CHADEMA bila ya Tundu Lissu Bungeni ni sawa na Real Madrid bila ya Christian Ronaldo

Mleta uzi hafikiri vema na kwa maslahi ya taifa. Ni mjinga pekee anayeweza kushabikia upuuzi unaofanywa na naibu spika na kundi lake la uongozi wa bunge. Siioni busara katika maamuzi yao na ndiyo maana rais kasema wazee wa aina ya Mkuchika wanaiharibu nchi. Ni kweli hajaongopa.
Na watu wenye calibre ya lizaboni mnashangilia kupitishwa kwa sheria mbovu na mbaya kwa kusimamishwa kwa kina Lissu. Siyo makosa yenu bali ya mfumo mbovu mnaoutumikia usiojali taifa bali matumbo yenu.
Nilifikiri lizaboni ungehamaki kwa timu pinzani kuwakosa wachezaji mahiri wenye kuisumbua timu yako ili ukijue kiwango chake na uweze kukiboresha kwa mechi zijazo. Hujioni kuwa kuna mbinu utazikosa kutoka kwao? Mwambie naibu spika aache uoga na ushabiki usio na tija kwani kitendo chake hicho kinamjengea taswira mbaya kwenye jamii ya kistaarabu.
Awe fair kwani hata hao wenzake wa ccm wanamshangaa kwa kuachwa kuendelea na vikao.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Tundu Lissu ni kila kitu kwa CHADEMA ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuwepo kwake kunawafanya wabunge wengine wajiamini kwa vile ni yeye ndiye anayewaelekeza vifungu vya kusoma pindi wanapoomba Mwongozo wa Spika (Rejea Mwongozo wa Saed Kubenea juu ya wabunge kuvuliwa shanga). Kinyume chake, kutokuwepo kwake kunawafanya wabunge wa Upinzani wakose kabisa ujasiri si tu wa kuomba muongozo bali hata wa kuingia bungeni na kushiriki mijadala. Hivi uliwahi kuiona Real Madrid ya sasa ikicheza bila ya uwepo wa Christian Ronaldo? Jibu utakalopata lisogeze kwa CHADEMA bila ya Tundu Lissu.

Baada ya Tundu Lissu kuondolewa kutoshiriki vikao kadhaa vya bunge hadi Januari 2017, CHADEMA na kambi rasmi ya Upinzani watapata wakati mgumu sana bungeni. Hawatakuwa na ujasiri tena wa kuomba miongozo. Hawatakuwa na ujasiri tena wa kushinikiza jambo fulani bungeni. Hawatakuwa na ujasiri tena wa kuchangia hoja. Ujasiri watakaokuwa nao ni wa kutoka nje pindi mambo yanapowaendea mrama.

Natafakari sana hoja ya Mbowe kususia Bunge hasa baada ya akina Tundu Lissu kupewa adhabu hiyo. Ukiunganisha dots utagundua kuwa tatizo si Dr Tulia Akson bali tatizo ni akina Lissu kutokuwepo Bungeni. Najaribu kuwaza hivi ikitokea Dr Tulia akaongoza vikao vyote vya bunge nini hatma yake? Najaribu tu kuwaza na naamini pia na wewe msomaji unawaza kama mimi.

Hakika Lissu umeacha pengo kubwa sana ambalo hakuna wa kuliziba bungeni ndani ya Kambi ya Upinzani. Daima wana CHADEMA wanakulilia Tundu Lissu. Watakumiss sana kwa kipindi hiki hadi Januari 2017. Mwenyezi Mungu akujaalie ujasiri na utulivu huku akikujaza siha njema ili urejee tena Bungeni ifikapo Januari 2017

Bila Tundu Lissu bunge lote litabuma. Hata huko ccm hakuna kama yeye ndiyo maana alikuwa anaombwa ushauri na spika mstaafu Anna Makinda.
 
Mleta uzi hafikiri vema na kwa maslahi ya taifa. Ni mjinga pekee anayeweza kushabikia upuuzi unaofanywa na naibu spika na kundi lake la uongozi wa bunge. Siioni busara katika maamuzi yao na ndiyo maana rais kasema wazee wa aina ya Mkuchika wanaiharibu nchi. Ni kweli hajaongopa.
Na watu wenye calibre ya lizaboni mnashangilia kupitishwa kwa sheria mbovu na mbaya kwa kusimamishwa kwa kina Lissu. Siyo makosa yenu bali ya mfumo mbovu mnaoutumikia usiojali taifa bali matumbo yenu.
Nilifikiri lizaboni ungehamaki kwa timu pinzani kuwakosa wachezaji mahiri wenye kuisumbua timu yako ili ukijue kiwango chake na uweze kukiboresha kwa mechi zijazo. Hujioni kuwa kuna mbinu utazikosa kutoka kwao? Mwambie naibu spika aache uoga na ushabiki usio na tija kwani kitendo chake hicho kinamjengea taswira mbaya kwenye jamii ya kistaarabu.
Awe fair kwani hata hao wenzake wa ccm wanamshangaa kwa kuachwa kuendelea na vikao.
Naibu Spika hakuna anachoshabikia, anasimamia Kanuni. Wanaoshabikia ni wale wanaotoka nje ya Bunge.
 
Naibu Spika hakuna anachoshabikia, anasimamia Kanuni. Wanaoshabikia ni wale wanaotoka nje ya Bunge.

Ushabiki una sura nyingi mkuu..........nakwambia anashabikia CCM

naibu%2Bspika.jpg
 
Bila Tundu Lissu bunge lote litabuma. Hata huko ccm hakuna kama yeye ndiyo maana alikuwa anaombwa ushauri na spika mstaafu Anna Makinda.
Spika siyo wa CCM , ni wa wabunge wote, Makinda alikuwa na haki ya kuomba ushauri kwa Mbunge yeyote yule. Na kuomba ushauri haimaanishi huyo ndiye anajua kuliko wengine. Ila kwa Chadema Lissu ni muhimu hauoni wanavyohaha?
 
Back
Top Bottom