commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,956
Mkuu kilichozuiwa siyo mikutano ya siasa ila ni zile movement za nchi nzima,majimboni mnaruhusiwa kujiachia kwa raha zenu.Kuhusu hao wazee wetu wala hawatutishi,tunachotamani ni kuona upinzani ulio imara na kutoa matumaini kwa taifa,siyo njaa na kiu ya madaraka.
Ifike mahali mtu aone upinzani unaoweza kutawala na uliojiandaa kwa hilo siyo hizi habari za eti madaraka kwanza mengine yatajulikana mbele ya safari.Tumechoshwa na viongozi wala rushwa,wakwepa kodi,na wachumia tumbo.
NB,kumbuka ruzuku ni fedha za watanzania zifanye kile zinapaswa kufanya.

