CCM Mnapeleka wapi Fedha mnazopata kwenye Makaa ya Mawe Ruvuma? Wananchi tunataka kujua mnalipa kodi kiasi gani? Mmefanya Mradi upi wa CSR?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
16,809
35,817
Kashfa kubwa zaidi ya Ufisadi Nchini Tanzania kuliko zile za EPA na ESCROW!!

CCM wanamiliki mgodi mkubwa sana wa Makaa ya Mawe Mkoani Ruvuma. Haifahamiki pia ni kwa namna gani na kwa taratibu zipi za manunuzi walipata leseni na haki ya kufanya mradi huu mkoani humo?
Screenshot_20250412_110342_Google.jpg

Kwenye mgodi huo ambao wanafanya uchimbaji kwa ubia na Kampuni moja ya nje ya Nchi, Makaa ya Mawe yanachimbwa kwa Masaa 24 na kuuzwa nje ya Nchi kwa kusafirishwa na maroli muda wote kuelekea Bandari ya Mtwara (Kwenda Bara la Asia) pamoja na nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.

Mwaka 2017 Nchi yetu ilipitisha Sheria za Ulinzi wa Maliasili za Nchi na Utajiri Asilia.

Moja ya vifungu katika Sheria hizo yanazitaka Kampuni za Madini kuweka fedha zao nchini na kulipa kodi stahiki.

Pia Sheria zile ziliwataka wawekezaji kufanya miradi ya huduma kwa Jamii kwa lazima.

Jambo linalosikitisha, Katika Mgodi wanaohodhi CCM huko Ruvuma, hakuna mwananchi anayejua wanalipa kodi kiasi gani? Hakuna taarifa za Wazi za Mapato yanayopatikana kutokana na Biashara hiyo wanayofanya ya Maliasli za Taifa.

Hakuna mradi wowote wa kijamii waliofanya. Hili likiwa ni takwa la kisheria kama zilivyopitishwa na Bunge. Vijiji vinavyozunguka mradi huo na Mkoa wa Ruvuma kwa pamoja wananchi wana umaskini wa kutisha.

CCM watoke hadharani waseme. Kwa nini wanawabia Wananchi wa Tanzania Maliasili zao? Kwa nini Wanachimba Madini ya Wananchi alafu hawalipi kodi Stahiki wakati wanauza madini hayo Nchi za Nje ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda na Bara la Asia na kupata fedha nyingi sana? Fedha hizo wanapeleka wapi?

CCM watoke waseme hadharani. Je kukamatwa kwa Tundu Lissu Mkoani Ruvuma ni kwa sababu aliongelea suala la Wizi wa Maliasili za Taifa ambazo ni mali za Wananchi kunakofanywa na CCM na wabia wao huko Ruvuma?

Tunasuburi majibu.

Mods. Naomba msifute huu uzi. Huu uzi ni very sensitive maana unahusu namna CCM wanavyowaibia Watanzania na kulifisadi hili Taifa.

Let's bring back JF ya 2000's
 
CCM wanamiliki mgodi mkubwa sana wa Makaa ya Mawe Mkoani Ruvuma.

Kwenye mgodi huo ambao wanafanya uchimbaji kwa ubia na Kampuni moja ya nje ya Nchi, Makaa ya Mawe yanachimbwa kwa Masaa 24 na kuuzwa nje ya Nchi kwa kusafirishwa na maroli muda wote kuelekea Bandari ya Mtwara (Kwenda Bara la Asia) pamoja na nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.

Mwaka 2017 Nchi yetu ilipitisha Sheria za Ulinzi wa Maliasili za Nchi na Utajiri Asilia.

Moja ya vifungu katika Sheria hizo yanazitaka Kampuni za Madini kuweka fedha zao nchini na kulipa kodi stahiki.

Pia Sheria zile ziliwataka wawekezaji kufanya miradi ya huduma kwa Jamii kwa lazima.

Jambo linalosikitisha, Katika Mgodi wanaohodhi CCM huko Ruvuma, hakuna mwananchi anayejua wanalipa kodi kiasi gani? Hakuna taarifa za Wazi za Mapato yanayopatikana kutokana na Biashara hiyo wanayofanya ya Maliasli za Taifa.

Hakuna mradi wowote wa kijamii waliofanya. Hili likiwa ni takwa la kisheria kama zilivyopitishwa na Bunge. Vijiji vinavyozunguka mradi huo na Mkoa wa Ruvuma kwa pamoja wananchi wana umaskini wa kutisha.

CCM watoke hadharani waseme. Kwa nini wanawabia Wananchi wa Tanzania Maliasili zao? Kwa nini Wanachomba Madini ya Wananchi alafu hawalipi kodi Stahiki wakati wanauza madini hayo Nchi za Nje ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda na Bara la Asia.

CCM watoke waseme hadharani. Je kukamatwa kwa Tundu Lissu Mkoani Ruvuma ni kwa sababu aliongelea suala la Wizi wa Maliasili za Taifa ambazo ni mali za Wananchi kunakofanywa na CCM na wabia wao huko Ruvuma?

Tunasuburi majibu.

Mods. Naomba minute huu uzi. Huu uzi ni very sensitive maana unahusu namna CCM wanavyowaibia Watanzania na kulifisadi hili Taifa.

Let's bring back JF ya 2000's
Gentleman,
huyo kibaka na tapeli anaesota korokoroni ndie anaejua vizuri,

nadhani ataijibu hiyo swali mahakamani baada ya Pasaka kuanzia tar.24.5.2025.🐒
 
Wamemwaga mboga, sie tunamwaga ugali na kuvunja jiko.
Tatizo ushahidi. Lisu vitu vyake vingi huongea bila ushahidi.

Mahakamani vyote alivyosema kavikana kuwa hakusema.Na hayo ya makaa mawe.yamo humo kwenye kukana kuwa hakusema

Utapiteza muda wako kutafakari mambo ya uongo yasiyo na ushahidi ya Lisu

Tafuta hela achana na Lisu
 
Ni vizuri ukajikita kwenye hoja iliyopo mezani na kuacha maneno ya shombo kuharibu mjadala.

Mind you!
Uzi huu unahusu mnavyolifisadi hili Taifa.
Gentleman,
unless hufahamu au hufuatilii mambo, akiwa pale mbinga Songea baada ya kuchangisha pesa kwenye kibakuli ambapo hazionekani zilipo mpaka sasa,
.huyo kibaka na tapeli wa kisiasa anae sota korokoroni mpaka sasa, alisema amehesabu malori zaidi ya mia2 yamebeba makaa ya mawe na akataja hayo malori ni ya nani na pesa nani anachukua nani,

ni muhim kusubiri kwanza tusherehekee Pasaka ndipo sasa, huyo muungwana aithibitishie mahakama dhidi ya uropokaji huo.

So,
nipo ndani tena ndani zaidi kwenye hoja mahususi mezani.
Na ikiwa umekasirishwa na ukweli huo, hiyo hainihusu mimi kabisa gentleman.

Mimi huwa naeleza mambo ya msingi tu 🐒
 
Tatizo ushahidi. Lisu vitu vyake vingi huongea bila ushahidi.

Mahakamani vyote alivyosema kavikana kuwa hakusema.Na hayo ya makaa mawe.yamo humo kwenye kukana kuwa hakusema

Utapiteza muda wako kutafakari mambo ya uongo yasiyo na ushahidi ya Lisu

Tafuta hela achana na Lisu
Mambo gani ya uongo yapo kwenye huu uzi?

Mgodi wenu wa Tujitegemee ulipo Mkoani Ruvuma umeingiza mapato kiasi gani? sema hapa?

Mmefanya mradi upi wa CSR kwa mujibu wa Sheria?

Kila siku mnafanya biashara masaa 24 kwa kuuza makaa wa mawe mnayochimba kupeleka Kenya, Uganda, Rwanda na mengine mnayasafirisha kwa meli kupitia Bandari ya Mtwara.

Tuambieni mnalipa kodi kiasi gani? Mnatoa Mrabaha Kiasi gani? Mnalipa kodi kwenye Halmashauri husika kiasi gani?
 
Back
Top Bottom