina ya wabunge na vyamba mbalimbali,kuwa na chama kimoja chenye nguvu kupindukia ni mazingira hatarishi kwa taifa. Ikiwa CHADEMA inatengeneza njia ya kurekebisha suala hili ni vyema tukawapongeza na kuhimiza wengine kufanya hivyo ili tuwe na siasa zenye afya zitakazochochea ustawi wa taifa letu kwa ujumla wake.
Lengo na kuanzisha mjadala huu msukumo wake si "Usimba na Uyanga" kama ulivyoainisha bali ni kutambua jitihada za CHADEMA katika ujenzi wa Demokarsia Tanzania. Niko tayari kujadli na kutafakari nawe kama kipo chama kilichofanya vyema zaidi ya CHADEMA mwaka 2008.
Asante