Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,872
- 5,594
Vijana wengi sasa hivi wameanza kurubuniwa kwa kupewa ofa ndogo ndogo na kuanza kuchukua kadi za CCM.
Walengwa wengi ni hawa vijana wa bodaboda na makundi mengine ya kijamii.
Watu wameanza kuchukua kadi kimya kimya huku mitaani, hususani vijana.
Ikumbukwe uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika mwaka huu.
Vijana chagueni kiongozi bora bila kujali chama mgombea anachotoka, na sio kuchagua viongozi kwa kuangalia vyama.
Msifurahie raha za muda mfupi na kusahau Karaha za muda mrefu. Nyie bodaboda ndio uwa mnalia kila siku huko mabarabarani.
Fanyeni maamuzi sahihi wakati wa kuchagua viongozi kwa mustakabali mrefu wa Taifa letu.
Tanzania itajengwa na mimi na wewe, na Tanzania ikiyumba, sote tunayumba nayo