Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 747
- 1,608
Naona mambo yanazidi kunoga tu!
===============
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimeonya vikali watu wanaobeza maamuzi ya Mkutano Mkuu wa chama hicho ya kuwateua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kupeperusha bendera ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Aidha, chama hicho kimeonya dhidi ya upotoshaji wa taarifa zinazohusu maamuzi hayo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Daudi Yasini, ametoa onyo hilo wakati wa matembezi ya kuunga mkono maamuzi hayo, akisema kuwa uamuzi wa kuwateua viongozi hao unazingatia mafanikio makubwa ya utekelezaji wa ilani ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia.
Soma Pia: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Yasini ameeleza kuwa miradi mikubwa imetekelezwa mkoani Iringa, akitaja mfano wa mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi katika wilaya ya Iringa, unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 50. Amesema mradi huo unatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wakulima na kuchangia kukuza uchumi wa mkoa huo.