Mkebora Jina lako zuri sana lov lakini unahasira sanaaaa, unajua wanaume walivyo kuna wakati wanapenda wawe treated like a Man, anyway huja chelewa am sure unampenda sana mr wako ndio mana umekua na wasiwasi na jazba.NImpende nani, hapana na nimesema pale juu kuwa tabia hii sijawai iona kwake, na ndio maana nilitaka nisiipe muda, kuna mambo mengine hayafai kuyachelewesha yanapotokea maana pindi unapoyachelewesha ndio yanakomaa zaidi, ni nini kilichomshinda mr. kutoa simu wakati namuomba ili nihakiki? kama simu alipiga alombebea mizigo kutoka bandarini kwanini hakunipa na alipata hofu ya kuendelea na safari mpaka akaamua kushuka njiani? nimekuelewa na asante kwa ushauri wako
kaondoe haki kasichana hakajielewi.Tena wakati mie mama hajawai ata kunipigia simu, ata hio kuniomba vocha aliomba kwa msg tu, ni ukaribu upi unaopelekea kumuuliza mr uko wapi? maana angempigia tu nakumuomba vocha ingekuwa pia tofauti na kuanza kumuuliza uko wapi? hivo wakaka upo na mkeo shamba boy anampigia simu anamuuliza uko wapi? naomba uninunulie vocha mtanyamazia tuu? na bado wife unamuuliza kakupigia nani hakuambii ukweli, utakuwa na hisia ipi?
nyie wanawake ndio huwa hamjielewi na hamjiamini pia,wakati wote mnahisia mbaya juu ya waume zenu,alafu tabia za kupeana simu kupekua pekua sio nzuri na siku zote zinaleta matatizo,hapo umeshaweka hisia mbaya kwa dada wa kazi na mumeo umemvunjia heshima pia, mimi wife alikuwa ananiletea habari hizo hizo,unakuta nimetoka anachukua simu ya dada ananza kunitumia msg oooh vp mbona hujaniaga,mara oooh mbona hunisalimii siku hizi kama mna wasiwasi na h/girl ni kwanini mnawaleta majumbani?na mnajijua hakuna kazi mnazoweza kufanya siku hiziHabari zenu wana,
Ijumaa nikiwa ofisini dada angu wa kazi alinitumia msg akiniomba nimtumie vocha anataka kuwasiliana na kwao, nikamjibu mazingira ya ofisini hapa hakuna duka hivo nitakununulia nikiwa narudi home na nitakuletea jioni.
Tukiwa njiani tunarudi home niko na mr simu yake iliita akaipokea sasa ilikuwa na sauti ya kusikika as if kaweka loud, sauti ya house girl wangu iliuliza uko wapi sasahivi? mr akajibu nipo njiani narudi nyumbani, yule dada akamwambia simu yangu haina pesa nashindwa kuwasiliana na nyumbani, mr akajibu sawa na simu ikaishia hapo, alipokata tu nikamuuliza mr. uliongea na nani? akaniambia na watu ambao walinibebea mizigo leo kutoka bandarini, nikamwambia ok, naomba simu niangalie akagoma kutoa simu.
Nilikuwa naendesha mimi so nikapark maana tulikuwa mtaani tu uko ambako uko free kupark popote, nikamuomba tena naomba simu niangalie, akafungua mlango wa gari na kushuka, kwa kawaida ikitokeaga issue kama hiyo anatoaga simu fasta bila shida akijua hakuna shida, same kwangu mimi nikiongea na mtu akitaka kujua ni nani uwa nampa simu aangalie.
Sasa hii ya juzi imenishangaza, niliamua kuondoka na nikafika nyumbani tu nikamuita dada, nikamwambia dada naomba simu nikuunge na kifurushi, dada akanipa simu, nikakagua simu yake hakukuwa na mawasiliano, japo namba zingine alizopiga zilikuwepo, ikumbukwe kwamba sio dada mshamba, ni dada wa kujielewa tu alieishi mjini na kijijini ana 20 yrs (hapa mr aliposhuka nilimuona anapiga simu wakati naondoka bila shaka akimwambia futa hizo calls) huyu dada mpaka hiyo friday alikuwa na siku 3 tu maana alikuja j5, niliona nisiishie hapo.
Usiku watoto walipoenda kulala nikawaita wote dada na mr. nikamuuliza dada una ukaribu upi na baba hapa ndani mpaka unampigia simu na kumuuliza yuko wapi na kuomba vocha wakati mimi ulishaniomba? Dada akasema mi sijampigia baba, nilimpigia siku nakuja tu kwa vile ndie alikuja kunipokea, nikamwambia dada umempigia baba nina uhakika sipendi hii tabia ukiwa na tatizo wakuniambia ni mimi, nikamwambia na mr kuwa hii tabia siipendi, naomba uniheshimu kama ninavyokuheshimu tukamaliza hapo.
Siku ya pili dada akaniita anashida anataka tuongee, nikamsikiliza akaniambia yeye imemuumiza sana kilichotokea hivyo anaona bora aondoke maana asije akaleta shida zaidi baadae, hajisikii amani, nikamuuliza na vipi ukiondoka utajisikia amani? Akasema hapana ila tu nakuhofia wewe maana utakuwa na wasiwasi na mimi, nikampigia kaka yake ambae alinipa huyo dada, nilipompigia na yule dada alikuwa ameshamtumia msg yule kaka yake kumwambia kilichotokea, hivyo yule kaka akaniuliza mimi kuwa sasa naamua vipi?
Nikamwambia dada amekataa kuwa yeye hajafanya hivyo na sio mfanyaji wa hayo kama anakiri maneno yake mi sina maneno ila pia kama anataka kuondoka pia sina maneno, yule kaka akamwambia dada yake kwa vile hapo haujafukuzwa mi naomba ukae, ila kaa kwa heshima, usije kunitia aibu mimi nilokuleta uko, kama haujafanya na una hakika hautafanya hayo basi kaa, kama unaona linaweza kutokea hili jambo basi unaweza kuondoka, dada akasema basi nitakaa kaka.
Mdada yupo home namuongelesha vizuri tu, ila nina hasira mno na huyu mr. tumekaa bila msichana 3 weeks hapo nyuma nimehangaika sana kuhudumia familia unarudi umechoka, unapika, unafua uniform za watoto, unanyoosha, unaosha vyombo unapanda kitandani saa 6 kasoro na saa kumi na moja umeshaamka, tunapata dada mchapakazi yeye analeta upuuzi, huyu mwanaume hajasema lolote mpaka sasa kuhusiana na hili na hapa tunapishana tu ndani.
Hivyo ubabe huu anaojitika ni wa nini? Niko nae huyu mtu 6 yrs now mambo haya sijawai yaona ndio kwanza kwa house girl huyu ila in short ukisikia wadogo zake kwao wana kesi na wake zao basi ni za kutoka na mahouse girl wao, hivi ni pepo au wapuuzi?
Naombeni ushauri wenu maana nimechoka moyo wangu unavonituma naona naweza kufanya jambo baya nipeni mwongozo.
Tafuta house boy atamchangamkia housegirl na hakuta kua na kesi hizo tena
Ni ruhusa kushikana...si kushikiana simu
Yaani Evelyn si unajua kupata binti ilivo shida sasahivi, sijui naanzia wapi kwakweli najisikia kuumia mno, binti ni mchapakazi, anaamka mapema, anafanya kazi zake vizuri na anaelewa alafu unakuja kumuharibu, wanaume tuhurumieni jamani
hahahahha kwa mwenye moyo wakuhimili atakayo yaona RUKSAAAA lol...mie siwezi na hisi kama sijiaminiNi ruhusa kushikana...si kushikiana simu
Dadangu kweli kupata bint wa kazi si rahisi sana, mke wangu ana mwaka sasa anatafuta bint wa kazi, kama ikitokea huwezi kaa na huyo mdada tafadhali ni juze ili mradi tu kama ulivyosema anachapa kazi. Hayo mengine kwetu hayana nafasi. Pole sana dadangu.Asante mkuu lakini issue pia kwanini alificha ile simu wakati yeye alipigiwa? si angesema tu ni dada wa kazi? sasa hii ya kuficha ndio ambayo imenipa maswali zaidi