Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 25,701
- 76,706
Kalamu ya: Leah D. Mbeke
Kutoka: CCM Makao Makuu
Neno falsafa ni neno la Kigiriki, ambapo mwanafalsafa ni mpenzi au mfuasi (philia) wa hekima (sophia). Mtu anayefanya kazi katika uwanja wa falsafa anaitwa Mwanafalsafa. Mwanafalsafa ni aina ya mtu wa fikra na mtafiti.
Rais Samia Suluhu Hassan alitambulisha FALSAFA yake ya 4R katika uongozi wake na anapenda kuitumia falsafa yake ya 4R ambazo ni Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reforms (Mageuzi), Rebuild (Kujenga upya) katika uongozi wake na pia amewataka viongozi wanaomsaidia kutumia falsafa hiyo katika kufikia uamuzi wa aina mbalimbali wa kiutawala na Kiuongozi.
Katika kuendeleza Utekelezaji za Falsafa hiyo, Maelfu ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa sehemu ya mkutano mkubwa wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt.
Emmanuel John Nchimbi Mkoani Mwanza, tarehe 15 Agosti 2024 wamemchangia Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Ndugu Tundu Lissu milioni Tshs.5,320,000/= ili amudu gharama za kutengeneza gari yake anayotumia kwenye shughuli zake mbalimbali.
Kitendo hiki, kimeonesha Uungwana, Upendo, Kujali na kwamba CCM inaposema Binadamu wote ni Ndugu zangu kwa mujibu wa ahadi na.1 ya Mwanachama wa CCM, huwa inamaanisha na bila kuathiri Itikadi zakisiasa!. Lakini pia, CCM imeonesha dhahiri shairi kuwa ni Chama kinachopenda Maridhiano, ni Chama chenye ustahimilivu, ni Chama kinachosadifu yaliyomo ndani ya Falsafa ya 4R katika Utendaji wake.
Soma Pia: CCM wamchangia Lissu Milioni 5 atengeneze gari lake. Lissu azipokea
Mwisho, Falsafa ya 4R inaweza kutumika kuanzia Mtu mmoja mmoja, ngazi ya familia mpaka Taifa, sekta binafsi na za Umma, Taasisi binafsi na zile za Umma yaani falsafa hii inagusa kila Mtu na kila eneo. Ni wajibu wetu kuhakikisha tunazisoma, tunazielewa, tunazifafanua na tunaziishi ili kufikia malengo tuliyonayo.
#MatokeoYenyeSauti