CCM chukueni Hii ya Kagame 2030 Mgombea Urais awe na umri wa miaka 30-49

Sijajua Rais Kagame amewaza nini lakini nimeona ni ushauri Mzuri

Rais Kagame amesema mrithi wake wa uRais awe na umri wa miaka 30 hadi 49

Hii maana yake ingekuwa Tanzania uRais ungewahusu Akina Makonda, Mavunde, Jokate nk
Yeye anaachia lini, anataka asiyejua makando kando yake, na asiye na uwezo wakupambana naye au asiye na mtandao wowote wakumdburu
 
Anajua hao hawajui kina Cha historia nchi ilipotoka!!

Wakubwa zaidi ya hapo wanakumbuka Kwa kina Nini kilileta mauaji ya kimbari enzi zile!!

Uongo mwingi ndio unajulikana kuliko ukweli!!
Hivi unajua mauaji ya kimbali yameanza lini?. Usipende kuongea vitu bila utafiti. Mauaji ya Kimbali yameanza yangu Utawala wa King Kigali mpaka akaenda uhamishoni uingereza.
 
John, tunaongelea CCM ya watanzania sio Rwanda. Rwanda ni nchi ndogo sana kama mkoa wa, Kigoma.Kuiambia CCM ichukue ya Kagame ni kukidharau chama hiki. Nafikir wanaotakiwa kuchukua ya Kagame wapo na ni cdm na ACT. Ambao viongoz wao ni wa kudumu kama Kagame.
Punguza dharau wewe chawa. Ireland Ina ukubwa wa Mbuga ya Serengeti ila inatuzidi kiuchumi. Ukubwa wa eneo sio ukubwa wa maendeleo.
 
Nyerere alikaa muda gani madarakani?
 
Nyerere alikaa muda gani madarakani?
Nyerere alikaa muda wa miaka 23 kwa kuwa nchi ilikuwa haina wasomi wengi. Sasa, ni muda toka miaka ya Nyerere. Tusiwe viongoz wa kudumu, tuwe na taasisi za kudumu.
 
Punguza dharau wewe chawa. Ireland Ina ukubwa wa Mbuga ya Serengeti ila inatuzidi kiuchumi. Ukubwa wa eneo sio ukubwa wa maendeleo.
USA, Canada na China zina ukubwa wa eneo na pia zina uchumi mkubwa. Hata Tanzania ni wa pili kiuchumi EA. Hatulingani na viinch vya hovyo hovyo kama Rwanda , ambavyo ili vikue vinahitaji kuiba madini nchi za jirani.
 
Nyerere alikaa muda wa miaka 23 kwa kuwa nchi ilikuwa haina wasomi wengi. Sasa, ni muda toka miaka ya Nyerere. Tusiwe viongoz wa kudumu, tuwe na taasisi za kudumu.
Kwahiyo hiyo miaka 23 yeye ndio alikuwa msomi pekee? Na ww ukauziwa hiyo propaganda ukajaa!
 
Sijajua Rais Kagame amewaza nini lakini nimeona ni ushauri Mzuri

Rais Kagame amesema mrithi wake wa uRais awe na umri wa miaka 30 hadi 49

Hii maana yake ingekuwa Tanzania uRais ungewahusu Akina Makonda, Mavunde, Jokate nk
MUHIMU KUTOKA KWA KAGAME NI CCM KUBADILISHA KATIBA URAIS UWE MIAKA 7 NA RAIS AKAE VIPINDI 5
 
Sijajua Rais Kagame amewaza nini lakini nimeona ni ushauri Mzuri

Rais Kagame amesema mrithi wake wa uRais awe na umri wa miaka 30 hadi 49

Hii maana yake ingekuwa Tanzania uRais ungewahusu Akina Makonda, Mavunde, Jokate nk
Labda ndio umri wa yule kijana wake
 
Back
Top Bottom