CCM wanamhujumu Lowassa

swali hili kamanda ingekuwa busara kwanza ungewauliza Lissu Tundu ,Dr Slaa, team Mbowe yote bila kusahau Kubenea. hawa wazee walijigamba wana ushahidi wote kuwa Lowasa ni fisadi. rejea magazeti ya Kubenea, magazeti ya kiuchunguzi wa ukweli kama alivyojitapakaga. list of shame ikiandaliwa na nani kwani? ? na tueleze kwa nini iliondolewa kwwnye mtandao wa chadema yetu. msituchanganye makamanda tusije tukatoa matusi hapa
Walishindwa kuthibiyisha ndo maana wamenyamaza, weye unoendeleza kelele toa huo ushahidi, pia Wewe tukana tu wala hutotupandisha mori,
 
Lowassa ni madini ktk hii nchi kwa bahati mbaya tumeshindwa kumtumia, lkn atakumbukwa vizazi Na vizazi mtumishi huyu
uko sahihi kabisa, kuwa huyo jamaa ni mtendaji mzuri sana, tatizo lake anakashfa nyingi sana za kulihujumu taifa hii. hilo.
off topic; nimeimisi sana ile avatar yako!
 
ujinga nikuamini maneno ya ccm kuwa alikataliwa na Nyerere,utafikiri Nyerere aliiumba dunia ya Tanzania na hao walio kubaliwa na Nyerere ndio yaliyo filisi na kuuza mali zote za watanzania,refer kilio cha mwalimu baada ya Mkapa kuuza NBC,alie kataliwa na Nyerere alisimamia na kuhakikisha Shinyanga,Kahama na mikoa yote jirani na kanda ya ziwa wanapata maji safi na salama,watoto wa masikini wanaenda shule kwa kuasisi ujenzi wa shule za kata kwa nguvu za wananchi wenyewe,na hizi shule zimekuwa mzigo nikwasababu waliopokea hiyo idea hawa kuwa na maono mapy,a hawa kuwa na mbinu mpya za kuhakikisha alipo ishia mzee Lowassa atakae mpokea aanzie wapi na kuhitimisha wapi,wao wakawa wanaenda tu,ndio tatizo lakuigilizia unacopy mpaka jina na sahihi ya jirani..!!Lowassa anamaona sana ni msaada mkubwa kwa taifa hili
 
uko sahihi kabisa, kuwa huyo jamaa ni mtendaji mzuri sana, tatizo lake anakashfa nyingi sana za kulihujumu taifa hii. hilo.
off topic; nimeimisi sana ile avatar yako!
 
Hata monduli hana umaalufu, hvi kunawatu bado wanataja hlo jina,? M nikilisikia tu na jua ndo mpigaji mkuu kuliko wote waliowahi kuwepo, na huenda hawatakuwepo..
Umaalufu ndio nini? hii ndio product ya shule za kata zilizochakachuliwa .Pole
 
Hivi hela inayookolewq inaenda wapi si watugeie kitaa
hela ya ufisadi wa rada ya chenge iliyorudishwa na uingereza ilipigwa na manyang'au wengine wa CCM. maCCM yameifanya nchi hii ni shamba la mama yao.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Dr Edward Ngoyai Mollel Saitoti Ole Lowassa, ndiye alyekuwa kinara na muasisi wa shule za Kata. Pia alikuwa amekusudia baadaye kuanzisha Zahanati za Kata, kwamba kila Kata katika nchi hii iwe na Zahanati yake kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote.

Baada ya kugundua kwamba mikakati hii ingempaisha Dr Ngoyai kisiasa, CCM wakaamua kumuundia zengwe na hatimaye kumuangusha kutoka nafasi yake ya Uwaziri Mkuu kwa skandali feki ya Richmod. Hapa ndipo wakapata mwanya wa kuhujumu mikakati aliyokuwa ameiandaa Dr Lowassa kwa maslahi ya umma. Shule za kata alizozianzisha Dr Ngoyai zikatelekezwa na kuachwa solemba.

Badala ya kuboresha shule hizi, CCM wakaanza kuchakachua mfumo wa utahini kutoka madaraja ya awali na kuanzisha mfumo kanyaboya wa GPA. Lengo lilikuwa ni kuharibu kabisa mfumo wa elimu ili shule za Lowassa za Kata zionekane si lolote wala chochote, na hakika wamefanikiwa kuvuruga mfumo wa elimu yetu kwa hasara ya wananchi. Hapa ndipo serikali ya CCM ilipolifikisha taifa hili. Tazama jinsi wanafunzi wa shule za Kata walivyofeli mitihani yao ya mwaka 2015! Zaidi ya 98% ya wanafunzi wa shule hizi wamepata madaraja ya IV na 0!

Haya ni matunda ya CCM na serikali yao. Walilenga kumdhoofisha Lowassa kisiasa lakini wanaoumia ni watoto wa walalahoi wasiokuwa na uwezo wa kusoma kwenye shule za Akademi huku watoto wao wakisoma Ulaya na Marekani. Ipo siku kitakuja kunuka katika nchi hii, na hapo ndipo tutakapokuja kuheshimiana. Kumbuka kwamba chokochoko humchokoa pweza. Hizi chokochoko za CCM iko siku zitakuja kuwachokoa wananchi wenye hasira na kusababisha taharuki isiyokuwa ya lazima katika nchi hii ya Tanganyika.
Acha kunywa "ukawa"
 
Lowassa (Waziri mkuu aliyejiuzuru kwa aibu) hakuwa muasisi Bali mtekelezaji na msimamizi wa sera na mpango Wa maendeleo Wa serikali ulioandaliwa kulingana na ilani ya chama chake
 
Back
Top Bottom