CCM inamdhalilisha Rais Samia

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,638
41,280
Bila aibu, baadhi ya viongozi wa CCM wanafanya vitendo vya kumdhalilisha Rais Samia.

Tumesikia kelele za baadhi ya viongozi wa CCM kuwa eti mwaka 2025, kwa upande wa CCM, itachapishwa fomu moja tu ya mgombea wa Urais, nayo atapewa Rais Samia.

Mimi nauona huu udhalilishaji dhidi ya Rais. Tafsiri ya kuchapisha fomu moja ni kwamba Rais Samia akishindanishwa, hawezi kushinda. Je, fikra hizo zina ukweli wowote? Kwa nini wamfanyie hivyo Rais Samia?

Ni nani hao ambao wanaamini kuwa Rais Samia akishindanishwa nao, hawezi kuwashinda? Ni hawa hawa wateule wake au kuna wengine?
 
Nashangaa nchi ya kidemokrasia, lakini CCM inaogopa kupingwa kijanja janja

Na hii ndio dalili ya wanayoyafanya hata kwenye uchaguzi dhidi ya vyama vingine

Ili tumpate Magufuli mwingine ni lazima kuwepo na upinzani mkali kuanzia ndani ya chama mpaka nje
Vinginevyo hapo tutapata mafisadi tu

Shame
 
Ngoja

Mkapa 2000 alishindanishwa na nani?

Kikwete 2010 alishindanishwa na nani?

Shujaa Magufuli 2020 alishindanishwa na nani?!

Niko pale......
Unafahamu yaliyo mtokea Shibuda 2010 pale Tabora Railway station akija Dodoma kuchukua form Dhidi ya JK?
Ndio zenu hizo mkisha ona mmeharibu na mnapingwa tokea ndani!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Nchi ina matahira wengi sana, jitu mpaka leo halijui hata utaratibu wa CCM mgombea anapogombea awamu ya pili.

Ngoja nikuulize mleta mada, eti una mtoto?
 
nchi ina matahira wengi sana, jitu mpaka leo halijui hata utaratibu wa CCM mgombea anapogombea awamu ya pili.

ngoja nikuulize mleta mada, eti una mtoto?
Hakuna mtu asiye kuwa na mtoto mkuu, 🤒🤒
 
JPM alifariki mwaka 2021 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kipindi chake cha pili na cha mwisho, cha miaka mingine mitano kuanza. Japo demokrasia ilibakwa katika ufachuzi wa 2020, lakini ushindi wake ndiyo uliokuwa unaenda kuhitimisha kipindi chake cha utawala wa miaka kumi ya awamu ya tano.

Kwa bahati mbaya kifo chake kilipelekea awamu yake ipokelewe na makamu wake. Huyu alikipokea kijiti ili kukidhi takwa la kikatiba katika kuihitimisha awamu ya tano.

Jambo hili lilikuwa ni kukidhi takwa la kikatiba la "transition of power" kwa kuwa mtawala aliyekuwepo madarakani alikiachia kiti chake cha urais. na Rais mpya ikapaswa akikalie kiti hicho kwa miaka minne iliyobakia. Awamu mpya hutokea kila baada ya miaka kumi ya utawala wa Rais aliyeshirikiv na kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu.
 
Bila aibu, baadhi ya viongozi wa CCM wanafanya vitendo vya kumdhalilisha Rais Samia.

Tumesikia kelele za baadhi ya viongozi wa CCM kuwa eti mwaka 2025, kwa upande wa CCM, itachapishwa fomu moja tu ya mgombea wa Urais, nayo atapewa Rais Samia...
NI mahaba ni mapenzi kwa raisi wetu, kwa mwenyekiti wetu ,kipenzi mwanamke wa pekee,Daktari wa madaktari Samia Suluhu Hassani mama wa kizimkazi tunataka kumshindanisha na Mbowe ndio mwenyekiti Lissu bado sana!
 
Mmmmmmhhhh!Kwa nini hamuachiani maji ya kunywa mezani?😎
 
JPM alifariki mwaka 2021 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kipindi chake cha pili na cha mwisho, cha miaka mingine mitano kuanza. Japo demokrasia ilibakwa katika ufachuzi wa 2020, lakini ushindi wake ndiyo uliokuwa unaenda kuhitimisha kipindi chake cha utawala wa miaka kumi ya awamu ya tano.

Kwa bahati mbaya kifo chake kilipelekea awamu yake ipokelewe na makamu wake. Huyu alikipokea kijiti ili kukidhi takwa la kikatiba katika kuihitimisha awamu ya tano.

Jambo hili lilikuwa ni kukidhi takwa la kikatiba la "transition of power" kwa kuwa mtawala aliyekuwepo madarakani alikiachia kiti chake cha urais. na Rais mpya ikapaswa akikalie kiti hicho kwa miaka minne iliyobakia. Awamu mpya hutokea kila baada ya miaka kumi ya utawala wa Rais aliyeshirikiv na kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu.
Katiba inahesabu kuwa 2021-2025 ni kipindi cha kwanza cha Samia. Ikiwa atagombea 2025 akashinda,akifika 2030 katiba haitamruhusu tena kugombea uraisi.
 
Bila aibu, baadhi ya viongozi wa CCM wanafanya vitendo vya kumdhalilisha Rais Samia.

Tumesikia kelele za baadhi ya viongozi wa CCM kuwa eti mwaka 2025, kwa upande wa CCM, itachapishwa fomu moja tu ya mgombea wa Urais, nayo atapewa Rais Samia.

Mimi nauona huu udhalilishaji dhidi ya Rais. Tafsiri ya kuchapisha fomu moja ni kwamba Rais Samia akishindanishwa, hawezi kushinda. Je, fikra hizo zina ukweli wowote? Kwa nini wamfanyie hivyo Rais Samia?

Ni nani hao ambao wanaamini kuwa Rais Samia akishindanishwa nao, hawezi kuwashinda? Ni hawa hawa wateule wake au kuna wengine?
CC: CHADEMA Board of Chairman Mpya Elections 2024.

CC: BAVICHA Board of Matusi Mtandaoni and Keyboard Warriors.

Wapenda Demokrasia wote.

Ujumbe Uwafikie.

Mapinduzi sio Ndani ya CCM pekee-Fanyeni mapinduzi haya CHADEMA.

Piiiiiiipoz.
 
Back
Top Bottom